Matokeo ya Maalim Seif Kumtambua Karume

Matokeo ya Maalim Seif Kumtambua Karume

.

Mkuu Mkandara, Wanzanzibari waone hivyo hivyo, tena haswa inapotokea ni waarabu wa Pemba. Pamoja na Karume kuwa sio chaguo la Komandoo, ni Chaguo la Bara, kilichotokea anakijua, game lilivyochezwa kumdhibiti Komandoo na chaguo lake, analijua, na kilichomkuta Komandoo na chaguo lake na timu yake nzima sote tunakijua, (complete cut off).

Sasa Karume hataki yamkute yaliyomkuta mtangulizi wake, yeye naye analo chaguo lake, huku kukutana na Maalim ni caveat dhidi ya bara, just incase bara ina chaguo tofauti, then watamback Maalim moja kwa moja to hell with Muungano.

Karume has nothing to loose, siku zake zinahesabika anyway, hivyo kaamua bora Seif kuliko mgombea wa bara. Masharti ya siri baina yao yapo!. Anaeutaka urais wa Znz sio Karume ni Seif, aliyeumia ni Seif, aliyelialia ni Seif leo hawezi kwenda kumlamba miguu Karume for nothing huku watu wake wakiendelea kunyimwa Zan ID na japo walijitokeza kwa wingi day one baada ya mapatano, kesho yake waliendelea kususa kusubiri kauli. Mpaka sasa hakuna kauli yoyote kwa Seif waende, its not for nothing.

Seif naye hii ndiyo karata yake ya mwisho, bado anaamini alikuwa mshindi akipokwa tonge mdomoni, safari hii, alishajipanga sio asipokwe tena, bali kuwahamasisha Wapemba kususia kujiandikisha na kuhakikisha Pemba hakuna kitakachoendelea bora wakose wote at the expense ya damu za Wapemba. Walijipanga kufanya kitu mbaya, Huku kumuangukia Karume sii bure bali ni kuepusha yale yote waliyoyapanga.

Hapa sasa wanaozugwa ni Bara, lets wait for much surprises ahead.


Pasco na Bob;

Masharti yapo, hayawezi kuwa public lakini yapo. Jiulize kitu kidogo tu, kwanini amtambue wakati kunakucha(alfajiri tena kuchiru)?.

Pia naungana na Pasco kusema kuwa bara wategemee kitu tofauti na matarajio.

Natabiri JK kama akiendelea tena miaka mitano ijayo, unless ajirekebishe nchi itasambaratika mikononi mwake.

GT ametoa analysis nzuri sihitaji kuzirudia.

Karume mdogo anataka urais Zenji na nadhani ni chaguo la Kaka Karume, bara wanamtaka Mwinyi....Maalim Seif awe makini dili halitaiva..
Na Dili likiiva basi Muungano unakwisha, Hivi akina Moyo, Mwkanjuki wapo wapi maana ndo wazee wa FITNA


FP
 
I see it a good start...Mambo hayo wanayofanya yanaingia katika kitabu cha zama zetu, kwahiyo historia itawahukumu wasipocomply, na makaburi yao yatapigwa mawe...
 
Game Theory,
Mkuu wangu usidanganyike hata kidogo.. Karume anawekwa na Bara hawezi kuzungumza kwa maslahi ya Zanzibar ikiwa yeye mwenyewe mguu nje ndani. Maalim Sief always stands for his own interest. Anasema saaana kuwavuruga vichwa tu, na kama alivyokosolewa huyu alikuwa Waziri kiongozi, na kisha waziri wa Elimu hatumsikia hata siku moja akipinga Muungano..mbali na hayo hakufanya lolote la maana kw Wazanzibar alipokuwa madarakani.

Mkuu wangu wazee waliopinga Muungano Zanzibar wanajulikana toka siku ya kwanza na wengine kutokujiunga na baraza la Mapinduzi. Na hakuna chombo chenye nguvu Zanzibar na bara kama baraza hilo kwani wasemavyo wao ndivyo itakavyokuwa.

Kama umesoma vizuri taarifa iliyotolewa ni kwamba hakuna masharti baina yao, meaning uchaguzi ujao ngoma ni ile ile..Na kutokana na mfumo wa serikali ya leo hata kama CUF watachukua uongozi Zanzibar, Wazanzibar wtaendelea kuwa ktk hali hii hii kwa sababu tatizo sii kuongozwa na CCM ila mfumo mzima wa madaraka.

Nimewahi kusema kama kweli kuna kiongozi yeyote Zanzibar mwenye nia ya kuvunja Muungano, iwe CUF au baraza la Mapinduzi basi hatua ya kwanza sii kuweka Muafaka baina yao ila kuitisha Refendum, kuwapa wananchi wa Zanzibar nafasi ya kuchagua kuwa huru kujitenga ama laa! Matokeo ya referendum hiyo ndiye yatakayo jenga misingi ya muafaka baina ya bara na visiwani na sio Karume na Maalim Seif..
Imefanyika hivyo nchi zote zilizotaka kuvunja muungano kwa amani, iweje Zanzibar viongozi wake wasifikirie kabisa njia hii isipokuwa zile zinazohusu nafasi zao za kazi?..

Pasco,
Mkuu wangu nawaelewa vizuri Wazanzibar na hasa viongozi wake..Huyu Maalim Seif atalamba miguu ya wangapi? Toka nimjue kila mara hutafuta mbinu ya kumwingiza ktk utawala wa Zanzibar ili apate nafasi yeye kwa ajili maalum ya haki za Wapemba. That is a fact, hana zaidi ya kutazama kwao na rangi yake kama ulivyosema.

Hata kwa huyo Komandoo alijaribu akakuta ukuta mzito.. Matatizo ya Komandoo yalikuwa within Baraza la Mapinduzi alipotaka kuongeza muda na pia alokusudiwa na wengi hakuweza kushika madaraka kwa sababu bara waliingilia kati kumweka Karume.
Hii ni kanyanga tu mkuu wangu, mtoto wa Mwinyi ana chance kubwa ya kuchukua Zanzibar kuliko Maalim Seif.. mnachoshindwa kuelewa ni kwamba huwezi kuwa rais wa nchi yoyote ikiwa wewe haupo ktk System... iwe bara au viziwani ni lazima uwe mwanachama wa KGB ya nchi hiyo..
Labda Mapinduzi yenyewe yaanze na wananchi kama kule Poland na Nchi za Amerika ya kusini. Ikiwa baraza la mapinduzi hawamtaki Salim kuwa rais wa Jamhuri ya muungano, leo unataka kunambia watampa baraka zao Maalim Seif! mtu ambaye ni hatari kwao kuliko hata Salim akiwa rais wa Jamhuri. Jamani msijidanganye hata kidogo na Siasa hizi.
Kweli Wapemba wanajuana kwa Vilemba, lakini sii Karume kwani yeye sii Mpemba wala hana asili hiyo..



kasome kitabu cha Aboud Jumbe kinaitwa PARTNERSHIP

thx
 
Point less afadhali ungenyamaza..pumba tupu..unatetea uwizi wa kura unaofanywa na CCM ambao kila mtu anajua? kichwa kiko salama au ushabiki imekuondoa akili..mgonjwa wewe
😀 Nilitegemea jibu la kijinga toka kwa mtu mjinga. Ukweli utabaki ukweli. wazenji mmeliwa na ni kwa ujinga wenu tu.
Bado kidogo tu mtaanza kula mapapai mabichi tena!
 
Pasco,
Mkuu wangu nawaelewa vizuri Wazanzibar na hasa viongozi wake..Huyu Maalim Seif atalamba miguu ya wangapi? Toka nimjue kila mara hutafuta mbinu ya kumwingiza ktk utawala wa Zanzibar ili apate nafasi yeye kwa ajili maalum ya haki za Wapemba. That is a fact, hana zaidi ya kutazama kwao na rangi yake kama ulivyosema.

Hata kwa huyo Komandoo alijaribu akakuta ukuta mzito.. Matatizo ya Komandoo yalikuwa within Baraza la Mapinduzi alipotaka kuongeza muda na pia alokusudiwa na wengi hakuweza kushika madaraka kwa sababu bara waliingilia kati kumweka Karume.
Hii ni kanyanga tu mkuu wangu, mtoto wa Mwinyi ana chance kubwa ya kuchukua Zanzibar kuliko Maalim Seif.. mnachoshindwa kuelewa ni kwamba huwezi kuwa rais wa nchi yoyote ikiwa wewe haupo ktk System... iwe bara au viziwani ni lazima uwe mwanachama wa KGB ya nchi hiyo..
Labda Mapinduzi yenyewe yaanze na wananchi kama kule Poland na Nchi za Amerika ya kusini. Ikiwa baraza la mapinduzi hawamtaki Salim kuwa rais wa Jamhuri ya muungano, leo unataka kunambia watampa baraka zao Maalim Seif! mtu ambaye ni hatari kwao kuliko hata Salim akiwa rais wa Jamhuri. Jamani msijidanganye hata kidogo na Siasa hizi.
Kweli Wapemba wanajuana kwa Vilemba, lakini sii Karume kwani yeye sii Mpemba wala hana asili hiyo..
.

Nilipata bahati ya kuhudhuria kampeni za Seif toka 1995 na Karume toka 2000. Kwa kuanzia Karume upstairs ni empty totaly, hivyo alikuwa boya tuu viko vichwa chini yake yeye ni yes man tuu. Hata alipotunisha msuli Butiama kuukataa muafaka, alikuwa si yeye, ni wapambe tuu.

Seif ana siasa za chuki, deep down inside, ukimsikiliza hotuba zake huku unamshudia machoni, utashuhudia chuki kwenye macho yake is for real sio politics tuu kitendo cha kuwahasisha wafuasi wake wasusie kujiandikisha, ni uthibitisho kuwa CUF imechoshwa na chaguzi kiini macho, walikuwa wamejipanga kufanya mambo. Hivyo huku kumkumbatia Karume must be a move of convenience, kuna kitu, sio hiki tuu tukionacho.

Kama ni kweli there is nothing than shaking hands, basi Pemba bado panafuka moshi na chini kuna moto.

Kwa vile Karume ni boya tuu na amekula deal na CUF ili tuu Seif aingie line kumbe ni deal ya kiunafiki, baadaye wale wenye nguvu zao Zanzibar wakamgomea Karume, kitakachofuatia hapo ni dimbwi la damu Pemba, hata huyo Seif hatanusurika maana sasa haya yatakuwa mapinduzi ya Pemba.
 
Hivi siyo hawa hawa ndiwo waliomkoromea JK na timu yake kule Butiama na kudai kuwa waachwe na mapinduzi yao lakini siyo kulazimisha muafaka!! au kuna mambo yametokea wengine hatujui.....inakuwa vipi mshikaji kasubiri mpaka dakika za majeruhi ndio anamwambia CUF apige jalamba, hata hivyo kama nimapatano ya kikweli kweli nijambo la kheli, tuchukue kapu tukavune, lakini kama wanafanya hivyo ili kuwasanifu watu fulani itakuwa upuuzi mtupu.....time will tell
 
Pasco na Bob;

Masharti yapo, hayawezi kuwa public lakini yapo.

Karume mdogo anataka urais Zenji na nadhani ni chaguo la Kaka Karume, bara wanamtaka Mwinyi....Maalim Seif awe makini dili halitaiva..
Na Dili likiiva basi Muungano unakwisha, Hivi akina Moyo, Mwkanjuki wapo wapi maana ndo wazee wa FITNA


FP
Yapo na ni ya siri, Seif atawaeleza wafuasi wake kwa siri na bara will be taken by surprise.

Karume mkubwa na mdogo ni paka na panya, the only two things in common to both of them ni whysky mkubwa yotote mpaka Nyagi kwa sana, mdogo only the finest ones na kona, mkubwa akikata kila kona mpaka na mazagamazaga ya uswazi, huku mdogo akichagua pa kupita.
 
of course baada ya kumtukana JK kule Butiama tunajua kilichotokea baadae

ZANZIBAR ilikosa umeme for more than 1 week..kisa eti kuna kidude kimeharibika na kilitakiwa kununuliwa Sweden ...na of course ilichukua more than 2 weeks kupatikana

Bila kusahau Huyo mlevi Karuume alisahau kuwa kukaa pale amekaa kwa sababu JK huyo huyo ndiye anayempa vyombo vya kumlinda...so ilibidi asomewe RIOT ACT...matokeo yake alifanyanini? well, hakuna siri hapo...jamaa aliamua kurelax na JACK DANIELS

useless kabisa


Kuhusu Muungano...well its obvious GEO-ECONOMICS ndizo zitakazo amua mustakabadhi wa huu muungano, kama mnavyoona kule South Orsetia, Nargono Kabarak,Kosovo,Est Timor na Bosnia
 
Talking of political stunts, I think this one would fall into an XXX category!!
 
Kweli Wapemba wanajuana kwa Vilemba, lakini sii Karume kwani yeye sii Mpemba wala hana asili hiyo..[/QUOTE]

Ingawa Karume si Mpemba lakini mke wake (shadia karume) ni mpemba!
 
hongereni sana wana cuf hongereni watanzania hongereni ccm hongereni chadema na vyama vyote visivyotajwa..,ni furaha isiyoepukika kwa mwaka 2009 kwa mwenyekiti wa cuf s.h.seif kumkubali na kuikubali serikali ya zanzibar........swali lwangu bado nauliza iweje yanatokea karibu na kipindi cha uchaguzi?????embu wana cuf mtutoe hofu kwa hili sababu za kukubaliana na serikali ya zanzibar.......,wapo wanaoongea mengi ambayo kwa sisi wapenda amani hatutaki kuamini embu wana cuf mtutoe hofu kunani???nawatakia heri na fanaka kwa hili uhusiano huu usirudishwe nyuma kama mambo ya zimbabwe.....
 
kasome kitabu cha Aboud Jumbe kinaitwa PARTNERSHIP

thx
Mkuu wangu nimekisoma na ndio maana namwona Jumbe kama mwosha maiti tu..
Mkuu wangu Baraza la Mapinduzi halimhitaji Maalim Seif kabisaaaa kujitenga na bara. Wakitaka kujitenga watajitenga kesho bila mawazo yoyote toka kwa Maalim Seif kwani siasa za Maalim Seif ni rahisi kabisa kwa chama chochote kuzitumia na wakafanikiwa.
leo hii CCM- Zanzibar wakiandaa maandamano kupinga Muungano basi wanachama wote wa CUF watahudhulia na kupongeza hotyuba ya kiongozi yeyote wa CCM.
Mkuu wangu nimeyaona hayo huko Quebec ambako nilikaa kwa miaka minne na hakika huo Ubinafsi wao, kile walicholilia kama zanzibar ndicho kilichoniondoa kule pamoja na wafanyabiashara kibao. Quebec never recover economically pamoja na kwamba referendum ilishindikana..
 
JUMUIYA ya Wanawake wa Chama Cha Wananchi (CUF) imeomba radhi kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kutokana na kitendo cha kumpinga hadharani na kuangusha vilio baada ya kutolewa kauli ya kutambuliwa Rais Amani Karume.
Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wanawake, Zahra Ali Hamad katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Demokrasia na kuhudhuriwa na maelfu ya wanawake wa mikoa mitano ya Unguja.
Wiki iliyopita Katibu Mkuu wa chama hicho, aliwaambia wanachama na wapenzi wa CUF kwamba chama chake kimemtambua Rais Karume kuwa rais halali wa Zanzibar jambo kauli amabyo ilipingwa vikali wa wanachama hao na baadhi yao kuangua vilio wakisema Maalim Seif amekisaliti chama chake na hivyo hawakubaliani na uamuzi huo wa kumtambua Rais Karume.
“Tunakuomba utusamehe kwa hisia kali tulizozionesha wiki iliyopita katika viwanja hivi hivi. Tulikuwa hatujakuelewa. Sasa tumekuelewa na kutoka kwetu tegemea mashirikiano yasiyo masharti katika hili. Kwako ujumbe wetu ni mmoja tu, nao ni kwamba tulikupenda, tunakupenda na tutaendelea kukupenda maana nawe daima umekuwa ukitupenda!” alisema Zahra huku akiungwa mkono wa wanawake wenzake.
Amesema ni jambo la fakhari kuwa wanawake ndio ambao wamekuwa jumuiya ya mwanzo kuuona umuhimu wa maamuzi hayo yaliyofanywa na uongozi za CUF na, hivyo, kuamua kuingia barabarani kuthibitisha uungaji mkono wa kufanya kila lililo ndani ya uwezo wao ambapo dhamira ya pamoja itaweza kutimia.
“Kuna ambao wanajiuliza kwa nini wanawake hawa hawa ambao wiki iliyopita kwenye viwanja hivi hivi walilia kwa uchungu na hasira pale Katibu Mkuu wao alipowafahamisha msimamo mpya wa Chama chao wa kumtambua Rais Amani Karume, na leo ndio hawa hawa ambao wanaandamana kumuunga mkono! Ndiyo, tulilia kwa mengi. Kumbukumbu za mateso na madhila, za unyanyasaji na dhuluma, za kupoteza na kudhalilishwa ndani ya nchi yetu wenyewe. Tulilia pia kwa upya wa habari yenyewe na wingi wa maswali ambayo kwa muda ule mchache hayakuwa na majibu. Tulilia tukijiuliza, hivi sasa Habibi Kipenzi Chetu, Maalim Seif Sharif Hamad, anatupeleka wapi mama zake, dada na shangazi zake, binti na wakwe zake?” aliuliza Naibu Katibu huyo.
Aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano huo kwamba wana jawabu kwa kila swali kupata jawabu na fakhari kuwa uongozi wa Chama ulikuwa wa mwanzo kuja hadharani kunyoosha mkono wa ushirikiano, umoja na mshikamano kwa ajili ya Zanzibar, Tanzania, Afrika Mashariki na dunia kwa ujumla.
“Tunaona fakhari kwamba sisi sasa ni sehemu ya kuibadilisha nchi hii, na kwa hilo hatuna la kujutia wala hatuna la kupoteza. Wanawake wa Zanzibar hatuna cha kupoteza zaidi ya minyororo ambayo nchi yetu ilikuwa imefungwa kwa zaidi ya miaka 50 sasa!” alisema.
Alisema wanawake ndio ambao wamekuwa wakibeba sehemu kubwa ya machungu yanayosababishwa na kufeli kwa mfumo wa siasa za Zanzibar kwa miaka yote hiyo 50. ambapo alisema sio kusudio lao kuwalaumu wanaume, ambao kwa miaka yote hiyo wamekuwa ndio vinara wa siasa zao.
“Lakini tunakusudia kusema kwamba sifa zetu za kuwa mama, dada, wazazi na walezi, ndizo zinazotufanya tuumie zaidi pale maafa yanayosababishwa na kufeli kwa siasa zetu yanapotokea” Alisema Naibu huyo.
Akikaribishwa katika mkutano huo na kuzungumza kwa ufupi, Katibu Mkuu wa Chama Cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alipokea salamu za wanawake hao na kusema kwamba yeye amewasamehe wale wote waliomzomea na kumpinga kwa kuwa awali wengi wao walikuwa hawajafahamu lengo na madhumuni ya tamko hilo la kumtambua Rais Karume.
“Mimi kwani nimechukia mlipokuwa mkinizomea mimi nilikuwa nacheka kwa kuwa najua hakuna hata mmoja wenu aliyekuwa ananichukia au ana nia mbaya nami na najua uchungu wa mzazi kwani kauli ile ilikuwa nzito kwani mnafikiri hata sisi tulipokutana ilikuwa ni jambo jepesi huko katika vikao vyetu? Ni jambo zito lakini niwahakikishie wale wanaosema Maalim Seif amechemsha nasema mimi bado injini yangu ipo makini na sijachemsha bado” alisema na kuungwa mkono na wanawake hao ambao awali walimpinga vikali.
Maalim Seif alisema wakati mwengine maamuzi mazito yana gharama zake kwa kuwa huku akitoa mfano wa mtoto mgonjwa “Kwani unapompa mtoto wako dawa lakini akawa hataki kunywa ile dawa si inakubidi uchukue uamuzi wa kumnywesha kwa nguvu jee utakuwa humpendi mtoto wako au ndio unataka anywe ile dawa ili apone kwa kuwa anaumwa” Alisema kwa ufupi Maalim Seif huku sauti zikisikika ‘tumekufahamu na tumekuelewa mwanzo tulikuwa hatujajua sasa tumejua.
Zahra alisema hivi sasa si wakati wa kukumbushana wapi na vipi yaliwapata lakini itoshe kunukulu msemo wa wenzetu Wanyarwanda, ambao baada ya kuangamizana kwenye mauaji ya kutisha ya miaka ya ’90, sasa wenyewe wameinuka na kusema ”NO MORE!” Basi tena! hivyo na wanzanzibari waseme kwa pamoja, NO MORE. Basi tena!
“Mheshimiwa Mgeni rasmi tunasema basi, basi tena! Basi tena kugawanywa na tugawanyika kwa misingi ya asili zetu. Basi tena kugombanishwa na tukagombana kwa misingi ya vyama vyetu. Basi tena kupiganishwa na tukapigana kutetea itikadi zetu. Basi tena kutishwa na tukaogopana kwa misingi ya visiwa vyetu. Basi tena kumpa nafasi mtu wa kando asimame baina yetu. Basi kwa kila jicho la adui na la hasidi dhidi ya nchi yetu. Basi tena kwa yote hayo, na mengine maovu zaidi ya hayo, dhidi ya nchi yetu” alisema huku akishangiriwa na wanawake.
Katika mkutano huo ambao misemo ya watu washuhuri ndio iliyotawala Zahra alisema “Sasa, tunachokitaka sisi wanawake wa Zanzibar ni nchi yetu tu. Zanzibar hii ambayo kwa miaka 50 sasa imekuwa ikichinjwa na kukatwa vipande vipande, tuna jukumu leo hii la kuikusanyakusanya na kuileta pamoja. Na tafauti wanavyosema watu kwamba La Kuvunda Halina Ubani, Zanzibar yetu haijavunda. Bado inawezekana kuiunda tena, ikasimama kuchukua nafasi yake iliyokuwa imeshikilia kwa karne kadhaa huko nyuma, yaani kitovu cha elimu, ustaarabu na maendeleo. Na kama alivyokuwa akinadi kampeni zake Barack Obama, ambaye hata babu yake Bwana Onyango Hussein Obama, alipitia Zanzibar na kufaidika na ustaarabu wa watu wa nchi hii, YES WE CAN! Ndiyo, na sisi Wazanzibari tunaweza, na lazima tuweze” aliwaeleza wanawake wenzake.
Zahra alisema “Kwa viongozi wote wa Zanzibar kutoka pande zote mbili kuu, tupelekee ujumbe wetu kwao kwamba Waingereza husema IT TAKES TWO TANGO, na Waswahili husema kuwa KIDOLE KIMOJA HAKIVUNJI CHAWA. Ikiwa kuna sehemu yoyote duniani ambayo imethibitisha misemo hii ya Wahenga, basi ni Zanzibar. Licha ya viongozi hao kuongoza siasa za nchi hii kwa miaka yote hiyo 50, kwa kuwa kila mmoja alisimama kivyake, basi ndiyo maana Zanzibar imekwama. Kwao ujumbe wetu ni wa wazi, nao ni kwamba HESHIMA YAO KAMA VIONGOZI ITATAFSIRIWA TU KWA KUJITOLEA KWAO KWA AJILI YA ZANZIBAR. Nasi tutawaheshimu kwa kuiheshimu kwao Zanzibar, Wazanzibari na Uzanzibari!” alisema.
“Kupitia hadhara hii ya leo pia, tunamuomba Katibu Mkuu wetu, Maalim Seif, atufikishie salamu zatu kwa Rais wa Zanzibar, Mhe. Amani Karume. Uongozi wa Chama chetu umetutaka tumtambue kama rais halali wa Zanzibar. Mwanzoni tuliupinga uongozi wetu si kwa kuwa tu hatukufahamu, lakini pia kwa sababu ya kutokuiamini dhamira ya Mhe. Karume na wenzake panapohusika khatima ya Zanzibar. Tumefahamishwa na sasa tunaelekea kufahamu na kwa hivyo, sisi wanawake wa Zanzibar tunamtambua Mhe. Karume kwamba ndiye Rais wetu. Kwamba yeye ndiye mwenye jukumu la kuikoa nchi hii. Lakini tungeomba ujumbe wetu kwake uwe mfupi na wa moja kwa moja, nao ni kwamba sisi mama, dada, binti na wakwe zako wa zanzibar tunakupa imani yetu, tafadhali usije ukaibwaga chini!” alimalizia Kiongozi huyo.
Wanawake hao walisema wenzao wa Tanzania Bara, katika wakati kama huu ambapo Wazanzibari wanatafuta njia za kuwaleta pamoja, wao ni ndugu ambao msaada wao unahitajika. Zanzibar iliyo pamoja na inayoshirikiana ina maslahi zaidi kuwa nayo kwenye Muungano kuliko Zanzibar iliyogawika. Zanzibar imara ni kwa Muungano imara na Zanzibar dhaifu ni kwa Muungano dhaifu. Kwa hivyo, watu wa Tanzania bara ni ndugu wa damu damu wawe ni sehemu ya utatuzi wa matatizo na wasiwe sehemu ya tatizo ambapo wamesema ujumbe weo kwao ni mfupi nao ni kwamba Udugu Ni Kufaana, Udugu Si Kufanana!
“Salamu zetu za mwisho, lakini za muhimu na za lazima ziende kwa Wazanzibari wote walio ndani na nje ya nchi. Tunakuomba Mgeni Rasmi pamoja na viongozi wenzako wote, popote mutakapokutana nao, muwape ujumbe wa wanawake wa Zanzibar kwamba milango ya nchi yao inafunguka. Ombi letu kwao ni kuwa tushirikiane ili kuhakikisha kuwa hivyo vinavyoingia ndani wakati milango hii ikifunguka, ndivyo vile vyenye kheri kwa nchi yetu. Kwa pamoja tuwe mawakala wa kuibadilisha Zanzibar na sio mawakala wa kuibakisha Zanzibar hapa ilipo au kuirudisha nyuma zaidi. TUSHIRIKIANE KUIJENGA ZANZIBAR MPYA” alisema Zahra katika mkutano huo amabo ulitanguliwa na maandamano makubwa ya wanawake.
“Kwa Mwenyekiti wa Chama chetu, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, tuna wingi wa shukrani na heshima ya hali ya juu. Ni unahodha wake imara kwa Chombo chetu ndio ambao umetuwezesha kuvuuka dhoruba na mawimbi ya kutisha katika safari yetu. Prof. Lipumba amekuwa akithibitisha uprofesa wake na kila mmoja wetu ni shahidi ya vile anavyolitimiza jukumu lake la kuwa kiongozi kwetu. Tunampongeza sana kwa kulisimamia hili hasa la kuwaona ndugu zake Wazanzibari wanakuwa kitu kimoja na kwa kujitolea kwake daima kwa ajili ya Chama na nchi yetu. Ushindi wa karibuni katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa huko Tanzania Bara usingelipatikana ikiwa si uimara wa uongozi wake” alimsifu Mwneyekiti wao.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wao walisema “Kwa Katibu Mkuu wa Chama chetu, Kipenzi chetu, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye Chama kilikupa jukumu zito la kuja hadharani kutangaza msimamo mpya kwa maslahi ya nchi yetu, tunakwambia kwamba sisi wanawake wa Zanzibar tuko pamoja nawe. Tuko pamoja na uongozi wa Chama chetu katika kuizamua Zanzibar kutoka miaka 50 ya siasa za mgawanyiko ambazo hazijawahi kuwa na faida kwa yeyote kati yetu” alisema Zahra ambaye pia ni mwakilishi wa viti maalumu vya wanawake.
Makamu Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo aliwaambia wanawake hao kwamba wasiwe na wasi wasi na kiongozi wao kwani Maalim Seif ameahidi kuwatumikia wazanzibari zaidi ya miaka 20 iliyopita hivyo sio rahisi kuwageuka au kuwasaliti kama wengi wanavyodhania.
“Msiwe na khofu na Maalim Seif nyinyi hamumjui lakini sisi tunayemjua hatupati tabu ngoja nikwambieni kwamba Maalim Seif aliahidi tokea miaka hiyo akiwa anafanya kazi katika ofisi ya waziri kiongozi alisema atawatetea wazanzibari akiwa ndani ya serikali au nje ya serikali akiwa ndani ya chama au nje ya chama na wakati huo alikuwa CCM na sisi sote tulikuwa ni CCM na pia aliwaahidi wazanzibari kuwa atawatetea kwa njia yoyote akiwa ndani ya Zanzibar au nje ya Zanzibar kwa hivyo huyo ndio Maalim Seif hawezi hata siku moja kuwasaliti wazanzibari ahadi yake bado hajaitumiza kwa nini tena awasaliti? Alihoji Makamu huyo huku akishangiriwa na mashabiki wa chama hicho.

SOURCE:ZANZIBAR YETU WEB BLOG

n.b, Msisitizo ni wangu
 
Asalamu alaykum.

Swali hilo wanajiuliza wengi why leo na isiwe tokea miaka hiyo ya nyuma ambapo takriban miaka minne CUF wametoa msimamo wa kutomtambua Rais Karume lakini kama walivyosema wenyewe CUF kwamba wametafuta nafasi hiyo kwa miaka mingi ili wapate fursa ya kuzungumza na Rais lakini hali ilikuwa hairuhusu lakini sasa hali imeruhusu jamaa amekwua katika good will ndio CUF wamepata chance ya kwenda na ndipo hapo hapo wakaingia Ikulu.

Na kama alivyosema Nwalimu Nyerere kila kitu kina wakati wake na hili muamini kwamba wakati wake umefika huko nyuma si unajua kiburi cha urais, upya na mambo mengine kama hayo mimi ndio rais mimi ndio kiongozi wa nchi mimi... mimi.... kama mjuavyo madaraka matamu.

mimi wala swali hilo silioni kubwa sana kilicho kikubwa kangu ni kwamba kwa nini Kikwete aliwaahidi watanzania kwamba suala hilo atalimaliza then kaingia mitini wakati aliliahidi bunge na kama ujuavyo kule bungeni kuna utaratibu wa kuandikwa kila kinachosemwa na huyu jamaa aliahidi kwa khweli mimi sijui sheria lakini suala hili huwa najiuliza nadhani ningekuwa mbunge ningeuliza hii ahadi imefikia wapi maana alipokwenda ulaya nilimsikia akizungumza na wazungu kwamba hawezi kuwa dikteta katika kuingilia suala la zanzibar haaaa mimi nilishangaa sana ikiwa kiongozi unakwepwaje kuwa dikteta for some how? maana kama kiongozi lazima ujue nini unafanya na baadhi ya maamuzi lazima utatolee mamuzi ya kidekteta as special katika nchi zetu hizi za kiafrika maana tusidanganyane hatuna utaratibu wa kufuata demokrasia kihivyo.

ciao
 
Haki sawa kwa wote,asiyependa haki,abaki CCM kwenye mafisadi
 
I feel sorry 4 my people.hakuna hata moja la kusheherekea katika mamuzi yaliyofanywa na Maali seif na wenziwe zaidi ya tutakuja kujuta kila siku zikikaribia huko usoni kwani tumekuwa tunarudia yale kwa yale . (majuto mjukuu)
 
Unajua wakati chama cha cuf kinaanziwshwa wengi walisema wanayoweza kusema waliandika wanachoweza kuandika...kuna mambo mazuri yametokea 2009/nov na itakumbukwa daima ila kuna mambo mabaya ya mauwaji yalitkea kule zanzibar kwa kutokubali serikali ya karume...na kufikia watu 28 kufariki tena wengine kwa bastola live....
VIongozi mnatueeleza nini sisi ndugu wa marehemu kama mlikuwa na uwezo wa kukubali toka mapema hamwoni mngesaidia kuokuwepo kwa haya mauwaji ya jan 28???embu vyama vya upinzani mkiwa mnaamua mambo yenu msiamue kishabiki angalieni madhara yake...leo hii watu wengi walilala ndani vikongwe kwa vikongwe kule pemba...hamwoni dhambi zote hizi mtazibeba ninyi......,??tuwe makini na maamuzi yetu ........ni jambo jema lililofanyika lakini kwa nini mpaka watu wafe????????
 
Back
Top Bottom