Matokeo ya Maalim Seif Kumtambua Karume

Matokeo ya Maalim Seif Kumtambua Karume

Ninaungana na Wapenda Amani wote wanaoliona tukio hili kuwa ni chanzo cha amani Zanzibar na Tanzania kwa jumla, lakini kama Watanzania wengine, na mimi nina wasiwasi na makubaliano yenyewe. Kwa nini Karume na Seif au tusema viongozi wa CCM na CUF wasiweke mambo hadharani ili wananchi tujue kinachoendelea.
Mnakumbuka kuwa Salmin na Seif walikutana Ikulu na kuzungumza "SIRI" ambayo daima hatukuambiwa?
Binafsi siamin chochote mpaka nione matokeo, kwani kama Watanzania wengi, nimechoshwa na "Miafaka" ya "Kutoafikiana". Ninaitakia mema Zanzibar na Tanzania kwa jumla, lakini ninaliona hili kama sehemu tu ya Mchezo wa Kuigiza ambao tumekuwa tukiushuhudia miaka nenda miaka rudi. 2010 haiko mbali,tusubiri tuone watatufikisha wapi. Ninamuomba Mungu iwe nimekosea.
 
Mkandara,
Kwani katika kitabu cha Jumbe analilia Zanzbar kujitenga au anachohoji makubaliano sahihi ya muundo wa muungano?
Huku ukikumbuka kuwa wakati Muungano ukiasisiwa Jumbe alikuwa ndo mshauri nambari moja wa Mzee Karume, hivyo anaujuwa muungano kuliko mimi na wewe...na aliamua kuandika kitabu hicho baada ya Nyerere kumkashifu na kum paint kama msaliti wa Zanzibar...hoja ya Jumbe katika kitabu hicho,ambacho hata watoto wa shule za msingi wanakisoma(kwa tafsiri ya kiswahili na Ali Saleh "Alberto"),ni kuwa Muundo wa muungano uliokusudiwa haukuwa wa serikali mbili bali ni serikali tatu na hii si kuvunja muungano bali ni kuwa na muundo muafaka kwa pande zote. Kama ukioana wazanzibar wanalia basi hawalii kuvunja muungano, kitu ambacho ni ujinga kufikiria,bali wanalia kuwa na muundo bora wa muungano wenye manufaa kwa pande zote...na hili,kama Jumbe alivyosema, ni suala la kukaa kukubaliana lakini Mwalimu alikukuwa mbishi kwa kuwa alikuwa ana dhamira chafu ya kuimeza na kuifuta Zanzibar kama taifa huru.Pili, Jumbe ameonyesha mpaka mapungufu ya katiba ya Tanzania ambayo imeundwa ktika mfumo uleule wa katiba ya TANU,ambayo anasema wazi kuwa ndo inayochangia matatizo makubwa,yanayoitwa kero za muungano,ambazo hazitakwisha kama katiba hiyo haijaandikwa upya...na kwa kuthibitisha kuwa Jumbe hakuwa akipayukwa, hata leo utaona kilio cha vyama vya upinzani vikitaka katiba mpya...kwa kuwa hii ya sasa ipo kimfumo wa chama kimoja(Tanu sasa CCM).

N.b,
book tittled: Partner-ship
 
Mkuu Babylon,
Usijali utaelewa tu...kidogo kidogo...lakini kumbuka mkataa wengi mchawi.
 
Pdidy,
Tunaweza kusamehe lakini hatutasahau.
Kama Mungu tumkoseavyo kila siku na tukirudi kwake anatusamehe na riziki zake anatupa...kwanini isiwe hivyo kwa wanaadamu...wakati kusameheana kunaleta umoja,mshikamano....visasi vinasogeza shari na mapigano kila siku yote ya nini hayo?
 
Asalamu alaykum.

bwana game theory sikubaliani na wewe kwamba wote hawautaki muungano na hilo ndio tatizo kubwa la watu wa bara wanadhani kwamba wazanzibari wote hawautaki muungano na hilo linafikiriwi la upande wa zanzibar mjue kuwa hata upande wa bara hawautaki muungano na nakumbuka siku ya mwisho ya kifo cha marehemu professa haroub othman katika uzinduzi wa kitabu uliofanyika zanzibar dkt salim ahmed salim alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi ule na alisema suala hilo kuwa wazanzibari wanaonekana kuwa hawataki muungano lakini asilimia kubwa ya watu wanaosema hatutaki muungano ni watu kutoka bara maana wao ndio wanaosema kwamba tumechoka na malalamiko ya wazanzibari, wazanzibari wao madai yao sio kuukataa muungano wao wanachotaka na ndio kilio chao cha siku zote kuwa wanataka usawa.

na kilio chao ni kuwa yale mambo 11 ambayo ndio original ya article of union ndio yafuatwe na hayo yalioingizwa kinyemela yatolewe hilo ndio dai kubwa la wazanzibari lakini tatizo wengine wanapindisha maneno kwa makusudi kwa kisingizio cha kusema wazanzibari hawataki muungano no hawakatai wana madai ya msingi na ndio hayo yashughulikiwe hebu kupigwe kura ya maoni muone ni akina nani waliokuwa haataki muungano, lakini kwa kuwa madai huwa hayashughulikiwi ndio inakuja ile dhana ambayo watu wengi huitumia.

mimi nitatoa mfano mdogo tu wa kifamilia 'ikiwa mtu ana mume au mke katika nyumba yake kila siku makelele na ana madai ya msingi au haki zake za msingi ambazo hatekelezewi ndani ya nyumba na huku fursa ya kudai kuondoka pale anayo atasemaje atakaa anyanyasike au atadai talaka aondoke na akatafute mwengine? Hivyo si mnaona hata kwa wakiristo ambao hawana kitu talaka siku hizi wanapeana talaka wanapochokana itakuwa kwa wenye haki ya kupeana? kwa kuwa amedai amechoka hasikilizwe wala hatekelezewi inabidi achukue uamuzi wa kujikwamua katika madhila hayo badi na hilo kwa wazazibari ndio hayo hayo huwa wanasema bora jahazi lipasuke tugawane mbao.

Kuhusu mazungumzo ya Rais Karume na Maalim Seif kila mpenda amani bila ya kujali itikadi za kisiasa au ushabiki atafurahia suala hilo na khasa katika kipindi hiki kigumu ambacho kinaelekea uchaguzi mkuu wa 2010. kama mjuavyo mazingira ya uchaguzi zanzibar ni mabaya sana.

mimi kwa mtazamo wangu sikubaliani na suala la serikali ya mseto kwa kuwa naamini ni kuviza demokrasia ninachotaka mimi aliyeshinda apewe ushindi wake na aunde serikali ya kushirikisha jamii yote lakini sio uibe then utake kuunda serikali baada ya migogoro kama inavyofanyika kwa afrika hivi sasa huko ni kuendeleza wizi, kuviza demokrasia na kukiuka misingi ya haki za binaadamu na utawala bora. lakini katika hili la zanzibar kumtambua karume nasema hata kama kesho ndio uchaguzi leo cuf ndio wanataka kumtambua rais basi nakubaliana nao kwa kutokana na hali halisi ilivyo.

sio mchezo msifanye masikhara pahala pakiwa na migogoro ni hatari na hatari yake sio ya siku moja au mbili na mjue kuchochea cheche za moto ni very simple lakini kuuzima huo moto wake au cheche zake ni very hard.

na burundi, ruwanda na sehemu nyengine zenye migogoro hazikuanza moja kwa moja au hazikuumbwa ziwe hivyo zilianza taratibu na kama mchezo tu lakini moto ulipowaka ni kiasi gani zimetumika kugharamia kurejesha amani? hebu tujiulizeni swali hilo, lakini jengine hwa jamaa hawajakutanishwa na mtu wamekutana wenyewe baada ya kuona wamewachokesha wazanzibari kwa hivyo sisi tuwape moyo wakubaliane vyema na sio kuwavunja moyo

mpaka hapa panatosha
 
Junius,
Unapokataa mimba ulotungwa ni sawa na kukataa mtoto aliyezaliwa. Hayo yaliyofuata baada ya kumlea mwana huyo huyo, (muungano) ni maswali ambayo nyie mlitakiwa kumuuliza Jumbe.
 
- Pdid Mkwawa akirudi leo wale wabongo tuliooa wazungu tutanmwambia nini? Mwalimu akirudi leo tunamwambia nini na huu ufisadi,

- Hizo ndizo politics na politicians, lazima uwe mnafiki na hakuna permanent truth, wala permanent friends ukiingia kichwa kichwa shauri yako!


Es!
 
Maalim Seif aliahidi tokea miaka hiyo akiwa anafanya kazi katika ofisi ya waziri kiongozi alisema atawatetea wazanzibari akiwa ndani ya serikali au nje ya serikali akiwa ndani ya chama au nje ya chama na wakati huo alikuwa CCM na sisi sote tulikuwa ni CCM na pia aliwaahidi wazanzibari kuwa atawatetea kwa njia yoyote akiwa ndani ya Zanzibar au nje ya Zanzibar kwa hivyo huyo ndio Maalim Seif hawezi hata siku moja kuwasaliti wazanzibari ahadi yake bado hajaitumiza kwa nini tena awasaliti? Alihoji Makamu huyo huku akishangiriwa na mashabiki wa chama hicho.
Alipokuwa CCM aliwatetea kwa yapi vile?..hivi kweli matatizo ya Wazanzibar yameanza toka Maalim Seif aondoke CCM au!
 
Pdidy,
Tunaweza kusamehe lakini hatutasahau.
Kama Mungu tumkoseavyo kila siku na tukirudi kwake anatusamehe na riziki zake anatupa...kwanini isiwe hivyo kwa wanaadamu...wakati kusameheana kunaleta umoja,mshikamano....visasi vinasogeza shari na mapigano kila siku yote ya nini hayo?

mkuu ni kweli kabisa ndio maana nimemmpongeza kwa uamuzi wake ila nikasema vyema tufikirie mara mbili..unajua mkuu yawezekana watu walikuwa na malengo yao....ni wazo tu..ndio maana nkatoa angalizo isitokee kwa vyama vingine mkuu......hicho alichofanya november kinamtosha kumsamehe mkuu.......ila tuwe makini mkulu
 
Mkandara,
Kumuuliza Jumbe ni misjoinder of the events...Jumbe katoa maoni yake tu, yeye si katiba,si chama wala si mtawala...tutaihoji katiba,mkataba wa muungano,watawala na chama chao...labda nikufahamishe tu,Msaidizi wa Jumbe wakati ule, Mh. Ramadhani Haji Faki,ambaye alikuwa waziri kiongozi, anayomengi ambayo hayajasemwa...na hwenda yakaibuka karibuni tu na watu watajuwa mbivu na mbichi ya Muungano(watu hawaogopi tena sasa)...habari nilizozipata za "nyumba kubwa" zanzibar zimenistua kidogo,nilipozikia nikakumbuka maneno ya Bhoke Munanka...aliwahi kusema"...huu muungano una siri na mambo mengi ambayo watu hawayajuwi na hayasemwi...tuulizeni sisi tulioasisi kabla hatujaondoka..." si muda mrefu baada ya kusema maneno yale mzee yule aliaga dunia...kwa hiyo mengi hatuyajuwi...na hatuwezi sema kuwa Jumbe kaandika kila kitu.
 
Hii ni dalili nzuri kwamba wadau wa siasa za Zanzibar hasa wanachama wa CUF wameshamwelewa Maalim Seif. Shime dumisheni Amani na mshikamano Zanzibar tukizingatia kauli mbiu: TUPINGANE BILA KUPIGANA!!!
 
na wale tuliopoteza ndugu zetu katika vita ya Kagera tuliyopigana kiushabiki tu kwani nyerere alitueleza nini?? nothing na maisha yakaendelea mpaka leo
 
- pdid mkwawa akirudi leo wale wabongo tuliooa wazungu tutanmwambia nini? Mwalimu akirudi leo tunamwambia nini na huu ufisadi,

- hizo ndizo politics na politicians, lazima uwe mnafiki na hakuna permanent truth, wala permanent friends ukiingia kichwa kichwa shauri yako!


es!


mkuu fmes
salute
 
Ni kweli wakuu tuombe mungu usiwe ule unafiki wakina shangirwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaiiiiiiiiiiiiiii zimbabwe
 
Alipokuwa CCM aliwatetea kwa yapi vile?..hivi kweli matatizo ya Wazanzibar yameanza toka Maalim Seif aondoke CCM au!
Mkandara, Matatizo ya Zanzbar yameanza tarehe 12 Januari 1964 na yakapamba moto zaidi kuanzia tarehe 26 April 1964...mpka leo hatutambuwani.
 
Cha muhimu sana katika hili ni kuwapa moyo kama wenyewe walivyosema wamepigana vya kutosha, wametengana vya kutosha, wameumizana vya kutosha sasa wameamua kusema basi na iwe basi sisi ni kuwaombea Mungu hapo walipofika waendelee zaidi kuwa wamoja na kuinusuru nchi.

suala la watu waliouawa mbona hao waliouawa na waliouwa au waliochangia kuuwa ni wengi kwa tanzania hii lakini maisha yanakwenda watu lazima wafike pahala wasameheane, hata zanzibar mamia ya watu waliuliwa wakati wa mapinduzi lakini hao hao wauaji wamekwend akuposa kwa familia zilizouliwa familia zao na wamepewa wake na hadi leo wapo nao hiyo ndio life bila kusameheana hakuna life kutakuwa na vurugu maana kutawekwa visasi amabvyo matokeo yake ni mabaya kwa kuwa yatazalisha chuki, ufisadi, hasama na mwisho kulipizama visasi kwa kuuwana au kudhuriana.

tuseme basi na tujenge nchi hivi sasa nasisitiza bado kwamba tuwape muda hawana viongozi watusaidie katika kujenge nchi

usiku mwema
 
Mkandara, Matatizo ya Zanzbar yameanza tarehe 12 Januari 1964 na yakapamba moto zaidi kuanzia tarehe 26 April 1964...mpka leo hatutambuwani.
Haswaaa sasa hizi imani ya sifa za kumpa huyu Maalim Seif zinatoka wapi? Binafsi kama ningekuwa Mzanzibar ningerudisha chama cha UMMA Party chama ambacho kilifanya Mapinduzi na yakadumu kwa mwezi mmoja tu kbala wavamizi hawanyakua tonge mdomoni. Ndicho chama kilichokuwa kati ya Hizbu na Afro Shiraz na walikuwa na nia njema kwa Zanzibar yote..kinyume cha hapo ni kupotosha ukweli.
Nyuma ya hapo mkuu wangu unataka kuturudisha kwa Sultan, utawala wa kina Ian Smith na kina Botha kwani hata Zimbabwe matatizo ya wazungu walianza siku ZANU PF walipopindua nchi hiyo
 
Back
Top Bottom