Kwi kwi kwi!!!....yaani nimewaonea huruma kweli CHADEMA asubuhi ya leo. Ni kama ile ya Bush kumshinda Kerry, yaani siku ile sitaki kuisahau. Nililala nikiamini jamaa ameshinda, kuamka asubuhi nikafikiri naota ndoto.
Walikuwa na nafasi ya ku capitalize haya makosa ya CCM na ufisadi lakini inaelekea wanashindwa kuandaa mkakati wa ushindi. Kuanzia sasa hakuna uchaguzi mdogo tena mpaka ngoma kuu 2010.
Mzee Tainga Tainga kaweka record ya kushinda majimbo yote kwenye chaguzi ndogo. Hata Tarime wangempeleka yeye huenda jimbo lingelikuwa la CCM.
Watani wa CHADEMA poleni sana, mwondoeni huyo msanii wenu Mbowe labda chama kitabadilika. Mbowe karibu kila kitu hana tofauti na akina JK au Lowassa, in fact ni rafiki yao kwenye ulaji.