SoC02 Matokeo ya Kidato cha Nne lazima yachunguzwe

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 22, 2022
Posts
7
Reaction score
3
UTANGULIZI.

Ni miaka mingi sasa, kuna ukakasi katika mfanano wa Matokeo ya Kidato cha Nne na Sita, Licha ya kuwepo mfanano huo kuna Utofauti wa Matokeo hayo baina ya Skuli na Skuli, wilaya na wilaya, Mkoa na mkoa hata katika ngazi ya Taifa ambapo kuna baadhi ya Skuli zinaonekana kung'ra huku nyengine zikishika nafasi za mwisho kila msimu.hapa kuna viashiria vya wazi kuwa matokeo sio mazuri kwa wanafunzi wote na wakati mwengine baadhi ya skuli hukosa hata Mwanafunzi mmoja ambae anawakitisha Skuli kwa kusonga mbele.hali hii kwa asilimia kubwa huzikumba Skuli za serekali ukilinganisha na binafsi hali hii inatufanya tuchunguze Matokeo haya kwa umakini ili kujua nini chanzo.

CHANZO CHA TATIZO.
Hakuna Hata mmoja ambae anaweza kukataa kuwa Wanafunzi wengi wanapoteza muda mwingi katika kusoma kutokana na kuongezeka kwa Uelewa juu ya Umuhimu wa Elimu na Kuwepo kwa vifaa vya kutosha katika baadhi ya Skuli.

Kwa upande mwengine, Njia ambao Wanafunzi wanatumia kujibu Maswali zinalingana na zile zinazopendekezwa na BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA (NECTA) kutokana na kutoa vitabu vinavyowaongoza Wanafunzi kujibu Mitihani Vitabu ambavyo hutolewa kila mwaka na kila somo. Kwa ithibati hii ni wazi kuwa kuna mambo yanachangia Wanafunzi wengi kushindwa kuendelea;Terejelee dondoo zifuatazo:

Masomo ambayo hayana Tahasusi maalumu yapunguzwe.
Wanafunzi wanapoingia kidato cha nne huwa na ndoto zao ambazo hutoka katika masomo yao wanayosoma, lakini wanakutana na Masomo ambayo kwa kiasi flani yanawanyima uhuru kuegemea zaidi katika masomo wanayotaka kushikilia.hapa ni Lazima kuwe na njia ambazo masomo hayo yanapunguzwa kwao ama kwa kuondolewa kabisa ama kupangiwa tahasusi ambazo wanafunzi maalumu watasoma masomo hayo.hii itasaidia Wanafunzi kuzitambua ndoto zao mapema nankuepusha kutofanya vizuri katika mitihani yao.
ieleweke kwamba kila somo ni muhimu kwa nafasi yake.

Kukosekana kwa misingi bora ya kuwaandaa Wanafunzi kukabilina na Mitihani. Wanafunzi wengi wanapoingia kidato cha Nne hawana uwelewa wa kutosha juu ya kile wanachotakiwa kufanya kwani, bado mawazo yao huhusisha Mtihani wa kidato cha pili na kile cha Nne, wengi wao husoma ili kupata cheti cha kumalizia masomo jambo ambalo wakati mwengine hupelekea cheti hicho kukikosa.Hapa lazima misingi ijengwe kwa kuweka vipaumbele bora vya kuwafanya wanajitambua.

Kutokuwepo kwa Uwiano kati ya Wanafunzi wanaotoka Tanzania bara na Tanzania visiwani(Zanzibar). Kama tujuavyo kuna Wanafunzi wanaotahiniwa na "BARAZA LA MITIHANI LA ZANZIBAR" na wale wanaotahiniwa na "BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA(NECTA) hasa kwa kidato cha Pili jambo linalopelekea utofauti kati ya Wanafunzi wanaopatikana ambao kwa kidato cha Nne wote hutahiniwa na NECTA.ni ukweli uliowazi Wanafunzi kutoka baadhi ya Skuli za Zanzibar hawana uwezo wa kufanya mtihani wa kidato cha Nne ukilinganisha na wale wanaotoka Tanzania bara.Labda hapa Lazima Kuwe na Baraza moja la mitihani ambalo litafanya kazi kwa Wanafunzi wote ili kuepusha tofauti hizo.

Mazingira sio rafiki kwa baadhi ya Skuli.Jambo hili linaweza kuthibitika kupitia baadhi ya Shule ambazo mazingira yake ni ni rafiki kwa kujifunza. Hebu turejelee katika shule zilizoshika nafasi kumi za juu katika matokea ya 'KIDATO CHA NNE' miaka miwili iliyopita.mfano wa Shule hizo ni, Marian boys na Girls, Feza Boys na Girls nk.....Je mazingira yake ni sawa na zile zilizoshika nafasi kumi za meisho?.Mfano mwengine Tuangalie Skuli ya Sekondari Dr.Ali Mohd Shein ya Wilaya ya Mjini-Unguja na Skuli ya Sekondari Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini Unguja, hapa ni wazi kuwa kuna tofauti ya matokeo ambayo yamechangiwa na tofauti za mazingira ya kujifunzia kwa skuli hizo mbili ambazo zote ni Skuli za serekali.

Kuwabagua wanafunzi kulingana na uwezo wao.Suala la kuwatenga wanafunzi wa Vipawa maalumu, Michepuo na Kawaida ni jambo ambalo linachangia kwa kiasi fulani baadhi ya Skuli zionekane zinafanya vizuri na kuleta utofauti wa matokeo ya Mitihani. Mfano Kuna Skuli za Vipawa maalumu za Fidel castro na Lumumba, Pamoja na Skuli za Michepuo ya Sayansi za Tumekuja na Banbella Girls Skuli ambazo Matokeo yake ni Tofauti na Skuli za Bumbwini, Mnyanjani, Makoongwe na Pwani Mchangani. Hapa lazima tuangalie kwa makini.

MAPENDEKEZO.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Taasisi zilizo ndani yake, pamoja na Wadau wa Elimu na Asasi za kiraia kubuni njia ambazo zinaweza kuondoa matatizo hayo ambayo kwa kiasi fulani yanatia doa tasnia ya Elimu nchini.
'Elimu hujengwa na Wasomi imara wanaotokana na mipango toshelevu na endelevu"

Wenu Habibu hamadi haji(manji).
Mwanafunzi.Chuo kikuu ya Taifa cha Zanzibar (Suza).Shahada ya Kwanza ya UALIMU NA SANAA.
Barua Pepe.habybuhaji@gmail.com
simu.0777492109.
 
Upvote 2

Wakati mwengine huwa nadhani haya matokeo yanapangwa kwa kuangalia skuli fulani hasa za Tanzania bara.ifike wakati iangalie kwa makini
 
Back
Top Bottom