Sitaki tena kusikia habari za makonda wala dawa nimechoka, tumepoteza mda mwingi sana tumeshindwa kujadili mambo ya msingi kama elimu ya tanzania, vichwa vyote vimegeukia kwenye hoja za kijinga kabisa.
Mh. Ndalichako vipi tathimini yako hukusu kufeli kwa shule za serikali au ndiyo na wewe umejificha kwenye kichaka cha makonda, mimi bado niko na wewe sikuachi.
Mwisho kabisa uliingia kwa mbwembwe mara hakuna kuvaa majoho, mara sayansi ni ladhima n.k. tunaomba majibu kwasababu tuko mwaka 2017 bado miezi michache tu form wafanye paper tena.