Matokeo ya 1-1 Liverpool na Man City yaipa faida Arsenal kwenye EPL

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Manchester City umemalizika kwa sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Anfield, matokeo ambayo yanaipa faifa Arsenal kubaki kileleni katika Premier League kwa faida ya magoli mengi ya kufunga

Magoli yaliyoamua mechi ya leo Machi 10, 2024 yamefungwa na John Stones kwa City na Alexis Mac Allister kwa Liverpool.

Baada ya matokeo hayo, Arsenal inaongoza ikiwa na pointi 64 sawa na Liverpool wakati Man City ipo nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 63, timu zote zikisaliwa na michezo 10 kukamilisha msimu wa 2023/24 katika EPL.
 
Klabu ya Liverpool imetoka sare ya 1-1 dhidi ya Man City katika mchezo mgumu na wenye kutoa uelekeo wa ubingwa wa EPL.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Anfield, Man City ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kipindi cha kwanza kupitia John Stones kabla ya Liverpool kusawazisha kipindi cha pili kupitia Mac Allister kwa mkwaju wa penati.

Kwa matokeo hayo, Liverpool yupo nafasi ya pili akiwa na alama 64 huku Man City akiwa na alama 63 katika nafasi ya tatu.
 
Habari zako nyingi unazopost ndio huwekwa kwenye chanel ya JF kule Whatsapp. Unaupiga mwingi na jamaa zako wanajua kukubeba
 
Hizi ndo mambo napenda kuona city na liver wakiuana wenyewe kwa wenyewe
 
Kweli mpira tumezidiwa leo,ila bado sioni kama City tutapoteza ubingwa,na huu ndio uzuri wa Epl mambo hayatabiriki
hayatabiriki wapi mzee acha kuficha ficha city akika juu pale Ni ngumu sana kumsusha tuacha tu unafiki jamaa anaenda tena kubeba ubigwa
 
Yule luis diaz mechi ya leo inaweza kuwa alitumia madawa ya kuongeza nguvu maana sio kwa kasi ile
 
Hapa umepuyanga mkuu
Nimepuyanga Nin mzee humfungi united pale old trafford umesahau last season kakufanyeje na unakumbuka mara ya mwisho lini
umemfunga united old trafford kwenye ligi njoo kwa City karibu mechi zote pale ETIHAD uwa unabondwa bado uyo Spurs anaitaka Top Four wew ndio unasafari Ngumu kuliko wezako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…