Ng'azagala
JF-Expert Member
- Jun 7, 2008
- 1,288
- 222
Muda mchache uliopita nimesikiliza taarifa ya habari toka TCB-TV ambapo CCM imetangazwa kushinda kiti cha Ubinge-Bmulo. La kusikitisha na kushangaza matokeo rasmi hayajatangazwa hapa Bmulo. Hakuna kauli yoyote Zaidi ya mahojiano yaliyofanywa na Mkurugenzi wa Uchaguzi na Radio Kwizila ya Ngara ambapo Mkurugenzi alikiri CHADEMA kuelekea kushinda.
Sasa TBC inapomtangaza mgombea wa CCM kushinda ni kwa kura zipi? Zilizopigwa kupitia TV au mabox ya uchaguzi? Yawezekana kulikuwa na uchaguzi mwingine unaendeshwa kupitia TV!
Mkulu Invisible nawe uthibitisho wa matokeo rasmi umeutoa wapi?
Kwa sasa kinachofanyika ni propaganda. Invisible kuwa makini usijekuwa sehemu ya Propaganda Pima Upepo Tutekeleze Letu
pole sana Mkuu
labda wamepata kutoka Tume maana hapa taarifa tunazopata ni kuwa tume imetangaza ila chadema wamekataa na hivyo bado kuna malumbano