Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Ingawa matokeo rasmi hayajatangazwa, CHADEMA wameweza kuwashinda kwa karibu kabisa CCM kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Biharamulo hii leo.

Mpaka zinapatikana hesabu za mwishomwisho kukiwa bado kituo kimoja cha Nyabugombe B chenye wapiga kura 394 CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa 50.6% huku CCM ikiifuatia kwa karibu ikiwa na asilimia 48.8% ya kura zote na TLP ikiwa imejinyakulia 0.55% ya kura zote.

Matokeo yanatarajiwa kutangazwa rasmi punde

Lakini matokeo ambayo yamejumlishwa mpaka dakika hii ni haya:

CHADEMA: 17,313

CCM: 16,6682

TLP: 187

Turnout ilikuwa 39.24%
(incredible!)

Hicho kituo kimoja ndicho kitaipatia CCM ushindi wacha tusubiri filimbi ya mwisho.
 
Hongera sana CHADEMA kwa kuwagaraza CCM huko Birahamulo. Inaelekea kila jimbo wapiga kura wachache sana wanatumia haki yao, je hii ni kwanini?
 
I would advise John S. Malecela that it is time he started planning a graceful retirement from active politics.

He should be reminded of the old adage that CRIME DOESN'T PAY.

We observed the beating up of straggling young democrats in Busanda, the organization of which he backed or turned a blind eye to. That was criminal and unpardonable to a distinguished "servant of the people" aged 75.

I would advise JSM to follow the footsteps of those who have occupied positions similar to what he once occupied, like Cleopa David Msuya, Salum Ahmed Salum and even young Frederick Sumaye, who now move in dignity amongst citizens of Tz without the blemish of nipping Tanzanian democracy in the bud.

After all, as a former Prime Minister and Vice President of Tanzania, his pension for life is guaranteed by statute; he is to have a personal car, driver and bodyguard for life and can be treated at government expense in any Hospital abroad of his choice. What else could Tanzania give to demonstrate her gratitude?

In return and in order to ensure that Wananchi continue to earn as decent a living as possible so that they pay taxes for his enjoyment, we ask him to let them choose a vibrant Parliament, capable of curbing incompetence, corruption and irresponsibility in Government. In other words, give the people genuine freedom to choose their M.P.s.

Plan to retire gracefully, JSM. Dettach youself from thugs labelled as 'green guards', brandishing mapanga and simes against fellow Tanzanians. Urge the police, whom you control, to curb this hooliganism. This trend will taint your name in the history of Tz.
 
Nafikiri kutokana na ushindi huu wa CHADEMA na anguko kwa TLP, huu ni muda muafaka kwa Bw. Lyatonga Mrema kupumzika na kuwaachia vijana waendeleze TLP. Kama bado anahitaji kuendelea na siasa ni bora arudi SISIEMU alikotokea.
Mrema hata sasa hivi akiamua kugombea ukatibu kata kwa chama chake hawezi kupata kura za kumuwezesha kushinda huo uchaguzi.

Mrema, Kiraracha yakungojea, pumzika sasa.

Mkandara

Mambo ya wapinzani kwa kweli inabidi tuwe tunaongea kwa tahadhari kubwa sana. Mimi ndiyo maana nimeamua nifunge safari nije nione mwenyewe. kweli wapinzani wakiungana kuna nguvu kidogo itaongezeka lakini ukiwasikia maneno yao hutataka waungane tena hata kama ni kushinda uchaguzi kwani utajua kuwa wana malengo tofauti kabisa. nina baadhi ya crip za mrema itabidi niziweke hewani nikifika sehemu yenye speed kubwa ili mjionee wenyewe mliokuwa mnataka eti chadema wajiunge na na chama kama TLP

Jamani msisahau kuwa Mrema yuko kazini ati. Kwahiyo msitegee hata siku moja wapinzani wakapata nguvu through support ya Mrema. Ni usalama wa taifa yule na yuko huko kuwavuruga tu wapinzani.
 
Hahaha,

Sawa Yesu Mweusi, jaribu kujumlisha uone CCM itafikia wapi!

Nasikia TZ na Kenya kwa kubadirisha matokeo ya uchaguzi wamequarify kwa degree ya juu sana.

Kitu ambacho kilimpelekea Rais wa IRAN kabla ya uchaguzi wake kuja TZ na Kenya kuuchukuwa huo uzoefu na kwenda kui implementi nchi kwake. teh teh teh teh
 
Hongera sana CHADEMA kwa kuwagaraza CCM huko Birahamulo. Inaelekea kila jimbo wapiga kura wachache sana wanatumia haki yao, je hii ni kwanini?

Hili jambo la watu kuwa wachache kwenye hizi chaguzi limenitatanisha sana siku nyingi lakini pamoja na kuwa kwenye kumi na nane nimeshindwa kujua. swala la kununua shahada naona inakuwa ngumu kuliweka hapa kwani hata katika maeneo ambayo chadema wamefanya vizuri kwa mfano kituo cha Bisebo utaona kwenye kituo c wapiga kura waliotarajiwa ni 340 lakini walio jitokeza ni 192 na chadema wamepata 160 na ccm 32 na kwa mtizamo wangu hawa jamaa sizani kama wangeuza shahada.

nimejaribu kuwadadisi wenyeji nao hawajui kwa kweli na sababu wanazo hisi ni, vifo, movement za watu, watu kuona aibu kuwa hawajui kuandika na kusoma, uchaguzi mkuu kuwa na vinyang'anyiro vingi (uraisi,ubunge na udiwani) na baadhi ya watu bado hawaamini mfumo wetu ni kuwa ni huru hivyo kuhisi kuwa kura zao hazina maana
 
Mkuu Invisible,
16,6682
rekebisha kidogo hizo namba za CCM inaonesha kama laki moja hivi?
 
Hili jambo la watu kuwa wachache kwenye hizi chaguzi limenitatanisha sana siku nyingi lakini pamoja na kuwa kwenye kumi na nane nimeshindwa kujua. swala la kununua shahada naona inakuwa ngumu kuliweka hapa kwani hata katika maeneo ambayo chadema wamefanya vizuri kwa mfano kituo cha Bisebo utaona kwenye kituo c wapiga kura waliotarajiwa ni 340 lakini walio jitokeza ni 192 na chadema wamepata 160 na ccm 32 na kwa mtizamo wangu hawa jamaa sizani kama wangeuza shahada.

nimejaribu kuwadadisi wenyeji nao hawajui kwa kweli na sababu wanazo hisi ni, vifo, movement za watu, watu kuona aibu kuwa hawajui kuandika na kusoma, uchaguzi mkuu kuwa na vinyang'anyiro vingi (uraisi,ubunge na udiwani) na baadhi ya watu bado hawaamini mfumo wetu ni kuwa ni huru hivyo kuhisi kuwa kura zao hazina maana

Hata mimi siwezi kupoteza mda wangu kupiga kura kama unaamini wagomea wote ni feki,hiyo ndiyo sababu kuu.

Mfano 2010 kwanini nijisumbue kupiga kura kwa mgombea urais kama safu itakuwa hivi,JK,Mbowe,Mrema,Lipumba
 
Mpambanaji hakati tamaa...nafikiri nitapiga kura miaka yote kwa mtu na chama ambacho naona ni afadhali katika zilizopo??
Lazima kutakuwa na better evil in all evil (nakushauri piga kura mpaka kieleweka na tuhamasishe wengine wapige kura...that is the way we choose our future. kati ya JK,Mbowe, Lipumba, Mrema kuna better evil..go for that...
 
Hongera CHADEMA.
Wasukuma wanasema "aliwaye hakui", kazeni buti safari bado ndefu.
UMK
 
Mpambanaji hakati tamaa...nafikiri nitapiga kura miaka yote kwa mtu na chama ambacho naona ni afadhali katika zilizopo??
Lazima kutakuwa na better evil in all evil (nakushauri piga kura mpaka kieleweka na tuhamasishe wengine wapige kura...that is the way we choose our future. kati ya JK,Mbowe, Lipumba, Mrema kuna better evil..go for that...

Aisi kwa safu hiyo ni vigumu kunihamasisha ,maana nikama unanihamasisha ili ni isaliti akili.

Hii ni sawa na mimi , mfano wewe ni mjahidina nikuhamasishe ule kama nyama ka nguruwe maana kanguruwe kenyewe kalikuwa kadogoooo tuuuu ,hivyo unajisi wake ni tofaute na lile libabayao la nguruwe.teh teh teh
 
Uamuzi ni wako mwenyewe lakini mjahidini yeyote kama mimi hata kula nguruwe hata aje nani?? ndugu...lakini sijaona uhusiano wake na siasa....ungejua hasara ya kula nguruwe usingejisifia ujinga...pole sana kula kilo kumi kwa siku kama wewe bingwa! ...then utaandika huo upuuzi wako hapa!!!
 
Tumaini,
Lakini nasikia kama hakuna alternative ya chakula kingine mjahidina anaruhusiwa kula nguruwe, kama niko-wrong nisahihishe.
 
Uamuzi ni wako mwenyewe lakini mjahidini yeyote kama mimi hata kula nguruwe hata aje nani?? ndugu...lakini sijaona uhusiano wake na siasa....ungejua hasara ya kula nguruwe usingejisifia ujinga...pole sana kula kilo kumi kwa siku kama wewe bingwa! ...then utaandika huo upuuzi wako hapa!!!

InakuwajeTumaini anatumia lugha za dharau kwa mwana JF mwenzake?Please moderator nipe mwongozo kwa kauli kama hizi zikiingizwa hapa JF, huwa unachukuliwa uamuzi gani?Anatakiwa ama afute kauli yake au akae chini?

Kumbukeni JF haina dini,anayekula paka ni juu yake na kizazi chake,anayekula bundi ni uamuzi wake,na anayesali hata kwenye mapango ni haki yake.Hamna mpumbavu kwenye jamii iliyostaharabika kama hii,na KAULI hii imenishtua!

Nawasilisha hoja na JF mnilinde!
 
Mkuu
haina haja yoyote yakumushutumu kwa lugha mbaya ,sisi tumefundishwa kuwapenda adui kama tunavyojipenda,hivyo kusema achukuliwe hatua kwa kauli mbaya ni kutomtendea haki mhusika maana wenda mafunzo yake tangu utoto ni kama ya kwetu ama yapo kinyume chake kitu kinachompa haki na uhalali wa kutamka maneno ya mfano huo.
 
Hongera B'MULO Hongera CHADEMA. Mtoa habari alidokeza hapo kabla kuwa watu wa maeneo hayo hawatabiriki, watachukua chochote utakachowapa lakini kura watampa wanayedhani anafaa, wamethibitisha hilo. Huu mwendo ungeenda hivyohivyo Tanzania nzima tungefika mbali. Kweli nimeamini hawa jamaa si waoga kama wa....
 
Nasikia TZ na Kenya kwa kubadirisha matokeo ya uchaguzi wamequarify kwa degree ya juu sana.

Kitu ambacho kilimpelekea Rais wa IRAN kabla ya uchaguzi wake kuja TZ na Kenya kuuchukuwa huo uzoefu na kwenda kui implementi nchi kwake. teh teh teh teh

Mh hebu tutajia hiyo source yako. Au ndiyo stori za maskani?
 
Niko Biharamulo na ninayo nakala ya Official Results za Chadema, data ni kama Invisible alivyoweka. Labda niongezee kidogo. Matokeo hayo ni ya jimbo zima isipokuwa kituo kimoja cha Nyabugombe "A" katika kata ya Nyakahura ambacho kina idadi ya wapiga kura 394. Hivyo Chadema wanasema hata CCM wakishindwa kwa 100% hicho kituo bado hawatafikia kura zao kwani tofauti ya kura ni 631.

Hivi sasa ni saa tisa usiku wafuasi wa Chadema bado wako nje ya ofisi ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wakiimba na kusheherekea, wakisubiri matokeo. CCM nao walikuja wakaanza na kuimba na kushangilia lakini wakazidiwa nguvu na wakaondoka. Walioko ndani ya nyumba ni Basil Lema wa Chadema na Watumishi wa Tume. Timu za CCM na TLP hazijaonekana. Habari kutoka ndani ya ofisi ni kwamba gari lililokuwa limebeba masanduku ya kura kutoka kata ya Kalenge (mpakani na Kibondo) limeharibika na limekwama Nyakanazi hivyo hamna majumlisho yoyote yatakayoendelea usiku huu. Lakini kuna habari kutoka Nyakanazi zinazosema dereva wa gari hilo anasema amepewa order apaki gari hapo Nyakanazi mpaka atakapopewe maelezo zaidi.

Uongozi wote wa CCM uliondoka Biharamulo jana na kuelekea Chato. Waliobaki ni watendaji waliokuwa na majukumu siku ya uchaguzi. Habari kutoka Chato ni kwamba kambi ya CCM imepata matokeo ya kata sita na bado hawana uhakika wa matokeo ya kata mbili: Kalenge na Nyabusozi. Licha ya hayo wanadai wameshinda kwa kura 1,971.

Sijui kama hapo kwa mkurugenzi patatosha kesho. Tusubiri tuone.
 
Udini kijana unakutafuna, hapa hujatoa maoni ya maana kazi yako unatafuta tu pale uislamu ulipoguswa, lol! After all mimi nilikuwa na-quote statement ya mtu mwingine, sasa shehe mbona waniandama mie ati!
Sasa mzee paroko... ulitaka tukunyamazie ili iweje?, udini unauona tu pale Muislam anapo kujibu... lol!
 
Back
Top Bottom