Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Tume ya Uchaguzi imetangaza ndoto ya Kikwete aliyoota usiku. Kama unaamini ndoto za Raisi ni reality basi CCM wameshinda Biharamulo na Tume haijabadilisha matokeo ya baadhi ya vituo.

Mkuu una maana gani? wameyapika juu kwa juu bila kurekebisha kwenye vituo?
 
Watu walikatwa mapanga, kumwagikiwa tindikali, Wizi kila aina ya ufisadi kila sehemu. nashindwa kuelewa kuwa hata mwaka 2005 CCM waliiba kura sio sahihi kama hivi. Tumechoka na wizi wenu na hiyo tume yenu ya Uchaguzi ambayo nayo yenu
 
Hawa viongozi na idara za serikali hawajui kusoma na kuelewa mikataba!

Hata hesabu za darasa la nne nazo hawajui?

Shame, we need to take them down sooner than later!
 
Kwakuwa Tume imeshatangaza matokeo ya uchaguzi na CCM imeshinda kwa sheria zilizopo hakuna kitakachobadilika...mimi nafikiri tujadili what next for wapinzani; kati ya sasa (2009-2010) kwakuwa muda ni mfupi tuwe na dai moja linalowezekana. Na kwa maoni yangu ni kuwa Viongozi wa upinzani kwa pamoja wafanye kitu kilichofanywa na wananchi wengi east europ..green revolution.
a) Nafikiri ni wakati muafaka viongozi wa Chadema na CUF wanaofahamu na kuumizwa na zengwe la CCM wawaandae wananchi for country wide demonstration say one week tudai yafuatayo:-
i. Tume huru ya uchaguzi before 2010
Nafikiri bila kudai tume huru before tutakuja hapa JF tunajadili maumivu ya kuibia kura na pengine wakati muafaka kuonyesha uongozi mbadala kwa manufaa na ustawi wa nchi yetu.
Fiada ya demonstration ni walau world can see our disatifaction with the way CCM handles democracy...in Tanzania. Na kwakuwa budget yetu inategemea donors na one condition ni good governance naamini "Hapa tutapata" tume huru.
Tukiwa na tume huru xao la viongozi kwenye uchaguzi mkuu 2010 itakuwa halali kuongoza nchi kuleta "Katiba mpya"
Ni MAONI YANGU JF mnasemaje?
 
kwi kwi kwi kwi..........yaani mlifikir mnaweza kutushinda kirahisi rahisi hivyo.....huku Mzee Tinga tinga mwenyewe akiwa ndani ya nyumba.............na mngeshinda tungekata rufaa...........i said it.......na sasa mjionee....mkakati ni kurudisha majimbo yote kwa CCM

Kwi kwi kwi!!!....yaani nimewaonea huruma kweli CHADEMA asubuhi ya leo. Ni kama ile ya Bush kumshinda Kerry, yaani siku ile sitaki kuisahau. Nililala nikiamini jamaa ameshinda, kuamka asubuhi nikafikiri naota ndoto.

Walikuwa na nafasi ya ku capitalize haya makosa ya CCM na ufisadi lakini inaelekea wanashindwa kuandaa mkakati wa ushindi. Kuanzia sasa hakuna uchaguzi mdogo tena mpaka ngoma kuu 2010.

Mzee Tainga Tainga kaweka record ya kushinda majimbo yote kwenye chaguzi ndogo. Hata Tarime wangempeleka yeye huenda jimbo lingelikuwa la CCM.

Watani wa CHADEMA poleni sana, mwondoeni huyo msanii wenu Mbowe labda chama kitabadilika. Mbowe karibu kila kitu hana tofauti na akina JK au Lowassa, in fact ni rafiki yao kwenye ulaji.
 
Tume ya uchaguzi hatuna ni Kivuitu no.2.Vyama vya upinzani mdai tume huru ya uchaguzi kabla ya 2010.
 
Aleluya!

Hili kwa kweli halikubaliki kamwe kama hadi asubuhi ilikuwa imeonekana kuwa CHADEMA WAMESHINDA, wanachadema wanakila sababu za kuuliza kulikoni, tunacho waomba CCM na wajue ni kuwa sisi hatuhitaji umwagaji damu kama ilivyo kuwa kule Kenya nk. Imefika wakati sasa wakubali matokeo ili amani itawale na wasifikiri kweli nguvu za jeshi peke yake zinaweza kuleta amani. Wananchi wanajua ni nini wanahitaji na wapewe kile wanachohitaji.
Mungu wetu na atusaidie amani itawale! Amina!
 
Last edited:
Hiki ndicho mlichosahau sasa, kumwaga utitiri wa ma thread na ku cry baby!
 
Kwi kwi kwi!!!....yaani nimewaonea huruma kweli CHADEMA asubuhi ya leo. Ni kama ile ya Bush kumshinda Kerry, yaani siku ile sitaki kuisahau. Nililala nikiamini jamaa ameshinda, kuamka asubuhi nikafikiri naota ndoto.

Walikuwa na nafasi ya ku capitalize haya makosa ya CCM na ufisadi lakini inaelekea wanashindwa kuandaa mkakati wa ushindi. Kuanzia sasa hakuna uchaguzi mdogo tena mpaka ngoma kuu 2010.

Mzee Tainga Tainga kaweka record ya kushinda majimbo yote kwenye chaguzi ndogo. Hata Tarime wangempeleka yeye huenda jimbo lingelikuwa la CCM.

Watani wa CHADEMA poleni sana, mwondoeni huyo msanii wenu Mbowe labda chama kitabadilika. Mbowe karibu kila kitu hana tofauti na akina JK au Lowassa, in fact ni rafiki yao kwenye ulaji.

Wewe sasa unatafuta ugomvi na una put your credibility on line of fire.... subiri uone.

Simo!
 
viongozi wa chadema mliopo JF tupeni semeni kitu basi
 
ni huyo huyo; makamba atakuwa kapigiwa asubuhi ile akasave hicho kiti wasikiachie; shame on him

Mkuu najiuliza kama mimi ningekuwa CCM ningefanya nini. Nisingekubali kushindwa, lazima nigefanya kila ninaloweza nisiabike hasa katika kipindi kama hiki ninapokuwa na kashfa. Na ukiangalia hesabu wa tofauti ya kura inaruhusu kucheza rafu hiyo. Kama Jeshi ni lako, polisi ni wako, usalama ni wako na above all tumeya uchaguzi ni yako, kwanini usifanye ujanja? Tujaribu kujiweka kwenye nafasi ya CCM ili tuweze kuona kwa nini wanafanya wanachofanya, kama kweli wamefanya hivyo.
 
Dawa ni kuachana na TBC radio ya mafisadi. Tuanzishe ya kwetu CHABOCO ( Chadema Broadcating co-operations) kama tulivyo na TanzaniaDaima vile. Au tumwambie mzee na mfadhili wetu Mengi tubadilishe ITV na Radio iwe CHABOCO!

Mwendo mdundo!
 
pole sana Mkuu
labda wamepata kutoka Tume maana hapa taarifa tunazopata ni kuwa tume imetangaza ila chadema wamekataa na hivyo bado kuna malumbano
Sijajua kuwa maana kuna habari kuwa CCM imeshinda sasa inakuaje?? Mbona unaleta uongo tena na majungu hapa
 
CHADEMA mng'ang'ane hapohapo hadi tume ya Kivuitu no.2 ing'olewe kwani inawachezea akili Watanzania.
 
Bora mjiunge na CCM kuliko kuendelea kupoteza nguvu zenu...
 
Hivyo ni Kubaka Demokrasi ya Tanzania. Hakuna maana ya kufanya uchaguzi mdogo wala mjomba wake uchaguzi
 
Kwi kwi kwi!!!....yaani nimewaonea huruma kweli CHADEMA asubuhi ya leo. Ni kama ile ya Bush kumshinda Kerry, yaani siku ile sitaki kuisahau. Nililala nikiamini jamaa ameshinda, kuamka asubuhi nikafikiri naota ndoto.

Walikuwa na nafasi ya ku capitalize haya makosa ya CCM na ufisadi lakini inaelekea wanashindwa kuandaa mkakati wa ushindi. Kuanzia sasa hakuna uchaguzi mdogo tena mpaka ngoma kuu 2010.

Mzee Tainga Tainga kaweka record ya kushinda majimbo yote kwenye chaguzi ndogo. Hata Tarime wangempeleka yeye huenda jimbo lingelikuwa la CCM.

Watani wa CHADEMA poleni sana, mwondoeni huyo msanii wenu Mbowe labda chama kitabadilika. Mbowe karibu kila kitu hana tofauti na akina JK au Lowassa, in fact ni rafiki yao kwenye ulaji.

Pamoja na matokeo hayo ila nafikiri mzee invisible alitu bias kidogo kuhusu ushindi wa CHADEMA.Yeye alilipoti zilizobaki kura kuhesabiwa ni 340 hivi na zilizohesabiwa zimetoka wapi? na ukiangalia ktk makabrasha ya invisible namba za chadema zinaonekana nyingi na Tume imesoma namba kiduchu.

Sitaki kuamini mambo haya kama kuna wizi ama lah! maana simwamini huyo wa tume na pia simwamini invisible kwa data zake.
 
Back
Top Bottom