MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

Jamani, Kama
waliofaulu katika Division I mpaka III ni
40,388 kati ya waliofanya mtihani
wanafunzi 441,426, hivyo hiyo kwa
hesabu za haraka na rahisi ni asilimia
9.15% tu na siyo 11.50% kama
magazeti yanavyonukuu kuwa NECTA
imesema.
Kama waliofaulu ni 177,021 kati ya
wanafunzi 441,426 waliofanya mtihani
wa kidato cha nne, hivyo waliofaulu
wote (Division I mpaka IV ni asilimia
40.102% tu na sio inavyoandikwa
kwenye magazeti kuwa ni 50.4%
Kutokana kuwa waliofahuru ni 40.102%,
hivyo ni wazi kuwa ambao hawakufaulu
ni asilimia 59.898 (karibu 60%). Na hii
ndiyo asilimia halisi/ya kweli ambao
hawakufaulu.

My take; tarehe 5,february jumamos tuandamane! Tunapinga ubovu wa shule za kata,,, na uimara wa shule za kulipia!!
 
Jamani, Kama
waliofaulu katika Division I mpaka III ni
40,388 kati ya waliofanya mtihani
wanafunzi 441,426, hivyo hiyo kwa
hesabu za haraka na rahisi ni asilimia
9.15% tu na siyo 11.50% kama
magazeti yanavyonukuu kuwa NECTA
imesema.
Kama waliofaulu ni 177,021 kati ya
wanafunzi 441,426 waliofanya mtihani
wa kidato cha nne, hivyo waliofaulu
wote (Division I mpaka IV ni asilimia
40.102% tu na sio inavyoandikwa
kwenye magazeti kuwa ni 50.4%
Kutokana kuwa waliofahuru ni 40.102%,
hivyo ni wazi kuwa ambao hawakufaulu
ni asilimia 59.898 (karibu 60%). Na hii
ndiyo asilimia halisi/ya kweli ambao
hawakufaulu.

My take; tarehe 5,february jumamos tuandamane! Tunapinga ubovu wa shule za kata,,, na uimara wa shule za kulipia!!
 
Udini hautaisaidia nchi yetu tuachane nao. Dini iwe ya mtu na mungu wake na sio kero na usumbufu kwa watu wasio wa dini yako.

kwenye mada hii udini uko wapi?, hivi wewe huwaonei huruma hawa watoto ambao future zao zinaharibiwa na kusomeshwa katika shule ambazo waliozianzisha ni "irresponsible comunity/society/parents", kinachoelezwa hapa ni wenye shule hizi waamke usingizini waache kuangamiza vijana wetu na si udini. Kama unadhani ni udini ndo maana maendeleo hayapatikani.
 
Kinachotakiwa ni kufanya Research yaani utafiti wa kisayansi zaidi kuliko kiimani. Mtafiti achague shule tofauti tofauti kutoka kila mkoa au wilaya kuzingatia seminari za dini zote, za serikali/kata na kuchunguza mbinu zinazotumika. Kwa ufupi tatizo kubwa ni waalim na masilahi yao, malezi nje ya madarasa,vitabu vya kiada na ziada, maabara, ufaulu wa wanafunzi (Darasa la saba) wanaokwenda katika shule za kulipia, mfumo wa kutoa elimu za dini n.k. Isitoshe shule nyingi za St. sio seminary ni majina tu ili kupata unafuu fulani au kuaminika lakini umiliki sio wa taasisi za kidini.

analysis yako ni nzuri, lakini hebu tuwe objective zaidi: ukiangalia katika orodha ya shule 10 bora za mwaka huu nyingi ni truly za dini ya kikristo tena roman. Nakubalina nawewe kuwa inawezekana kinacho wafaulisha ni mazingira, mbinu na vifaa vya ufundishaji, je huoni sasa kama ni muhimu wamiliki na waendeshaji wengine kuwa na jambo la kujifunza kutoka hapa?.
 
Nadhan hili suala la shule za kiislam kufelisha sana tulichukulie serious kidogo.... Cdhan kama tatizo ni dini yao au imani yao... Nnadhan tatizo ni walimu wao pamoja na techniques wanazozitumia!...

wao hizo technik za kufundisha wanazipata wapi?, hao walimu wao wanawapata wapi?. Mimi nadhani uislam(brotherhood) inachangia. Nadhani wanapotoa ajira priority huwa ni mwenzao hata kama anauwezo hafifu na hawana cha kujifunza kutoka kwa taasis nyingine .
 
Sioni sababu ya kukata tamaa nahizi shule zetu za kata Tanzania au shule nyingine zozote hata hizo uziitazo Islamic School.

Wahindi walipoanzisha Univerisities zao miaka ya 1950 na 1960 Dunia nzima walikuwa wakicheka na kubeza.
Leo nchi nyingi duniani zinapeleka wanafunzi wake iIndia kusoma katka vyuo vile vile vilivyo dharauriwa miaka iliyopita.
Pia wahindi wanaexport Maengineer na Madaktari Dunia ya kwanza, waliocheka wanashindwa kuendelea kucheka kwa sababu wakicheka wanajicheka wao wenyewe.

Jambo kubwa na la Muhimu ni kuorodhesha matatizo sugu ya shule zetu za kata kuyaweka wazi na kuyavalia njuga kitaifa na kimataifa ili kutafuta suruhisho. Kukebehi, kukashifu kubeza shule ambazo tayari zimekwisha anza na kuthubutu kutoa walau few division IV ni kujididmiza kijamii na kifikra. Kudhani shule ikiwa ni ya Waislamu basi nia na madhumuni yake ni kufelisha wanafunzi wake huo ni uchuro nisio weza kuufumbia macho. Mtu au watu wenye maono kuliko maono yako yote utakayo ona katoka maisha yako ndiyo waliyoanzisha shule hizo unazo zikebei. Lengo la kuanzisha shule hizo lilikuwa ni kuwakomboa Watanzania na litaendelea kuwa hivyo hivyo hadi mwisho wa wakati

Kibohehe Sec School shule ya Bakwata iimesomwa na wanafunzi wengi Wakristo kwa Waislamu na wengi wamefika level ya University bila kelele wala mikwaruzo. Suala la Islamic School kuwa ni recipe of failure ni suala lisilo jenga na binafsi silikubali.
Shule zote Tanzania zina Matatizo yanayofanana. Kukosa walimu wenye sifa moyo na Ali. Kikubwa zaidi ni kukosa walimu wenye sifa.

Tunatakiwa kujiuliza kama wananchi wazalendo tutasaidiaje Elimu Tanzania bila kujali nani anasoma pale??
Tanzania haitajengwa na Wakristo au Waislamu pekee yao. Tanzania itajengwa na Watanzania si kwa uzalendo tu bali kwa kutambua kwamba Tanzania ndiyo nyumbani kwao, na ukweli kwamba kama WaTanzania hakuna mahali pengine popote duniani kama Tanzania.


Kushuka kwa elimu Tanzania ni Tatizo la kitaifa halina itikadi japo limesababishwa na utendaji duni wa serikaliya CCM.
Limesababishwa na Viongozi wa CCM kutamani sna ughaibuni kuliko Tanzania aliye mama yao wa kunyonya ziwa.
Kushuka kwa elimu Tanzania kumesababishwa na Uduni wa fikra za viongozi wa CCM kudhani kwamba kuiba Fedha iliyo fungu la Elimu na kuiweka mifukoni mwao bila aibu kutawapandisha chati wao wake zao na vimada uchi wao.
CCM wanajali Shopping Ulaya kuliko Elimu ya vijana wao, wanajali kujivinjari nchi za dunia ya kwanza kwa mbwembwe kuliko ustawi wa Taifa la kesho Tanzania.
Viongozi wa CCM wanadhani kuleta watoto wao kusoma hapa Ughaibuni ni sifa na heshima ya kitaifa japo watoto wao wengi huishia kuvuta bangi na wazungu, kuendeleza umalaya kama baba namama zao na hata kuishia jela kwa kushop lift.

Tuige mfano wa wenzetu wahindi walioanzisha vyuo vikuu kwenye mabanda ya Mabati na kuzvibadili taratibu hadi kufikia kiwango cha kimataifa.
Ni sisi wenyewe Watanzania ndiyo wenye uwezo wa kubadili mweleko na mwamko wa elimu Tanzania.
Viongozi wa CCM wameshindwa sisi wananchi ni lazima tuweze

Ni aibu hapa JF na mahali popote duniani hata kwenye sayari ya Mass kudhani shule ikiwa ni ya Kiislamu basi iko after kuferisha wanafunzi wake.

Kuishi kwangu kote mitaani na waislamu wengi sijawahi kuwa na ugomvi na Muislamu yeyote unao husu dini imani au kitabu cha dini.
Ugomvi wa maneno kuhusu imani yangu dhidi ya imani ya kiislamu nimeupata mtandaoni. Kuna mitandao kibao ambayo kazi yake kubwa ni kutoa kashfa zisizo kubaliwa hata na imani zao dhidi ya imani nyingine.

Wote tujiulize, tutasaidiaje kuinua kiwango cha Elimu Tanzania katika kipindi hiki ambacho tunajipanga kuiondoa CCM mdarakani na baada ya kuiondoa madarakani?? Tuna mikakati gani??
 
Nawasalimu wanamember wenzangu wadadavuaji wa mambo..yani cjui macho yangu yameona vibaya au ni vipi?ni hivi katika gazeti la jana la nipashe-28th january 2011 nimeona kama kuna picha la skuli ya makamba katika darasa mojawapo,je waungwana mazingira kama haya ni mazuri na yatachangia matokeo mazuri au mwenyejina YUSUPH MAKAMBA anaona fahari kwa hayo matokeo,na ningemwona mwenye busara kama hayo matokeo angetolea ufafanuzi kama anavyokuwa mwepesi wa kufafanua mambo huku akinukuu vifungu vya holy bible na holy quran...wanajf ninachoomba kwa mwenye gazeti la jana anipatie picha ya hlo darasa la makamba sec. school...nawasilisha mada
 
mfumo wetu ni mbaya sana; sioni sababu ya kwanini matokeo ya mitihani hii ya kiwango cha chini yanawekwa kwenye mtandao tu. Hivi hakuna uwezekano wa matokeo kupatiwa mtoto moja kwa moja badala ya kuyaweka hadharani? aliyeshinda anajua kashinda yeye na familia yake na aliyefanya vibaya yeye na familia yake wanajua. I DON'T LIKE THIS SYSTEM. Hatujali kabisa hisia za hawa watoto. Wengine wanafikiria hii ni aibu ya "watoto wa Kiislamu"; hii ni aibu yetu kama Watanzania.
 

HakiElimu yabeza ushindi wasichana kidato cha IV

Imeandikwa na Lucy Lyatuu; Tarehe: 28th January 2011 @ 23:57 Imesomwa na watu: 203

BAADA ya wasichana waliomaliza kidato cha nne mwaka jana kufanya vizuri kwenye mitihani hiyo na kuchukua nafasi nane za kwanza, Shirika la HakiElimu na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wamebeza ushindi huo na kusema ni wa chini.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa Januari 26 na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) wasichana wanane walishika nafasi hizo huku wakiwaongoza wavulana wawili katika kundi la 10 bora.

Hata hivyo taasisi hizo mbili zisizo za Serikali zimesisitiza kuwa bado kiwango chao cha ufaulu kiko chini kikilinganishwa na cha wavulana ambao zimesema bado wako juu.

Aidha, wamesema ipo haja sasa ya kutenganisha taaluma na siasa na kusimamia kwa dhati sera na mikakati ya kuboresha elimu, ili ifikie mahali elimu iwe ya kumkomboa mwanafunzi.

Hali kadhalika walitoa mwito jana wa kutekelezwa ahadi za elimu zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni mwaka jana, ili kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kisiendelee kushuka.

Akitoa tathmini ya matokeo ya kidato cha nne jana Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Elizabeth Missokia, alisema matokeo ya kidato cha nne yaliyotolewa na Necta yanaashiria hali ya hatari kuhusu mwelekeo wa elimu nchini.

Katika matokeo hayo, wanafunzi 40,388 kati ya 352,840 ya waliofanya mtihani huo ndio waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu, ambapo ni dhahiri kuwa ufaulu huo ni mdogo ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi 310,826 waliopata daraja la nne na sifuri.

Missokia alisema kwa mujibu wa matokeo ya jumla, wavulana wamefaulu kwa asilimia 56.28 na wasichana asilimia 43.47 huku takwimu hizo zikionesha kuwa wasichana wana ufaulu wa chini kwenye idadi ya ufaulu wa kiwango cha daraja la kwanza hadi la tatu.

Alisema takwimu zinaonesha wavulana waliofaulu kwenye ngazi hizo ni asilimia 14.6 na wasichana asilimia 7.81 ambayo ni tofauti kubwa na kwa ufaulu huo haiwezekani kujivunia idadi ndogo ya wasichana kuwa kwenye 10 bora wakati ufaulu kwa ujumla unaonesha bado wako chini.

“Ikumbukwe, kuwa taarifa zinaeleza idadi kubwa ya wasichana wanaendelea kukatisha masomo yao kutokana na mimba za utotoni na mambo mengine,” alisema na kuongeza.

“Hatuwezi kujifariji kwa kuangalia ufaulu wa wenzao wachache wakati huo huo fursa za walio wengi zikibinywa, malengo ni kuwaendeleza wote; wasichana na wavulana kwa haki sawa,” alisema Missokia.

Alisema anguko hilo la ufaulu limewakumba watoto wengi wanaosoma shule za kata ambapo wadau wengi wa elimu na watoto wenyewe, wamekuwa wakipigia kelele changamoto zinazowakabili kama uhaba wa walimu, mazingira duni ya kujifunzia, uhaba wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia na hamasa ndogo ya wanafunzi.

Missokia alisema hakuna haja ya kulumbana wala kuingiza siasa kwenye elimu, bali Serikali itekeleze mipango na sera zilizopo na kuondoa upungufu kwa kushirikisha wadau, kwa kuwa
nchi haiwezi kuendelezwa na watu wachache wanaopata fursa za kipekee kwenye shule chache huku elimu pana ikiwa shakani.

Ofisa Mchambuzi wa Sera na Uhamasishaji wa TENMET, Florence Francis, alisema matokeo hayo yanaashiria kwamba hatima ya watoto wengi walioko shuleni iko shakani kwa kuwa kati ya shule 4,266 za sekondari nchini, robo tatu yao ni za Serikali pamoja na shule za kata, ambako ndiko wanakosoma watoto wengi wa Watanzania masikini.

Alisema anguko kubwa la wanafunzi kwenye sekondari za kata na za Serikali linamaanisha ni anguko la maelfu ya Watanzania wanaosoma katika shule hizo.


 
mathematics ni tatizo kubwa in tz na walimu ndio vikwazo maana ukiangalia results mashuleni kama wamefeli basi wanafeli wote kama wakifanya vizuri basi wengi wao wanafaulu. nadhani kuwepo na michakato mashuleni ya kutambua uwezo wa walimu ktk masomo wanayofundisha.
 
Code:
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa Januari 26 na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) wasichana wanane walishika nafasi hizo huku wakiwaongoza wavulana wawili katika kundi la 10 bora. 
 
Hata hivyo taasisi hizo mbili zisizo za Serikali zimesisitiza kuwa bado kiwango chao cha ufaulu kiko chini kikilinganishwa na cha wavulana ambao zimesema bado wako juu. 
 
Aidha, wamesema ipo haja sasa ya kutenganisha taaluma na siasa na kusimamia kwa dhati sera na mikakati ya kuboresha elimu, ili ifikie mahali elimu iwe ya kumkomboa mwanafunzi.

Bila ya kupambana na umasikini na kujenga mazingira mazuri ya soko la ajira binafsi.................umuhimu wqa elimu kwa watoto wetu utakuwa mdogo sana.......na hawataona matunda ya kujiendeleza kwa sababu mafanikio yake hayaonekani kwenye jamii............
 
hilo ni la muda mrefu hata sasa watu bado hawaoni matunda ya elimu kumekua na kundi kubwa la unemployment elimu yetu haimwandai kijana kwa ajira binafsi

Code:
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa Januari 26 na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) wasichana wanane walishika nafasi hizo huku wakiwaongoza wavulana wawili katika kundi la 10 bora. 
 
Hata hivyo taasisi hizo mbili zisizo za Serikali zimesisitiza kuwa bado kiwango chao cha ufaulu kiko chini kikilinganishwa na cha wavulana ambao zimesema bado wako juu. 
 
Aidha, wamesema ipo haja sasa ya kutenganisha taaluma na siasa na kusimamia kwa dhati sera na mikakati ya kuboresha elimu, ili ifikie mahali elimu iwe ya kumkomboa mwanafunzi.

Bila ya kupambana na umasikini na kujenga mazingira mazuri ya soko la ajira binafsi.................umuhimu wqa elimu kwa watoto wetu utakuwa mdogo sana.......na hawataona matunda ya kujiendeleza kwa sababu mafanikio yake hayaonekani kwenye jamii............
 
Hahahaaa kumbe bado wananyanyaswa!! si Nyerere hayupo tena? JK na top leaders si wakwao? mbona bado? so simple conclusion, Hawa jamaa ni wavivu tu wakusoma!
 
hahahaaa kumbe bado wananyanyaswa!! Si nyerere hayupo tena? Jk na top leaders si wakwao? Mbona bado? So simple conclusion, hawa jamaa ni wavivu tu wakusoma!

s1921 luqman islamic seminary


div-i = 0 div-ii = 0 div-iii = 1 div-iv = 38 fld = 3
 
nawasalimu wanamember wenzangu wadadavuaji wa mambo..yani cjui macho yangu yameona vibaya au ni vipi?ni hivi katika gazeti la jana la nipashe-28th january 2011 nimeona kama kuna picha la skuli ya makamba katika darasa mojawapo,je waungwana mazingira kama haya ni mazuri na yatachangia matokeo mazuri au mwenyejina yusuph makamba anaona fahari kwa hayo matokeo,na ningemwona mwenye busara kama hayo matokeo angetolea ufafanuzi kama anavyokuwa mwepesi wa kufafanua mambo huku akinukuu vifungu vya holy bible na holy quran...wanajf ninachoomba kwa mwenye gazeti la jana anipatie picha ya hlo darasa la makamba sec. School...nawasilisha mada

s1806 yusuf makamba secondary school


div-i = 2 div-ii = 4 div-iii = 19 div-iv = 113 fld = 314
 
Back
Top Bottom