KERO Matokeo ya CBE Dodoma Mwaka 2018/19 na 2019/20 hayajawekwa katika Mfumo wa NACTVET

KERO Matokeo ya CBE Dodoma Mwaka 2018/19 na 2019/20 hayajawekwa katika Mfumo wa NACTVET

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Matokeo ya CBE Dodoma Mwaka 2018/19 na 2019/20 hayajawekwa kwenye Mfumo wa NACTVET, mtu aliyemaliza miaka hiyo akirudi chuoni kuendelea na masomo, anaambiwa matokeo yake bado hayapo NACTVET.

Miaka yote hiyo walikuwa wanafanya nini? Sasa mtu hawezi kuendelea na Degree mpaka matokeo yawepo NACTVET. Uongozi wa chuo hautupi ushirikiano, wakati udahili unaendelea mpaka sasa na deadline inakaribia.

Nikitumia namba yangu kwenye mfumo wa NACTVET kuangalia kama matokeo yapo au hayapo, nakuta hayapo. Pia nimeongea na Examination Officer, ambaye amesema tusubiri mpaka dirisha lifunguliwe ndipo waingize matokeo, lakini nina wasiwasi hawatafanya hivyo.

Naomba wahusika walisaidie suala hili ili tusikose nafasi za kuendelea na masomo.

Pia soma ~ CBE: Suala la matokeo ya Wanafunzi wa 2018/19 na 2019/20 kutowekwa katika mfumo wa NACTVET, linashughulikiwa
 
Back
Top Bottom