Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Awali:
Ingawa matokeo rasmi hayajatangazwa, CHADEMA inaelekea wameweza kuwashinda kwa karibu kabisa CCM kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Biharamulo hii leo.
Mpaka zinapatikana hesabu za mwishomwisho kukiwa bado kituo kimoja cha Nyabugombe B chenye wapiga kura 394 CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa 50.6% huku CCM ikiifuatia kwa karibu ikiwa na asilimia 48.8% ya kura zote na TLP ikiwa imejinyakulia 0.55% ya kura zote.
Matokeo yanatarajiwa kutangazwa rasmi punde
Lakini matokeo ambayo yamejumlishwa mpaka dakika hii ni haya:
CHADEMA: 17,313
CCM: 16,682
TLP: 187
Turnout ilikuwa 39.24% (incredible!)
========================================
UPDATE 1...
Matokeo ya kituo kwa kituo tuliyoyapata toka kwa mwakilishi wa JF jimboni humo yameambatanishwa hapa chini kama attachment:
![]()
========================================
UPDATE 2.
Tume ya uchaguzi imesema hivi:
CCM: 17,561 = 51%
CHADEMA: 16,670 = 48.4%
CHADEMA wameyakataa matokeo kwani wanadai matokeo ya kata 3 yamegeuzwa tofauti na walivyosaini wasimamizi wa matokeo na yalivyohesabika vituoni!
========================================
Update 3.
Tume ya Uchaguzi imemtangaza mgombea wa CCM kama mshindi kwa kura zinazoonyeshwa kwenye Update ya awali ingawa CHADEMA wameyakataa matokeo ya vituo 9 kati ya vituo 237 vya uchaguzi!
========================================
Hakuna nukta iliyoachwa?