Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Muda mchache uliopita nimesikiliza taarifa ya habari toka TCB-TV ambapo CCM imetangazwa kushinda kiti cha Ubinge-B’mulo. La kusikitisha na kushangaza matokeo rasmi hayajatangazwa hapa B’mulo. Hakuna kauli yoyote Zaidi ya mahojiano yaliyofanywa na Mkurugenzi wa Uchaguzi na Radio Kwizila ya Ngara ambapo Mkurugenzi alikiri CHADEMA kuelekea kushinda.
Sasa TBC inapomtangaza mgombea wa CCM kushinda ni kwa kura zipi? Zilizopigwa kupitia TV au mabox ya uchaguzi? Yawezekana kulikuwa na uchaguzi mwingine unaendeshwa kupitia TV!
Mkulu Invisible nawe uthibitisho wa matokeo rasmi umeutoa wapi?
Kwa sasa kinachofanyika ni propaganda. Invisible kuwa makini usijekuwa sehemu ya “Propaganda Pima Upepo Tutekeleze Letu”

pole sana Mkuu
labda wamepata kutoka Tume maana hapa taarifa tunazopata ni kuwa tume imetangaza ila chadema wamekataa na hivyo bado kuna malumbano
 
Tazama kura hizo maana idadi yao iliyoandikishwa ni wengi na wamejitokeza wachache sana, Mimi nasema kuwa watu tumechoka kwa tabia ya kuigiza na mzee wa kisanii kama hii. afadhali kusiwe na chaguzi kabisa ,maana watu kupoteza muda. kila kitu ni cha CCM hivyo wanachofanya ni kitu kibaya kabisa katika taifa letu na wapemba demokrasia Duniani kote. Mimi naona kuwa CCM hawana tofauti kabisa na Mugabe japo wanamuona ni kituko
Mzee hivyo ndivyo...afadhali mugabe siyo mnafiki hawa CCM bado watajipendekeza kwa donors ...wameshawazunguka...sijui kama sauti zetu zitaungwa mkono ..obviously (viongozi wa upinzani) wafanye move ambayo italeta impact to the world media otherwise jamaa watatuumiza sana chini kwa chini..wapemba unakumbuka walichofanywa...afadhali mombasa ni karibu..
 
hivi kwanini Muungwana, hajahudhuria hata kampeni moja ya uchaguzi mdogo si kiteto, tarime, mbeya busanda, magogoni wala bhmulo au zote zinafanyika akiwa angani kwenda kualika wawekezaji kama Steve Seagal, barrick. Au anaogopa zomea zomea ya maskini
 
pole sana Mkuu
labda wamepata kutoka Tume maana hapa taarifa tunazopata ni kuwa tume imetangaza ila chadema wamekataa na hivyo bado kuna malumbano

jamani ebu ni habarishene vizuri maana naona mna nichanganya hapa.CCM wameshinda au hawajashinda? kama tume imetangaza CCM imeshinda kuna malumbano ya nini tena,si ndio kawaida yao kulalamika then wananyamaza?
 
2010 serikali haina majeshi ya kuweza kuzuia fujo bara na visiwani, na waamini wa ZNZ lazima watakiwasha na kikiwaka ZNZ na bara lazima kiwake
Mwakani kutakuwa na ratiba tofauti za uchaguzi za ZEC na NEC wewe utaona moja ya sababu itakuwa security ili wathibiti eneo moja la muungano wapange matokeo then waende eneo jingine ...I gues tusibiri tuone..
 
Mwakani kutakuwa na ratiba tofauti za uchaguzi za ZEC na NEC wewe utaona moja ya sababu itakuwa security ili wathibiti eneo moja la muungano wapange matokeo then waende eneo jingine ...I gues tusibiri tuone..

Ilishatokea hiyo Mkuu unakumbuka? na ina impact kubwa sana
 
Naona umenyofoa thread yangu.....umeigeuza update
 
kwa nini ccm ikishinda si democracy?

Haishindi inatumia janja ya nyani wajue wanajipalia makaa umeona mwenyewe haya malalamiko ,huu ni uwakilishi tuu ,ukeli ni kuwa hasira za watu wengi ziko kama unavyoshuhudia hapa
 
Quote: masatu
tehe teh teh!

Haya sasa wenye wivu chukueni kamba zenu mjimalize!

We do not need you attention anyway hypocrite Masatu!Na sidhani kama familia yenu(Masatu) ipo njema kiasi kwamba unafurahia sana kwa CCM kushinda Biharamulo,si ajabu wazazi wako ni sawa na wazazi wa watu wengi nyumbani TZ ambao wanakwenda hospitalini hukosa dawa,hamna maji saafi na salama ya kunywa na hata elimu labda ya wajomba zako kama si wadogo zako na kaka zako ni haba kiasi kwamba wanakaa chini kwa kukosa madawati!

Masatu CCM ina wenyewe na wewe sidhani kama ni mmoja wao,sisi na wewe wote"tumefulia"na kuiacha nchi hii ikiliwa na akina Kinje ambao hata hajawahi kufikiria kwenda Kenya tu hapo jirani kutafuta maisha maana hamna anachokosa TZ. Masatu si ajabu na wewe unaandika habari hii ukiwa nje ya TZ ulipoenda ama kama mkimbizi wa kipato au mkimbizi wa elimu au vyote kwa pamoja kwa maana CCM hamna walichobakiza nyumbani!

Nasisitiza tena 'shame on you Masatu'!Here we Go CHADEMA na hamjafanya vibaya Biharamulo wala Busanda ila tume ya Jaji Makame kwa amri ya JK kawapa ushindi CCM!

Masatu CCM waachie akina Masha,akina Ngeleja,akina Nauye na wote waliopo ndani ya CCM ambao faida yao kuwepo pale CCM ni kubwa!Masatu,What do you have for being die-hard CCM supporter?And worse still you dont have any potential to be in CCM cycle!

This dude makes me outspoken and i'm very sorry for any inconvenience guys/ladies

Ad hominem at its best! sasa Masatu kishakuwa mada! familia yangu, kipato changu, elimu yangu vinakuhusu nini wewe? I can be hypocrite but you are STUPID! kwa kutoheshimu demokrasia unayo jidai kuipigania.

CCM ina wenyewe granted! Chadema je? au wewe unatoka kwenye house of Mbowe, Ndesamburo, Mtei etc? Shame on you big and bad loser!
 
Ilishatokea hiyo Mkuu unakumbuka? na ina impact kubwa sana
Kwa ustaarabu wa kura tutasubiri sana mageuzi ya kweli...kwanini hawa viongozi wa upinzani (CUF na Chadema) wasiandae wananchi wa Tanzania tukafanya green revolution tunadai
a) katiba mpya
b) tume huru before 2010
Mimi naona wakati ndio huu everyone is so angry in this country maendeleo yatoke wapi?? kila mtu apigwa kivyake kama siyo kwa ufisadi basi kwa kura kuibwa nk...
 
Tume ya Uchaguzi imetangaza ndoto ya Kikwete aliyoota usiku. Kama unaamini ndoto za Raisi ni reality basi CCM wameshinda Biharamulo na Tume haijabadilisha matokeo ya baadhi ya vituo.
 
They are very crap!! No human in there; there plastics with a breath or unthinking robot; where death of its people is ceremony for them; shame on CCM and its alies; someone must get us out of these mud; we are stack; nation with no focus; im afraid the coming of this country; are these guys here and ready to kill ( if possible) their own people!! Shame on them in name of GOD
 
Last edited:
Kuamrisha Tume ya Uchaguzi kutangaza chama cha Rais kimeshinda ni utawala mbovu. Shame on you Kikwete!
 
Imejidhihilisha wazi kuwa ccm , ni nambari wani kweli kweli, Wana Kagera wameelimika hawawezi kuichagua ndio maana Chadema wameyakataa matokeo,

najiuliza na sisi wote tujiulize, kila mahali wanashinda wao na upinzani wanapinga, nani mkweli na nini kifanyike?
 
Wizi mtupu na ufisadi mpaka kwenye uchaguzi hivyo mambo yote yana mwisho wake
 
Back
Top Bottom