Gilbert wa tarakea.
Senior Member
- Feb 2, 2014
- 179
- 82
mi naamini suala la dini sio ishu sana. mimi mwenyewe nilisoma moja kati ya shule za katoliki ila kiukweli sikuwahi kufuatilia imani yao wala wala mambo yoyote yahusuyo dini yao. na nikasoma nikamaliza o-level vizuri, sasa kama tunataka wadogo zetu wafanye vizuri kama hao wa seminari nafikiri tunatakiwa tujiulize ukiondoa imani na dini yao kwenye hizo shule zao ni kipi tunatakiwa tukikopi kutoka kwao. inaweza ikawa miundo mbinu yao ni mizuri ikiwemo maji, umeme, internet, walimu wako wa kutosha, vitabu vipo na vitu vingine vya kujazia. nafahamu kuna wazazi baadhi hawapendi kuwapeleka watoto wao kwenye shule hizo. kuna shule nyingi ambazo wakristo na waislamu wanaweza kwenda kusoma wakaishi poa na kumaliza salama na pia ni boarding ila Je ndo tujiulize zinafaulisha kama hizo seminari za R.C kama jibu ni hapana sasa hawa wenzetu huwa wanafanya nini mpaka shule zao zinafanya vizuri. tukishagundua kitu wanachofanya wenzetu labda nasi tukichukue hicho tukilete huku kwenye hizi mixed school ambazo, wapagani, wakristo na waislamu wanasoma. tuone kama tutafanikiwa kama wao. mfano hiyo shule ya st. Francis binafsi nilianza kuisikia 2003 ila mpaka leo naona inaendelea kufanya vyema ngazi ya kitaifa. anyway ngoja niishie hapa
Hapo umenena. Mimi nilisoma shule ya kiislam pale Dom. Hata siku moja sikuambiwa nikaswali. Mda wa dini ukifika tunaenda kusali kama iman yetu ilivyo. Waislam na wakristo waliokuwa wanajitolea kusoma walifaulu vizuri. Nikasoma advanced shule ya catholic Majengo moshi. Huwezi jua huyu ni mwislamu huyu mkristo, labda uwe na kiherehere kama cha mtoa mada hapo juu. Nafundisha shule ya serikali, kuna waislamu na wakristo wote wanatendewa haki na wale wanaojitahd mwishowe hufaulu. Mtu wa namna hii ya udini hawezi ongoza jamii. Akiwa headmaster ataweka watu kulingana na dini zao. Upuuzi huo.