MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

Nadhani makamba angekuwa na la kujivunia kama angehimiza uchangiaji wa hiyo shule kama madawati,vifaa vya maabara, vitabu nk ili kuboresha elimu.Lakini amebaki kupayuka payuka ovyo bila mpangilio wowote, hapo ndo angejitafutia sifa. Lakini pia hata shule za mama salma.anna mkapa,J Kikwete nazo zimefanya hovyo naona bora wafute haya majina zipewe majina ya mitaa zilipojengwa hizi shule manake hayo majina hayana msaada wowote kwao.KUna haja ya kuangalia upya umuhimu wa hizi shule hasa za kata kwanini wamefelei hivo? kwa div 4 wengi watahonga waende ualimu unadhani wakipewa ualimu si ndo elimu kwisha kabisa....na wengineo wataingia mitaani kufanya biasharara wkt hawana mtaji. Tetegemee hapa majambzi, machangu wengi nk yale yale ya Tunisia.....
 
uongozi ukibadilika kama walimu ni vihiyo itasaidia? maabara zipo?? madawati ndo hakuna wanakaa wapi??? je maktaba zipo????? nadhani bado kuna kazi hapa.
 
Katika kuangalia jinsi CCM inavyoua elimu kwa watoto wa wapiga kura wake nimekutana na shule inaitwa Jakaya Kikwate ...sijui iko wapi! Kuna matokeo ya form 4 hapa ambapo kati ya watoto 124 waliofanya mtihani % 61 wamepata sifuri .! na wengine walio baki wameambulia DV 4 ZA KUFA! KILICHONISHANGAZA NI HIYO ASILIMIA YA 0,KUFANANA NA ASILIMIA ALIZOPATA MH JAKAYA KIKWAETE KATIKA UCHAGUZI ....WHAT A KOINSIDENSI!
Nawapa pole vijana hawa lakini huo sio mwisho bado wananafasi ya kupiga kura



Kwenye red mkuu! you have made me day!! teh teh teh teh teh!!😛eep:
 
Ni ugonjwa mbaya sana huu! hakuna kitu ambacho unaweza ukashauri kifanyike hapa ili kuendeleza maendeleo ya hiyo shule. Simply because the whole education system needs a massive reforms. Na hii ni ktk ngazi yote toka Wizara mpaka huko chini, we are lacking competitive individuals in the system, majority of the professionals have been appointed only by favoritism and this is why we are lacking efficiency, creativeness, ambition, awareness, loyalty and creativeness. Hivyo dawa hapo ni ku get rid of the minister of education & Co, BUT THIS IS A DAY LIGHT DREAM! Because i can't see it happening since the president is falling in the same trap. Tunaelekea pabaya zaidi, We desperately need changes! inatisha!
 
Nina amini kabisa kama wanafunzi wa shule hiyo ya High Sec wangekuwa robo tatu yao ni wakristo watupu basi hao wanafiki toka baraza la mitihani la taifa wasingeenda huko Visiwani kusimamia zoezi zima la kufaya mitihani, kwani wewe huwajuwi Wakatoliki ndugu yangu?
 
Sababu za wanafunzi kufeli wengi wanasema ni shule kukosa majengo bora na madawati!!!

Inashangaza leo hii wanafunzi wanakaa alau kwenye sakafu zenye saruji na si udongo! Na wanafeli! Inashangaza sana leo hii wanafunzi wanapewa alau nauli za kuwasaidia kutoka na kwenda shule HAWAPIGI GOMBO toka Mwenge mpaka Uhuru mchanganyiko! na wanafeli!! Haisemwi alau siku hizi wanafunzi wanasoma mpaka saa tisa tu! hawafikishi saa kumi na mbili jioni kwa sababu kuna SOMO LA MICHEZO! na mchana wamekunywa maji safi ya chupa na si kukinga na kunywa maji kwa kutumia mikono na WANAFELI!!!

LAKINI HAKUNA ANAESEMA KWAMBA WALIMU BADO WAPO KWENYE MGOMO!!!

Hakuna anaetaka kusema WANAFUNZI Walikuwa kwenye ushabiki wa SIASA na UCHAGUZI!

Hakuna anaetaka kuthubutu kusema "ASILIMIA HIYO THEMANINI NA USHEI YA WALIOFELI NI WATOTO WA WALALAHOI" Kwa maana watoto wa WALALAHAI hawasomeshwi nchi hii kwa sababu wanaandaliwa kuwa WATAWALA!!

NA HUKO WALIKO Ughaibuni, HAWAGOMI hata kama wazee wao hawajawapelekea posho ila wao hutoroka na kwenda kujirusha. Watapata tu vyeti vyao maana wanasoma kwa pesa na majina! Watoto wa Walalahoi wao badala ya kujibidiisha na kusoma kwa kila aina ya njia inayowezekana wanadumbukia katika mtego wa maandamano na migomo! Wanasahau kwamba migomo na maandamano yao ndio kifo chao na elimu yao! (gomeni madogo wala msikubali kubabaishwa - ipo siku mtatambua kwamba mliowatumikia hawapo pamoja nanyi!)

Wala hakuna anaetaka kuhoji NI KWANINI NCHI HII VIONGOZI WANAKUBALIWA KUPELEKA WATOTO WAO WAKASOME NJE YA NCHI, KWANINI ISIPITISHWE SHERIA YA VIONGOZI WA SERIKALI WATOTO WAO WASOME KATIKA SHULE ZA SERIKALI. (Kwa maana zikiwa mbovu watakuwa na uchungu nazo) Na hawatathubutu kuwaambia walimu "kama hamuwezi kufundisha kwa mshahara huo nendeni mkalime!" Alipata kuwajibu walimu Mh. Waziri mmoja wa JMT!! Na sasa Walimu majibu yao ya kulima badala ya kufundisha yameanza kujitokeza!!!
 
NI zaidi ya mgomo wa walimu..

Ni mchanganyiko wa mambo, wanafunzi wanaweza kuwa sababu pia...

Mazingira, mtihani na hata usahihishaji unaweza kuwa chanzo pia..tufanye utafiti tufahamu kablay kufanya conclusion.
 
NI zaidi ya mgomo wa walimu..

Ni mchanganyiko wa mambo, wanafunzi wanaweza kuwa sababu pia...

Mazingira, mtihani na hata usahihishaji unaweza kuwa chanzo pia..tufanye utafiti tufahamu kablay kufanya conclusion.
Ndugu, basi unadhani hata tunao muda wa kufanya utafiti sasa? Tunatafuta nani atwishwe hilo zigo la wanafunzi kufeli na kufelishwa mchezo uishe!! Inasikitisha sana, kama ni kujenga taifa la wajinga nadhani sasa tunastahili hata kupewa nishani. Wazazi wana uchungu watoto wasome ili wakomboke katika lindi la ujinga. wanafunzi baadhi (walio wengi) wao hawana habari wala hawajali kwa maana hawajui nini maana ya elimu (WENGI WAO WANADHANI WAMEPELEKWA SHULE ILI WAKUE!) hawahitaji kujiuliza mara mbili kwa jambo lililo kinyume na lililowapeleka mashuleni! Inasikitisha mtu amerudia mtihani na anafeli tena!! Watahiniwa binafsi wametuangusha sana safari hii, zile alama walizopata awali wengi wao wamerudia kupata hizohizo ama pungufu zake (yawezekana kabisa wasahihishaji nao wapo kwenye mgomo! au wamechakachua mitihani maana umeshakuwa mtindo- Kiukweli pafanywe utafiti wa kina)
 
Lakini waislam mbona mnapenda sana kulia lia na mambo ya wakristo? Mbona na ninyi madrassa zenu watoto wanapasua pepa kinoma lakini sisi hatu lalamiki?
 
majina mara nyingi huenda sambamba na vijatabia vya wahusika, majina mengine hua yana gundu, we ona yaliyotokea kwa shule ya jina la makamba.
 
A looser can not make a winner!Hamna cha kushangaza hapo...wanafuata mkondo wa mwenye jina!
 
Matokeo ya kidato cha nne 2010 yanatishia hatima ya nchi yetu,na tusipobadilika na kuona umuhimu wa elimu bora katika zama hizi za ubepari,basi kama taifa tumekwisha.
Hebu angalia matokeo ya Shule ya Sekondari Lufyilo ambayo ipo katika wilaya ya Rungwe,Lufilyo ndio nyumbani kabisa kwa Prof:Mark Mwandosya,waziri wa maji.

Summary ya matokeo ni kama ifuatavyo;

DIV-1=0
DIV-2=0
DIV-3=2
DIV-4-47
FLD- 73
 
Thread ilianza kwa hoja nzuri lakini ikaja kubadilika katikati kwa hawa wapuuzi mujahedeena na Benedectas.

Watu wanashindwa kuwa hata na akili za kufikiria kwamba kwanini shule nyingi zimefanya vibaya.

Seminari ziko nyingi wasichana kwa wavulana, je wanawake wakianza kubeza wanaume kwamba hawakufanya vizuri kwenye mitihani ingekuaje?

Matokeo ya taifa kumi bora kuanzia wa kwanza mpaka wa sita ni wanawake ikafuata saba mvulana kutoka Ilboru nane mvulana kutoka Moshi tech, zote kumi bora zilizofuata ni wasichana ina maana hakuna seminari za wavulana?

Wengine wanasema matokeo mabaya shule za kata.
Nataka niwapongeze watoto wa masikini kutoka shule za kata ambao wamefanya vizuri hata kupita kwenye mashule makuu yanayojulikana.

Nimechukua shule moja ya kata kutoka kule Tanga ili kuonyesha kwamba watoto waliosoma kwenye mazingira mabovu, upungufu wa walimu, msongamano wa wanafunzi kwenye madarasa, ukosefu wa maabara lakini pamoja na umasikini wao wameshindana na watoto wa kupikwa ambao shule zao kila kitu wanacho.
http://www.moe.go.tz/NectaResults/CSEE2010/s1282.htm

Hao wa hap juu wamesoma kwenye mazingira ya kimasikini

http://www.moe.go.tz/NectaResults/CSEE2010/s0622.htm

Hawa watoto wa wazazi wenye pesa.
http://www.moe.go.tz/NectaResults/CSEE2010/s1085.htm


My take: ushukaji kiwango cha elimu umechangiwa kwa kiasi kikubwa na umasikini wa watanzania.
Watoto wengi wamesoma kwenye mazingira ya umasikini, shule zisizokua na walimu au maabara.

I,m shure watoto wengi wangefanya vizuri kama mazingira yangekua mazuri.

Shule kama Marian hata kama angepelekwa muuza vitumbua kule maandazi road angepita.
 
Back
Top Bottom