sababu za kufeli kidato cha nne hizi hapa:
1. Shule za kata
2. Hiki ndo kidato wakati kipo mwaka wa pili serikali ilifuta kufeli kidato cha pili, na kusema kila mwanafunzi atapita tu.
naomba kuicheka serikali nikiwa nimekasirika.
Hahahahahaha ! muda wenu umekwisha sasa upuuuuzi sasa basiiiiii ! tokeni
sababu za kufeli kidato cha nne hizi hapa:
1. Shule za kata
2. Hiki ndo kidato wakati kipo mwaka wa pili serikali ilifuta kufeli kidato cha pili, na kusema kila mwanafunzi atapita tu.
naomba kuicheka serikali nikiwa nimekasirika.
Hahahahahaha ! muda wenu umekwisha sasa upuuuuzi sasa basiiiiii ! tokeni
serikali imetelekeza sekta ya elimu,hivyo hata matokeo ya mwaka haikuwa kitu cha kushangaza kwa watu wanaofuatilia kinachoendelea kwenye sekta hiyo.
mimi nashauri serikali ifanye yafuatayo;
1.iboreshe maslahi walimu.
2.kuajiri walimu wenye sifa stahiki.
3.kuboresha shule zote za serikali kwa kiwango cha kutoa taaluma kama shule za private.
4.kuwepo na sheria ya kuwabana viongozi/watu wote watoto wao wasome shule za hapa nchini.
5.mtihani wa kidato cha pili kupewa kipaumbele kwa wanafunzi kwenda cha tatu.
6.kujenga nyumba za walimu na kuzingatia miundombinu ya barabara,umeme,maji,n.k.kama kigezo cha kuwafanya waishi nyumba hizo.
Suala la elimu kwa kweli ni janga la kitaifa. Toka enzi za Baba wa Taifa hayati JKN maadui walikuwa ni watatu umasikini, ujinga na maradhi na mwenendo wa wale ambao wako madarakani kipindi hiki ni kama wanajaribu 'kupromote' hivo vitu badala ya kupambana kuvitokomeza. Tuna wizara na taasisi kadhaa zinazoshughulikia elimu, kuanzia ile ya awali mpaka elimu ya juu sasa sijajua kama jukumu lao ni kutunga mitihani na kutoa matokeo au kuhakikisha kwamba elimu bora inapatikana Tanzania ili kujenga taifa linaloenda sambamba na mabadiliko ya dunia.
Kuna haja ya hatua madhubuti na za haraka kuchukuliwa ili kulinusuru Taifa na hili janga kuu. Leo hii tunaongelea 'Fast Track' kuelekea 'Regional Intergration' na hali yetu kielimu ndio dhoofu kiasi hiki... Hili ni balaa.
hao 11 ni wale wenye div 1-3 wenye uwezo wa kuendelea kwa hiyo watakaopata vyeti vya 4m 4 ni asilimia 50 :car:
mwaka 2008, Shule moja inayoitwa High view sec school inayomikiwa na mmoja ya mfanya biashar mkubwa visiwani Zanzibar iliongoza Zanzibar kwa kufanya vizuri yaani ilitoa div 1 zaidi ya 15, div 2 za kumwaga kati ya watoto wsiozidi 50. hii ni mara ya kwanza kwa shule hiyo kutoa idadi kubwa wanafunzi. nadhani hata Baraza la Mitihani la Taifa Necta ilishtuka, iljihoji na ilitaka kujua haya ni matokeo ya Kweli?
Mwaka uliofuta NECTA ilituma ujumbe mzito katika shule hiyo, kwa maneno ya vijana iliwabana vijana sana vijana shule hiyo kwa kuweka Ulinzi mkali kwa usimamizi, ufanyaji wa mitihani, baadhi ya wajumbe kutoka NECTA Makao makuu Walishiriki kikamilifu kusimamia exam shuleni hapo. nasema walishiriki kusimamia, kuchunguza na kuzuia kila aina ya Ujanja, walifikia hata kuwasachi kabla ya exam. matokeo yake wanafunzi waliofanya Exam matukio yao sio mazuri.(naamini hata NECTA kwa hili hawatakanusha).
lKN sijui kama NECTA hufanya mkakati kama huu ktk shule ambazo huwa zinaongoza hasa za seminary? sijui kama wanshtuka kama walivyoshtuka High view? sijui hutumia mkakati kama walivyotumia huko Zenj?
LKN cha kujiuliza jee hawa ndio wanaopta first class Vyuo vikuu? au ndio bogas
Hata huko zenji jina lakifanana na John basi unapasi vibaya sana.
Haika,
Huo ndio uzalendo. Keep it up.
Ni vizuri tukaangalia vijana wamefelije kwenye shule zote bila kujali inamilikiwa na nani kwasababu mwisho wa siku, hao waliofeli watakuwa bado ni watanzania wenzetu na tutahitaji walete maendeleo kwa nchi bila kujali wanaamini dini gani.
Great thinkers, naomba tuachane na ushabiki wa kidini, hauna tija as usual mbali na kuleta maumivu tu kwenye roho zetu.