MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

mimi huwanaamini kuwa huu ni mpango murua wa viongozi wasio na maadili ya kizalendo. Na wanaoongoza kwa kutumia Katiba isiyo na meno.
Tuweke katiba mpya itakayoondoa hawa watu madarakani MARAMOJA!!! time and time again, hata nikiwa mimi niondolewe.
 
Suala la elimu kwa kweli ni janga la kitaifa. Toka enzi za Baba wa Taifa hayati JKN maadui walikuwa ni watatu umasikini, ujinga na maradhi na mwenendo wa wale ambao wako madarakani kipindi hiki ni kama wanajaribu 'kupromote' hivo vitu badala ya kupambana kuvitokomeza. Tuna wizara na taasisi kadhaa zinazoshughulikia elimu, kuanzia ile ya awali mpaka elimu ya juu sasa sijajua kama jukumu lao ni kutunga mitihani na kutoa matokeo au kuhakikisha kwamba elimu bora inapatikana Tanzania ili kujenga taifa linaloenda sambamba na mabadiliko ya dunia.

Kuna haja ya hatua madhubuti na za haraka kuchukuliwa ili kulinusuru Taifa na hili janga kuu. Leo hii tunaongelea 'Fast Track' kuelekea 'Regional Intergration' na hali yetu kielimu ndio dhoofu kiasi hiki... Hili ni balaa.
 
sababu za kufeli kidato cha nne hizi hapa:
1. Shule za kata
2. Hiki ndo kidato wakati kipo mwaka wa pili serikali ilifuta kufeli kidato cha pili, na kusema kila mwanafunzi atapita tu.

naomba kuicheka serikali nikiwa nimekasirika.

Hahahahahaha ! muda wenu umekwisha sasa upuuuuzi sasa basiiiiii ! tokeni

Sababu zako nazikubali, ila tatizo kubwa zaidi kwenye hizo shule za kata hakuna walimu kabisa Hebu fikiria tukitoa yale masomo ya sayansi yanayohitaji maabara, mbona hata masomo yasiyohitaji maabara kama kiswahili, history na mengine yanayofanana na hayo wamefeli? Jibu ni kwamba walimu wakipangiwa hizo shule wanaenda kuriport haf wanaaga kwenda kufuata mizigo makwao hiyo ndo inakuwa gia ya kuondokea, yaani hawarudi ng'o. Tatizo shule nyingi za kata ziko kwenye mazingira Mabaya mno, hakuna maji, umeme, mawasiliano, usafiri na huduma nyingine muhimu za jamii. Kwa mwalimu ambaye ana sifa za ualimu anaona ni mradi aende hata shule za private ambazo zipo pazuri.
Kwa shule za mjini za serikali zimefelisha kwa sababu wengi wa walimu hawana moyo wa kufanya kazi kwa nguvu zao zote, kwani wanatakiwa kuwa na shughuli nyingine nje ya kazi ili kuongeza kipato, maana kwa kutegemea mshahara tu maisha hayaendi.
Wa kulaumiwa ni serikali, iboreshe mazingira ya shule za kata kwanza ili huduma muhimu zikiwemo nyumba za walimu pamoja na hosteli za wanafunzi zijengwe, na pia iboreshe maslahi ya walimu.
Hebu fikiria sitting allowance ya mbuge ya siku moja ni sawa na mshahara wa mwalimu wa mwezi je hiyo ni fair?


 
sababu za kufeli kidato cha nne hizi hapa:
1. Shule za kata
2. Hiki ndo kidato wakati kipo mwaka wa pili serikali ilifuta kufeli kidato cha pili, na kusema kila mwanafunzi atapita tu.

naomba kuicheka serikali nikiwa nimekasirika.

Hahahahahaha ! muda wenu umekwisha sasa upuuuuzi sasa basiiiiii ! tokeni

Naunganana na wewe wangetahiniwa kwanza pumba zingeishia kidato cha pili na shule ingebaki na vijana wenye mwelekeo na kupunguza gharama za kusomesha pumba
 
Labda na tuangalie na mitihani yenyewe vile vile. Je inakidhi haja? Na inapima uelewa wa wanafunzi?
 
serikali imetelekeza sekta ya elimu,hivyo hata matokeo ya mwaka haikuwa kitu cha kushangaza kwa watu wanaofuatilia kinachoendelea kwenye sekta hiyo.
mimi nashauri serikali ifanye yafuatayo;
1.iboreshe maslahi walimu.
2.kuajiri walimu wenye sifa stahiki.
3.kuboresha shule zote za serikali kwa kiwango cha kutoa taaluma kama shule za private.
4.kuwepo na sheria ya kuwabana viongozi/watu wote watoto wao wasome shule za hapa nchini.
5.mtihani wa kidato cha pili kupewa kipaumbele kwa wanafunzi kwenda cha tatu.
6.kujenga nyumba za walimu na kuzingatia miundombinu ya barabara,umeme,maji,n.k.kama kigezo cha kuwafanya waishi nyumba hizo.

Yes hii ni sehemu ya matatizo yanayochangia elimu ya yetu kushuka/kuporomoka, Changamoto iliyopo ni namgani kupambana na haya kwa watawala wetu hawa!!! Tunahitaji mabadiliko ya haraka kama tunataka kwenda mbele.
 
Suala la elimu kwa kweli ni janga la kitaifa. Toka enzi za Baba wa Taifa hayati JKN maadui walikuwa ni watatu umasikini, ujinga na maradhi na mwenendo wa wale ambao wako madarakani kipindi hiki ni kama wanajaribu 'kupromote' hivo vitu badala ya kupambana kuvitokomeza. Tuna wizara na taasisi kadhaa zinazoshughulikia elimu, kuanzia ile ya awali mpaka elimu ya juu sasa sijajua kama jukumu lao ni kutunga mitihani na kutoa matokeo au kuhakikisha kwamba elimu bora inapatikana Tanzania ili kujenga taifa linaloenda sambamba na mabadiliko ya dunia.

Kuna haja ya hatua madhubuti na za haraka kuchukuliwa ili kulinusuru Taifa na hili janga kuu. Leo hii tunaongelea 'Fast Track' kuelekea 'Regional Intergration' na hali yetu kielimu ndio dhoofu kiasi hiki... Hili ni balaa.

Yetu macho! Hiyo "FAST TRACK" sijui nayo inaweza kuwa kama VODA FASTER ya waalimu
 
kuweka bajeti ya kutosha kwa shule zote ili walimu hahiri waweze kuishi kila mahali, kwa maisha ya kawaida, waweze kwenda hospitali wapate maji, wapate mawasiliano, wapate huduma za mahitaji ya kila siku kama chakula. Hasa wenye familia.
Si haki kumpeleka mwalimu sehemu yenye utata wa kupatikana mahitaji ya msingi eti akajenge nchi.
KAma kuna sehemu hazina uwezo wa kupata hayo mahitaji, basi shule zifungwe, na badala yake sehemu ya karibu ijengwe shule ya kulala na wawapokee wanafunzi wengi zaidi, ila walimu wahudumiwe kikamilifu.
Mie nadhani walimu wakipata huduma stahili, elimu itapanda tu. Watoto wote wasio na mahitaji maalum wasome shule za karibu zaidi. baada ya hapo shule binafsi zitozwe kodi kubwa ili zilazimishe umma mkubwa zaidi wa watanzania upeleke watoto huko.
 
ndugu zangu,
mahala tunapoelekea,Tanzania kama taifa ni pabaya zaidi,
maana yake kila sekta ni madudu; afya, elimu, viwanda, kilimo n.k..... na hii i matokeo ya kuwa na serikali mbovu inayozingatia ushkaji katika kupeana nyadhifa mbali mbali.i.e kulipana fadhila... ISITOSHE, SISI WENYEWE WATANZANIA NDIO TUNACHANGIA KWA KIASI KIKUBWA KWA UPUUZI HUU UNAOENDELEA, MAANAKE WENGI WETU TUNARUBUNIWA KIRAHISI SANA KWA KUPEWA KOFIA NA KANGA ZAO NA MAY BE UBWABWA UNAOAMBATANA NA AHADI YINGI ZA ALINACHA (katika hali ya kawaida mtu hawezi kukuahidi kuwanunulia bajaji wajawazito wote nchini na still unashangilia, huo ni ukosefu wa akili na kutokujua kufikiri kwako wewe msikilizaji na yule anayekuahidi huo upuuzi)

WATANZANIA BADILIKENI FIKRA ZETU, CCM SIO ROHO YA NCHI KWAMBA TUKIITOA NCHI ITAKUFA... NCHI YETU NI HEAVEN HII ENDAPO TU IKIPATA UONGOZI BORA NA MAKINI;VIONGOZI WENYE UWEZO WA KUFIKIRI,SIO KAMA HAWA WANAOENDESHA NCHI KWA KAULI MBIU!
 
Wanafunzi watacha vipi kufeli wakati walimu wenyewe hawapewi mishahara? Ukiangalia shule za binafsi ndo nizimefanya vizuri kuliko za serikali. Walimu hao hao wa shule za serikali wanaenda kufundisha shule za binafsi na kuwatelekeza wanafunzi wao. Jamani kwa hali hii elimu itakuwa bora kweli. . . Mh
 
Naona nisipotoa wazo langu nitakuwa simsaidii mjukuu wangu atakaezaliwa miaka 30 ijayo...awali ya yote poleni nyote mlioshindwa kufanya vibaya katika mitihani yenu ila mkumbuke usemi wa wanafalsafa wa kale kwamba kufaulu au kushindwa ni sehemu ya maisha sio katika mtihani tu wadogo zangu......tukija katika chanzo naweza kutoa sababu nyigi ila leo hii nina hizi chache kwanza ni mwanzo mgumu wa huu mfumo endelevu wa shule za kata ambapo uchache wa maabara, walimu, vitendea kazi, na thamani mbalimbali.Pili ni mazingira magumu ya baadhi ya shule ambapo huwezi kumshawishi mwalimu mwenye umri mdogo akaishi sehemu ambayo kuyazoea mazingira ni lazima ajifunze kunywa mvinyo za kienyeji mbaya zaidi hata malazi yenyewe ni duni achana na masuala ya huduma ya maji na chakula ambapo unaweza kuwatuma wanafunzi ambao matokeo yao ni hayo tunayoyaita ni kufeli.Tatu ni utandawazi uliokithiri sababu wanaofeli sio wale wa vijijini tu pia huku kwetu mjini utandawazi umezidi kiasi kwamba mwalimu na mwanafunzi maisha yao ni kama panya na paka piga picha kama paka ndio ni mwalimu na enzi zile hayo hayakuwepo kwanini mwalimu asijitoe na hapo ndio neno ualimu ni wito lilipozaliwa...yapo hayo na mengine ngoja niache ukumbi kwa wengine.
 
naungana na wote waliosema ukosefu wa walimu,vifaa vya kufundishia kama maabara etc na walimu kutokuwa na mishahara inayoridhisha na mazingira mazuri ya kuishi ni sababu zinazochangia matokeo kuwa mabaya.
Serikali inahitaji kujipanga sana kwenye hii wizara,kila kitu hakipo sawa na inavyoelekea huko mbele hali itakuwa mbaya zaidi.........hakuna mwalimu anayetaka kukaa shule kwa masaa 8 kulipwa laki na themanini kwa mwezi ambayo akifundisha tuisheni kwa siku tatu anapata....au kukaa shule ya kata aliyopangiwa kulipwa hiyo laki moja na nusu tena kwa kuchelewa na mwenzie wa private mwenye qualification kama zake akilipwa laki sita au hata na zaidi.....serikali iboreshe mishahara na mazingira ya walimu kufanya kazi na ya wanafunzi kusoma otherwise mtoto wa maskini atabaki kuwa maskini.......

Nafikiri kuna haja ya kufanya monitoring and evaluation ya mikakati yote ya uboreshaji wa elimu ya serikali,ili kuweza ku-priotise waanzie wapi kubadili hali hii,lasivyo wakienda kisiasa,hakutakuwa na improvement,manake wanasiasa wanatamka lolote ku-gain publicity na kura,utekelezaji sifuri.......wanaoumia ni maskini wanaowapigia makofi na kuwapa kura.
 
...Wizara ya elimu akabidhiwe yule kanali MNANI aliyewacharaza waalimu wa shule ya msingi kule mkoani kagera.
 
Mimi natoa wito kwa serikali kwamba badala ya Kurudisha National Service ya kupigishana kwata, ni bora Wakaifanya kwa kuchukua vijana wetu waliopata division 1 mpaka 2 form six kuwatrain na kwenda kufundisha kwenye shule hizi mpya za kata japo kwa miezi Sita wakati wakisubiri kujiunga University hii iwe inafanyika kila mwaka , na wale waliopata division 3 mpaka 4 lakini wana pass nzuri za O-level wanaweza kwenda kujitolea kufundisha primary kwa kipindi cha muda kadhaa. kwa kufanya hivi serikali iwahakikishie mkopo wenye masharti nafuu wa kusoma katika vyuo mbali mbali, na ofcourse iwapatie vijisenti kadhaa vya kujikimu[ siyo full salary].
Utaratibu huu pia unaweza kusaidia katika shughuli mbali mbali za maendeleo kama kuhamasisha kilimokwanza, kupambana na ukimwi, kutoa elimu ya uraia n.k, wapo vijana vichwa vizuri tu wakipewa chaki kuwapigia wenzao mbona utawakubali, by the way mimi nimepitia TUITION, na waliokuwa wantupigia mbona ni vijana wenzetu(siyo walimu by profession), lakini mambo yakawa mazuri?
 
Shule za kata kufundishwa na form 6 leavers regardless of the results.

Wanafunzi kulundikana kupita kiasi hivyo waalimu kushindwa kufuatilia maendeleo ya wanafunzi. Kumbuka kuwa wanafunzi wa O level bado wanahitaji uangalizi sana.

Masilahi duni ya waalimu

Kudharau shule za serikali na kata, maana watoto wa vigogo wapo special schools

Waalimu kupunguzwa kutoka katika shule kongwe na hivyo shule kongwe kuwa na upungufu wa waalimu
Shule kongwe pia kuongezewa wanafunzi bila kuongeza miundo mbinu

Serikali hii inafanyaje
 
hao 11 ni wale wenye div 1-3 wenye uwezo wa kuendelea kwa hiyo watakaopata vyeti vya 4m 4 ni asilimia 50 :car:

Nimekusoma mkuu. Ila nashangaa kidogo kama kwa elimu ya TZ mwenye cheti cha F4 kama kitamsaidia popote. Hata kusomea ualimu wa chekechea i guess wanataka mwenye div III. Kwa hali hiyo waliofaulu ni 11% na waliopata vyeti vya F4 ni 50%.
 
mwaka 2008, Shule moja inayoitwa High view sec school inayomikiwa na mmoja ya mfanya biashar mkubwa visiwani Zanzibar iliongoza Zanzibar kwa kufanya vizuri yaani ilitoa div 1 zaidi ya 15, div 2 za kumwaga kati ya watoto wsiozidi 50. hii ni mara ya kwanza kwa shule hiyo kutoa idadi kubwa wanafunzi. nadhani hata Baraza la Mitihani la Taifa Necta ilishtuka, iljihoji na ilitaka kujua haya ni matokeo ya Kweli?
Mwaka uliofuta NECTA ilituma ujumbe mzito katika shule hiyo, kwa maneno ya vijana iliwabana vijana sana vijana shule hiyo kwa kuweka Ulinzi mkali kwa usimamizi, ufanyaji wa mitihani, baadhi ya wajumbe kutoka NECTA Makao makuu Walishiriki kikamilifu kusimamia exam shuleni hapo. nasema walishiriki kusimamia, kuchunguza na kuzuia kila aina ya Ujanja, walifikia hata kuwasachi kabla ya exam. matokeo yake wanafunzi waliofanya Exam matukio yao sio mazuri.(naamini hata NECTA kwa hili hawatakanusha).
lKN sijui kama NECTA hufanya mkakati kama huu ktk shule ambazo huwa zinaongoza hasa za seminary? sijui kama wanshtuka kama walivyoshtuka High view? sijui hutumia mkakati kama walivyotumia huko Zenj?

LKN cha kujiuliza jee hawa ndio wanaopta first class Vyuo vikuu? au ndio bogas



Nami niweke neno la ukweli hapa ...seminari hizi unazozisema ni zile za kanisa katoliki ambazo nidhamu ni ya juu ukipewa maelezo ya kukimbia kilomita moja wewe ukaongeza hutasifiwa ila ni utovu wa nidhamu na utapewa onyo la adhabu au kufukuzwa hivyo nidhamu ndio chanzo cha mafanikio hata ukipeleka jwtz waweke ulinzi watafanya vizuri tu.Pili kiwango cha idadi ya wanafunzi ni kidogo chenye uhusiano na taaluma ya kweli darasa moja wanafunzi 25 na kila somo lina mwalimu bora anayelipwa vizuri na huyo mwanafunzi ni mzuri kitaaluma na kitabia unategemea utawalaumu NECTA. Suala sio seminari maana seminari ni jina kama majina mengine ya seminari nyingine zisizo za katoliki.. tafadhali tuwe tunafanya na utafiti ili hii jammiiforum iwe ni nyumba ya watu wa fikara za kiutafiti chakufanya chukua peni tembelea seminari tatu za wakatoliki,tatu za walutheri,tatu za waanglikana, tatu za wapentekoste,tatu za waaadventista{wasbato},tatu za waislamu na hata tatu sekondari za kawaida halafu swali la utafiti liwe je nnini sababu ya mafanikio ya shule zao?hata kma hazina mafanikio najua utapata jambo la kulinganisha huo utafiti........,..NECTA ni fainali tu hata wasipoweka ulinzi na usimamizi kabisa seminari za wakatoliliki zitabaki palepale...niliwahi tembelea seminari moja nikaona table teaching{ufundishaji wa mezani} nenda katka shule za kwetu kule mwalimu na mwanafunzi ni chui na paka...nidhamuuuuuuuuuuuuuu.
 
Hata huko zenji jina lakifanana na John basi unapasi vibaya sana.

Pathetic!!! NECTA =UDINI
CDM = UDINI
Biashara za Mbowe = UDINI na UKABILA

That is all you can think of........uwelewa wenu upo ndani ya radius isiyozidi 15Km kutokea hapo mchambawima ulipo sasa hivi.
 
msemakweli huuawa kabisa kama sio kupingwa......nidhamu, juhudi na maarifa ndio kiongozi cha seminari licha ukiondoa syllabus ambapo wote wanaongozwa na hiyo...na hilo nalo tulijue wanajamii.
 
Haika,
Huo ndio uzalendo. Keep it up.
Ni vizuri tukaangalia vijana wamefelije kwenye shule zote bila kujali inamilikiwa na nani kwasababu mwisho wa siku, hao waliofeli watakuwa bado ni watanzania wenzetu na tutahitaji walete maendeleo kwa nchi bila kujali wanaamini dini gani.

Great thinkers, naomba tuachane na ushabiki wa kidini, hauna tija as usual mbali na kuleta maumivu tu kwenye roho zetu.

safi sana...na unakuwaje wewe ni great thinker? na wakati hata magreat thinkers hawakuleta udini wala vijembe ila walichallenge ili kuboresha ukweli ni uleule tuwasaidi kimawazo ili watoke kwenye pango la giza sio udini hapaaa.
 
Back
Top Bottom