Game Theory,
Mkuu wangu usidanganyike hata kidogo.. Karume anawekwa na Bara hawezi kuzungumza kwa maslahi ya Zanzibar ikiwa yeye mwenyewe mguu nje ndani. Maalim Sief always stands for his own interest. Anasema saaana kuwavuruga vichwa tu, na kama alivyokosolewa huyu alikuwa Waziri kiongozi, na kisha waziri wa Elimu hatumsikia hata siku moja akipinga Muungano..mbali na hayo hakufanya lolote la maana kw Wazanzibar alipokuwa madarakani.
Mkuu wangu wazee waliopinga Muungano Zanzibar wanajulikana toka siku ya kwanza na wengine kutokujiunga na baraza la Mapinduzi. Na hakuna chombo chenye nguvu Zanzibar na bara kama baraza hilo kwani wasemavyo wao ndivyo itakavyokuwa.
Kama umesoma vizuri taarifa iliyotolewa ni kwamba hakuna masharti baina yao, meaning uchaguzi ujao ngoma ni ile ile..Na kutokana na mfumo wa serikali ya leo hata kama CUF watachukua uongozi Zanzibar, Wazanzibar wtaendelea kuwa ktk hali hii hii kwa sababu tatizo sii kuongozwa na CCM ila mfumo mzima wa madaraka.
Nimewahi kusema kama kweli kuna kiongozi yeyote Zanzibar mwenye nia ya kuvunja Muungano, iwe CUF au baraza la Mapinduzi basi hatua ya kwanza sii kuweka Muafaka baina yao ila kuitisha Refendum, kuwapa wananchi wa Zanzibar nafasi ya kuchagua kuwa huru kujitenga ama laa! Matokeo ya referendum hiyo ndiye yatakayo jenga misingi ya muafaka baina ya bara na visiwani na sio Karume na Maalim Seif..
Imefanyika hivyo nchi zote zilizotaka kuvunja muungano kwa amani, iweje Zanzibar viongozi wake wasifikirie kabisa njia hii isipokuwa zile zinazohusu nafasi zao za kazi?..
.
Mkuu Mkandara, Wanzanzibari waone hivyo hivyo, tena haswa inapotokea ni waarabu wa Pemba. Pamoja na Karume kuwa sio chaguo la Komandoo, ni Chaguo la Bara, kilichotokea anakijua, game lilivyochezwa kumdhibiti Komandoo na chaguo lake, analijua, na kilichomkuta Komandoo na chaguo lake na timu yake nzima sote tunakijua, (complete cut off).
Sasa Karume hataki yamkute yaliyomkuta mtangulizi wake, yeye naye analo chaguo lake, huku kukutana na Maalim ni caveat dhidi ya bara, just incase bara ina chaguo tofauti, then watamback Maalim moja kwa moja to hell with Muungano.
Karume has nothing to loose, siku zake zinahesabika anyway, hivyo kaamua bora Seif kuliko mgombea wa bara. Masharti ya siri baina yao yapo!. Anaeutaka urais wa Znz sio Karume ni Seif, aliyeumia ni Seif, aliyelialia ni Seif leo hawezi kwenda kumlamba miguu Karume for nothing huku watu wake wakiendelea kunyimwa Zan ID na japo walijitokeza kwa wingi day one baada ya mapatano, kesho yake waliendelea kususa kusubiri kauli. Mpaka sasa hakuna kauli yoyote kwa Seif waende, its not for nothing.
Seif naye hii ndiyo karata yake ya mwisho, bado anaamini alikuwa mshindi akipokwa tonge mdomoni, safari hii, alishajipanga sio asipokwe tena, bali kuwahamasisha Wapemba kususia kujiandikisha na kuhakikisha Pemba hakuna kitakachoendelea bora wakose wote at the expense ya damu za Wapemba. Walijipanga kufanya kitu mbaya, Huku kumuangukia Karume sii bure bali ni kuepusha yale yote waliyoyapanga.
Hapa sasa wanaozugwa ni Bara, lets wait for much surprises ahead.