KERO Matokeo ya Diploma UDOM yamechelewa Wanafunzi tupo kwenye hatari ya kushindwa kuomba kujiunga na masomo ya Shahada

KERO Matokeo ya Diploma UDOM yamechelewa Wanafunzi tupo kwenye hatari ya kushindwa kuomba kujiunga na masomo ya Shahada

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

kayanza555

New Member
Joined
Jul 18, 2023
Posts
1
Reaction score
1
Wahitimu wa ngazi ya Diploma kwa mwaka wa masomo 2025/2026 tunakabiliwa na changamoto ya kushindwa kuomba nafasi za masomo ya Shahada kwa mwaka huu kutokana na matokeo yetu kutokuwa yamewekwa kwenye mfumo hadi sasa.

Hadi wakati huu, bado hatujapewa taarifa rasmi kuhusu sababu ya kuchelewa kwa matokeo hayo wala lini yanatarajiwa kuwekwa kwenye mfumo. Hali hii inatupa wasiwasi mkubwa, kwa kuwa muda wa kuomba nafasi za masomo ya Shahada unaendelea, huku sisi tukihitaji matokeo hayo pamoja na AVN ili kukamilisha maombi yetu.

Tunaomba UDOM itoe ufafanuzi kuhusu changamoto hii na kutueleza ni lini matokeo yetu yatawekwa kwenye mfumo ili nasi tupate fursa ya kuomba Shahada kwa wakati.

UDOM, tatizo ni nini? Tunaomba mtupatie majibu na suluhisho mapema, kwani kuchelewa huku kunaweza kutufanya tukose fursa ya kuendelea na masomo kutokana na sababu ambazo haziko ndani ya uwezo wetu.
 
Utaomba shahada mwakani.

Au ungeenda form six direct ukajiunga na shahada kama ulikuwa na haraka sana
 
Back
Top Bottom