Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Ufanyike uchunguzi kwanini watoto wa Mtwara wana poor performance. Jibu likipatikana ifanyiwe mkakati wa kuinua elimu Mtwara. Kama ni kuanzisha madarasa ya Jumamosi nje ya syllabus. Serikali itenge fungu maalum la kuinua elimu Mtwara.
Hali ikiachwa hivi, hii jamii itakua imetengwa sana kimaendeleo. Ninakumbuka Nyerere alifanya mkakati wa kuwapeleka shule wa Irak mkoa wa Arusha enzi hizo. Vijana waliomaliza darasa la saba walipelekwa shule za sekondari za serikali. Wengine walikataa kwenda kwani walikua wameshaoa lakini walihakikishiwa mshahara wa kima cha chini kila mwezi kama allowance. Nyerere hakutaka ile jamii ije itengwe huko mbele.
Jamii ya walioelimika ni rahisi hata kupeleka maendeleo na wakayaendeleza. Watu wasio na elimu ni shida hata kufuata ushauri wa daktari wakiwa wagonjwa. Matokeo yake ugonjwa unachukua muda mrefu kupona na gharama kuongezeka.
Jamii inapokosa elimu ni rahisi kujikinga na matendo ya kihalifu, kwa kushawishiwa au kwa kuongeza kipato. Kwa kifupi kuwa na jamii iliyokosa elimu ni sawa na bomu linaweza kukipuka muda woeste.