Matokeo ya Kidato cha 6 2024: Shule 710 kati ya 929 zimepata Wastani wa Daraja C la Ufaulu, Shule 100 zimepata Daraja A na B

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Kwa mujibu wa Matokeo ya Mtihani wa Kihitimu Kidato cha 6 uliofanywa Mei 2024 na kutangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Ufaulu wa Watahiniwa waliopata Daraja I - III umeongezeka kwa 0.10% kutoka Wanafunzi 95,442 (99.30%) mwaka 2023 hadi 102,719 (99.40%) mwaka 2024.

NECTA imesema licha kuongezeka kwa Ufaulu wa Tahasusi zote za Sayansi Asilia kwa 1.01% hadi 12.82% kwa Watahiniwa waliopata Divisheni I na II, Ufaulu wa Tahasusi za Masomo ya Fizikia, Advanced Mathematics na Sayansi ya Kompyuta (PMCs) umeshuka kwa 4.04% kulinganisha na mwaka 2023.

Pia, Tahasusi nyingine zilizoshuka Ufaulu ni pamoja na Kiswahili, English Language, Arabic Language
(KLA) 5.06%, Economics, Commerce, Accountancy (ECA) 1.20%. Aidha, Shule 710 kati ya 929 zilizofanya Mtihani zimepata Wastani wa Daraja C la Ufaulu, Shule 100 zimepata Daraja A na B, Shule 111 zimepata D, na 8 Daraja E.

1720946112482.png

Ufaulu wa Watahiniwa wa Shule Kimasomo Takwimu za matokeo zinaonesha kuwa, masomo yote yana watahiniwa waliofaulu kati ya asilimia 96.84 hadi 100 isipokuwa somo la Basic Applied Mathematics ambalo watahiniwa 12 wamefaulu kwa asilimia 77.55.

Aidha, ufaulu wa somo la Basic Applied Mathematics umeendelea kuimarika ambapo umeongezeka kwa asilimia 9.02 ikilinganishwa na mwaka 2023. Watahiniwa zaidi ya asilimia 66 katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, Advanced Mathematics, Economics, Commerce na Accountancy wamepata ufaulu wa gredi za juu ambazo ni gredi A hadi C sawa na alama 60 hadi 100.

Watahiniwa zaidi ya asilimia 50 katika masomo ya General Studies, English Language, Physics, Chemistry, Biology, Agriculture na Education wamepata ufaulu wa gredi za wastani ambazo ni D na E sawa na alama 40 hadi 59. Aidha, watahiniwa waliofaulu katika somo la Basic Mathematics wengi wapo katika mtawanyiko wa gredi C, D, E na S sawa na alama 35 hadi 69.

Somo la Advanced Mathematics lina asilimia 12.89 ya watahiniwa waliopata gredi A likifuatiwa na somo la Accountancy lenye asilimia 3.90 na somo la Chemistry lenye asilimia 2.73. Masomo ya Lugha ambayo ni French Language, Chinese Language na Arabic Language yana ufaulu mzuri ambao ni kati ya asilimia 96.84 hadi 100 japokuwa idadi ya watahiniwa katika masomo haya ni ndogo ambayo ni kati ya watahiniwa 43 hadi 251.

Mtihani wa Kidato cha Sita
Ufaulu wa Jumla
(a) Watahiniwa Wote
Jumla ya watahiniwa 111,056 wa Shule na Kujitegemea sawa na asilimia 99.43 ya watahiniwa wenye matokeo ya
Mtihani wa Kidato cha Sita 2024 wamefaulu. Wanawake waliofaulu ni 49,837 sawa na asilimia 99.61 wakati
Wanaume waliofaulu ni 61,219 sawa na asilimia 99.28. Mwaka 2023 watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 104,549
sawa na asilimia 99.23. Hivyo, ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.20 ikilinganishwa na mwaka 2023.

(b) Watahiniwa wa Shule
Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni 103,252 sawa na asilimia 99.92 ya watahiniwa wenye matokeo. Wanawake waliofaulu ni 46,615 sawa na asilimia 99.93 na Wanaume ni 56,637 sawa na asilimia 99.91. Aidha, watahiniwa walioshindwa mtihani ni 84 sawa na asilimia 0.08.

Mwaka 2023 watahiniwa 96,010 sawa na asilimia 99.90 ya Watahiniwa wa Shule walifaulu mtihani huo. Hivyo, ufaulu wa Watahiniwa wa Shule umeongezeka kwa asilimia 0.02 ikilinganishwa na mwaka 2023.

(c) Watahiniwa wa Kujitegemea Idadi ya Watahiniwa wa Kujitegemea waliofaulu mtihani ni 7,804 sawa na asilimia 93.34. Mwaka 2023 Watahiniwa wa Kujitegemea 8,539 sawa na asilimia 92.30 walifaulu mtihani
huo. Hivyo, ufaulu wa Watahiniwa wa Kujitegemea umeongezeka kwa asilimia 1.04 ikilinganishwa na mwaka
2023.

3.1.2 Ubora wa Ufaulu
Ubora wa ufaulu kwa kuzingatia madaraja waliyopata Watahiniwa wa Shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 102,719 sawa na asilimia 99.40 wamepata ufaulu mzuri wa Madaraja ya I-III. Aidha,
watahiniwa wengi wapo katika ufaulu wa Daraja la I na II ambapo 4 Daraja la I ni watahiniwa 47,862 (46.32%) na Daraja la II ni 42,359 (40.99%).

Mwaka 2023 watahiniwa waliopata ufaulu wa Madaraja I-III walikuwa 95,442 sawa na asilimia 99.30. Hivyo, ubora wa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.10 ikilinganishwa na mwaka 2023.
 
Attachments

Kwa mujibu wa Matokeo ya Mtihani wa Kihitimu Kidato cha 6 uliofanywa Mei 2024 na kutangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Ufaulu wa Watahiniwa waliopata Daraja I - III umeongezeka kwa 0.10% kutoka Wanafunzi 95,442 (99.30%) mwaka 2023 hadi 102,719 (99.40%) mwaka 2024.

NECTA imesema licha kuongezeka kwa Ufaulu wa Tahasusi zote za Sayansi Asilia kwa 1.01% hadi 12.82% kwa Watahiniwa waliopata Divisheni I na II, Ufaulu wa Tahasusi za Masomo ya Fizikia, Advanced Mathematics na Sayansi ya Kompyuta (PMCs) umeshuka kwa 4.04% kulinganisha na mwaka 2023.

Pia, Tahasusi nyingine zilizoshuka Ufaulu ni pamoja na Kiswahili, English Language, Arabic Language
(KLA) 5.06%, Economics, Commerce, Accountancy (ECA) 1.20%. Aidha, Shule 710 kati ya 910 zilizofanya Mtihani zimepata Wastani wa Daraja C la Ufaulu, Shule 100 zimepata Daraja A na B, Shule 111 zimepata D, na 8 Daraja E.

View attachment 3042026
Ufaulu wa Watahiniwa wa Shule Kimasomo Takwimu za matokeo zinaonesha kuwa, masomo yote yana watahiniwa waliofaulu kati ya asilimia 96.84 hadi 100 isipokuwa somo la Basic Applied Mathematics ambalo watahiniwa 12 wamefaulu kwa asilimia 77.55.

Aidha, ufaulu wa somo la Basic Applied Mathematics umeendelea kuimarika ambapo umeongezeka kwa asilimia 9.02 ikilinganishwa na mwaka 2023. Watahiniwa zaidi ya asilimia 66 katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, Advanced Mathematics, Economics, Commerce na Accountancy wamepata ufaulu wa gredi za juu ambazo ni gredi A hadi C sawa na alama 60 hadi 100.

Watahiniwa zaidi ya asilimia 50 katika masomo ya General Studies, English Language, Physics, Chemistry, Biology, Agriculture na Education wamepata ufaulu wa gredi za wastani ambazo ni D na E sawa na alama 40 hadi 59. Aidha, watahiniwa waliofaulu katika somo la Basic Mathematics wengi wapo katika mtawanyiko wa gredi C, D, E na S sawa na alama 35 hadi 69.

Somo la Advanced Mathematics lina asilimia 12.89 ya watahiniwa waliopata gredi A likifuatiwa na somo la Accountancy lenye asilimia 3.90 na somo la Chemistry lenye asilimia 2.73. Masomo ya Lugha ambayo ni French Language, Chinese Language na Arabic Language yana ufaulu mzuri ambao ni kati ya asilimia 96.84 hadi 100 japokuwa idadi ya watahiniwa katika masomo haya ni ndogo ambayo ni kati ya watahiniwa 43 hadi 251.

Mtihani wa Kidato cha Sita
Ufaulu wa Jumla
(a) Watahiniwa Wote
Jumla ya watahiniwa 111,056 wa Shule na Kujitegemea sawa na asilimia 99.43 ya watahiniwa wenye matokeo ya
Mtihani wa Kidato cha Sita 2024 wamefaulu. Wanawake waliofaulu ni 49,837 sawa na asilimia 99.61 wakati
Wanaume waliofaulu ni 61,219 sawa na asilimia 99.28. Mwaka 2023 watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 104,549
sawa na asilimia 99.23. Hivyo, ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.20 ikilinganishwa na mwaka 2023.

(b) Watahiniwa wa Shule
Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni 103,252 sawa na asilimia 99.92 ya watahiniwa wenye matokeo. Wanawake waliofaulu ni 46,615 sawa na asilimia 99.93 na Wanaume ni 56,637 sawa na asilimia 99.91. Aidha, watahiniwa walioshindwa mtihani ni 84 sawa na asilimia 0.08.

Mwaka 2023 watahiniwa 96,010 sawa na asilimia 99.90 ya Watahiniwa wa Shule walifaulu mtihani huo. Hivyo, ufaulu wa Watahiniwa wa Shule umeongezeka kwa asilimia 0.02 ikilinganishwa na mwaka 2023.

(c) Watahiniwa wa Kujitegemea Idadi ya Watahiniwa wa Kujitegemea waliofaulu mtihani ni 7,804 sawa na asilimia 93.34. Mwaka 2023 Watahiniwa wa Kujitegemea 8,539 sawa na asilimia 92.30 walifaulu mtihani
huo. Hivyo, ufaulu wa Watahiniwa wa Kujitegemea umeongezeka kwa asilimia 1.04 ikilinganishwa na mwaka
2023.

3.1.2 Ubora wa Ufaulu
Ubora wa ufaulu kwa kuzingatia madaraja waliyopata Watahiniwa wa Shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 102,719 sawa na asilimia 99.40 wamepata ufaulu mzuri wa Madaraja ya I-III. Aidha,
watahiniwa wengi wapo katika ufaulu wa Daraja la I na II ambapo 4 Daraja la I ni watahiniwa 47,862 (46.32%) na Daraja la II ni 42,359 (40.99%).

Mwaka 2023 watahiniwa waliopata ufaulu wa Madaraja I-III walikuwa 95,442 sawa na asilimia 99.30. Hivyo, ubora wa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.10 ikilinganishwa na mwaka 2023.
Tatizo elimu imeingiliwa na siasa nyingi huo ufaulu sio halisia ya uwezo wa wanafunzi.......shule moja ya serikali haina walimu wa biology na physics takriban kwa miaka miwili, ila hamba mwanafunzi alie pata f ya phisics wa mwisho alipata s.
 
Saiv mwenye Div 2 ni sawa kama kafeli akapambane na Diploma
Kwani Division 2, hupati mkopo?. Maana mdogo wangu kapata 2 ya 11, ya HKL, niambie kuhusu Mkopo na Chuo kwa siku hizi, maana zamani unapata mkopo na chuo.
 
Kupata Mkopo itategemea Taarifa zake na course atakayosoma...ila kwa HKL akipata sana 50% apo ashukuru
 
Tatizo elimu imeingiliwa na siasa nyingi huo ufaulu sio halisia ya uwezo wa wanafunzi.......shule moja ya serikali haina walimu wa biology na physics takriban kwa miaka miwili, ila hamba mwanafunzi alie pata f ya phisics wa mwisho alipata s.
Ulisoma advance? Unasema physics na biology hakuna aliyepata F, Ila kuna waliopata S? Unaelewa maana ya "S"?
 
Tatizo elimu imeingiliwa na siasa nyingi huo ufaulu sio halisia ya uwezo wa wanafunzi.......shule moja ya serikali haina walimu wa biology na physics takriban kwa miaka miwili, ila hamba mwanafunzi alie pata f ya phisics wa mwisho alipata s.
Haya matokeo yamapikwa yakaiva wanavyotaka wao.
Wange yaachia kama yalivyo ingekuwa ni balaa.
Wanafunzi hawasomi ........walimu hawafundishi.
 
Back
Top Bottom