Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Pasco, hapa nimeongea na Zitto akanambia hivi:

Imetubidi kujumlisha upya matokeo, tumerudia mara ya pili tukapata hivi:

CHADEMA: 17,313

CCM: 16,682

TLP: 187

Lakini CCM wanatwambia wametushinda kwa tofauti ya kura 1,700 kitu ambacho hatukubaliani nacho, tunarudia kuhesabu mara ya 3!

Kaaazi kwelikweli

Huu ndio unyangumi! Wezi wakubwa hawa, wasipewe nafasi kabisa!
 
Hata wakipewe hizo kura za TLP kama ilivyofanya ZNP na ZPPP zamani za Zanzibar bado hawafikii kura za CHADEMA, sasa wameshindaje kwa zaidi ya kura 1700?
 
Ee mungu ibariki demokrasia ikue Tanzania. Hongera CHADEMA
 
Hata wakipewe hizo kura za TLP kama ilivyofanya ZNP na ZPPP zamani za Zanzibar bado hawafikii kura za CHADEMA, sasa wameshindaje kwa zaidi ya kura 1700?
Ndio hivyo sasa tumeshinda kwa kura 1700 zilizopigwa na wananchi wa biharamulo, siku nyingine mkome kushangilia ushindi uliotangazwa na Tanzania Daima gazeti la mbowe au kutegemea taarifa za zitto kabwe katibu wa chadema msubiri kauli za tume EBOH!!!
 
Hahha nna mdogo wangu yupo tume ya uchaguzi na yeye yupo Biharamulo nimempigia sasa hivi hataki kusema imekuwaje maana yeye ni CCM damu hahahaha anasema matokeo bado hayajatangazwa eti hajui hahaha CCM kushne maana CHADEMA sasa mwendo mdundooo

Na kigugumizi cha kutangaza cha nini? Yaani hapa hawa mafisadi wasitake chezea akili za watanzania ebo! Kwahiyo Kivuiti yuko anajiandaa kutangaza upside down?

Na wakimtangaza wakati hamja mchagua wana B'mlo mfukuzeni asije huko kwenu waondoke naye, make ni wao si wenu!
 
Hongereni sana Chadema kwa siasa nzuri za kisasa. La muhimu ni kukaza uzi mwakani tufanye mambo makubwa ya mabadiliko
 
Augustino Ramadhani ni jaji mkuu; nadhani unamaanisha Lewis makame-huyo ndio NEC Chairman
 
Ndio hivyo sasa tumeshinda kwa kura 1700 zilizopigwa na wananchi wa biharamulo, siku nyingine mkome kushangilia ushindi uliotangazwa na Tanzania Daima gazeti la mbowe au kutegemea taarifa za zitto kabwe katibu wa chadema msubiri kauli za tume EBOH!!!

Burn, na wewe kumbe ni wale wale. Basi kazi ipo, kumbe kuna watu wengi sana wanaosababisha kuzorota kwa maendeleo Tanzania. Yani unashabikia wizi wa kura hii kweli kiboko.

TANZANIA BILA YA CCM INAWEZEKANA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Pasco, hapa nimeongea na Zitto akanambia hivi:

Imetubidi kujumlisha upya matokeo, tumerudia mara ya pili tukapata hivi:

CHADEMA: 17,313

CCM: 16,682

TLP: 187

Lakini CCM wanatwambia wametushinda kwa tofauti ya kura 1,700 kitu ambacho hatukubaliani nacho, tunarudia kuhesabu mara ya 3!

Kaaazi kwelikweli

Mkuu yale masanduku yaliokwama njiani vipi? yameshafika? samahani kwa kuwa nakubandikia kazi ambayo upo mbali nayo
 
In lousy democracies like ours, Its easy to win votes over incumbent, but to win election over incumbent u need to win decisively/massively....

omarilyas
 
Mkuu yale masanduku yaliokwama njiani vipi? yameshafika? samahani kwa kuwa nakubandikia kazi ambayo upo mbali nayo
Ndo yaliyozua zogo mkuu... Ngoja kuna mtu naongea naye ni wa CCM nitarejea soon, ni vema kupata kujua pande mbili zinasemaje... Upande wa tatu naona kama washakubali matokeo (TLP & CUF)
 
KWa usemi huo yaonyesha kabsa CCM walishaiba kura wakapanga matokeo yawe hivyo ushindi kwa kura 1700 sasa wamechemsha, hawa wote wanastahili adhabu ya viboko 12 wakiingia na wakitoka 12 wakawaonyeshe wake zao gadem zao
 
Mkuu yale masanduku yaliokwama njiani vipi? yameshafika? samahani kwa kuwa nakubandikia kazi ambayo upo mbali nayo

Hii sasa kali, kuna masanduku yaliyokwama njiani!!! Kama zoezi la kuhesabu kura limeshakamilika hayo masanduku yanatoka wapi??? Selous mbona kama vile unataka kupotosha umma???
 
Ndo yaliyozua zogo mkuu... Ngoja kuna mtu naongea naye ni wa CCM nitarejea soon, ni vema kupata kujua pande mbili zinasemaje... Upande wa tatu naona kama washakubali matokeo (TLP & CUF)

Hapa kuna namna hii sio bure na safari hii hatutakubali yaliyotokea Busanda yajirudie. Hapa tunasubiri matokeo yasomwe na sio kuhesabu kura. Hilo swala la masanduku kukwama mahahi linatoka wapi???

Safari hii hatuta kubali UFISADI wa aina yoyote ile. Mpaka sasa hivi zimebaki dakika kama 17 tu ili matokeo yatangazwe.
 
Hii sasa kali, kuna masanduku yaliyokwama njiani!!! Kama zoezi la kuhesabu kura limeshakamilika hayo masanduku yanatoka wapi??? Selous mbona kama vile unataka kupotosha umma???
Hapana Mkuu, sina nia mabaya ila kuna masanduku yalikwama somewhere tuliambiwa hapa hapa. Hi ndo chanzo cha habari na pia rejea pages za nyuma for reference
 
True, lakini 2010, Dr. mbassa si atatetea kiti chake? Kumbuka sasa hivi ataingia kwa nguvu na atakuwa anaanza kuonyesha ufanisi. kwahiyo mwakani kwake nadhani itakuwa rahisi zaidi!
Mambo yanaweza kumuwia magumu kwa sababu hatokuwa na usaidiziw a nguvu kwenyen kampeni kama alioupata sasa hivi. Kumbuka wakati huo akina Slaa watakuwa nao wanaopambana kulinda majimbo yao
 
Hapana Mkuu, sina nia mabaya ila kuna masanduku yalikwama somewhere tuliambiwa hapa hapa. Hi ndo chanzo cha habari na pia rejea pages za nyuma for reference

Poa mkuu, hapo nimekupata.
 
Back
Top Bottom