Matokeo ya Maalim Seif Kumtambua Karume

For more details
the guardian tomorrow 16nov 2009
 
kama haya makubaliano yatafanikiwa na ndivyo tunavyoomba basi wale walouwawa watabaki kuwa mashujaa katika historia ya zanzibar na tunawaombea mola awalaze pema peponi. nadhani ni vyema tusiangalie waliouwawa kabla ,tuangalie watakufa wangapi zaidi kama hatujayapatia baraka haya makubaliano?.
Mungu atuepushe mbali ,kama hayajafanikiwa haya makubaliano basi zanzibar itakuwa katika hali mbaya zaidi kiupinzani (namuomba mola asitufikishe huko na naomba ayabariki makubaliano haya yawe ndio chanzo cha maelewano zanzibar. amen)
 
hii habari niliisikia tangu jana. kaeni mkao wa kula. kuna nyengine nzito ipo njiani
 
Msamaha


Hakuna alokamilika, sote tuna mapungufu,
Hutokea kengeuka, kwani si wakamilifu,
Binadamu hupotoka, huonesha udhaifu,
Pale unapokosea, basi omba msamaha.

Usiogope kukosa, sote tumeumbwa hivyo,
Ni mtego tunanasa, vile tufikiriavyo,
Ama tukajenga visa, mengi t'watendeavyo,
Pale unapokosea, basi omba msamaha.

Wala sione aibu, kuuomba msamaha,
Mwenye kukosa hutubu, wala si kukosa raha,
Neno zuri ndo wajibu, kwa kuitunza staha,
Pale unapokosea, basi omba msamaha.

Samahani neno zuri, kwa wanaotuzunguka,
Tukosapo tukikiri, tunazidi heshimika,
Huo ndiyo ujasiri, tena usio na shaka,
Pale unapokosea, basi omba msamaha.

Haifai ujeuri, haifai endekeza,
Ijenge yako nadhari, watu itawapendeza,
Wala siyo jambo zuri, wenzako ukawakwaza,
Pale unapokosea, basi omba msamaha.

Makosa hurekebisha, zile tofauti zetu,
Msamaha huboresha, tuishivyo na wenzetu,
Upendo huimarisha, udugu kati ya watu,
Pale unapokosea, basi omba msamaha.

Hakuna aliye mwema, kwa asilimia mia,
Wenzetu wakitusema, haipaswi kuwanunia,
Makosa yanatupima, uwezo kuvumilia,
PALE UNAPOKOSEA, BASI OMBA MSAMAHA.


Posted by P2THED:57 PM
 

CUF kama mngekuwa na maneno matamu hivi mngeepusha mambo mengi sana! Anyway, tusahau yaliyopita maana hayajengi!
 
hii kushirikiana pia imekuwa ulaji. akili zetu waafrika ziko kinegative negative tu. si subirini mpaka yatokee ndo mseme.
 
Rais wa zanzibar mh dk abeid aman karume ameagiza chama cha cuf kuchagua watu wawili kuingia baraza la wawakilishi.......hiko mi kionjo tu jamani ktk guardian la kesho si mnajua mkipew yote hamnunui...
 
Kwa maoni yangu huu ni usanii kuelekea 2010 na baada ya uchaguzi wa 2010 na CCM kufanya tena vitu vyao kama walivyofanya 1995, 2000 na 2005 CUF watapigwa tena mueleka mzito huku wakibaki wanalialia kwamba CCM imeiba kura na uchaguzi haukuwa halali. Hawa CUF ni rahisi kweli kudanganywa! Karume kwa nini hakulifanya hili tangu 2006!? Tusubiri tuone labda kutakuwa na "muafaka" wa kweli na wa kudumu.
 
Mi swali langu nauliza hizi nafasi mbili alikuwa kazishikilia "dk karume" ama "dk j m kikwete"" yawezekana zilikuwa vyumbani vyao
 
Mi swali langu nauliza hizi nafasi mbili alikuwa kazishikilia "dk karume" ama "dk j m kikwete"" yawezekana zilikuwa vyumbani vyao

Na ni kwanini ni nafasi mbili tu siyo 6 au nane?
 
cuf kama mngekuwa na maneno matamu hivi mngeepusha mambo mengi sana! Anyway, tusahau yaliyopita maana hayajengi!


baba ushaona juu msamaha msamaha wamekubali kutorudia tuwape muda.....labda kwa breakin nyuziiiiiiiiiiii

rais karume leo amewataka cuf kuchagua watuu wawili yaani 2 kuingia baraza la wawakilishi/....kumekucha yapo mengi ...mlichelewa tu kusoma nyakati unajua huu usemi if u cant'm join'm very nice..hongereni ila poleni kwa kuchelewa
 
Sijamwona Karume akihudhuria vikao na sherehe nyingi za Muungano,

- Mkuu hivi kwa nini hamuwaonei huruma viongozi wetu, unataka Karume akakae chini na hawa viongozi wetu useless! Hata mimi ningefanya kama Karume!

Respect.


FMEs!
 
Hiyo katiba imebadilishwa lini - rejea msimamo wa CCM mwanzoni mwa mwaka. CUF kwa ulafi wao wameamua kuingia mtegoni kichwa kichwa - takrima kwa kuweka silaha chini. Nilisema makubwa yanakuja na hizi ni rasha rasha tu, subirini ! CCM kiboko !

.
Swali: mtego au zilipangwa ?
 
- Mkuu hivi kwa nini hamuwaonei huruma viongozi wetu, unataka Karume akakae chini na hawa viongozi wetu useless! Hata mimi ningefanya kama Karume!

Respect.

FMEs!

Field Marshall ES, are you Serious?
Does Karume really has any leadership integrity/status worth comparing with anybody in the URT Government?
....Kuna watu/viongozi (Tanzania) zamani, walikuwa wakiitwa makatibu kata.......
 
mwinyi sio mzanzibar hilo ulijue na itakuwa vigumu sana yeye kuwa rais kwani hana sapota yoyote kule na ujue huyu mwinyi baba yake ameshakuwa rais hii haitoonyesha pic nzuri
 
nadhani wengi wanajua hali ya muelekeo wa znz kwa sasa tanganyika wanataka kuifuta znz isiwepo na ndio maana sasa wazenji wameshashtukia hilo na ndio maana wameamua kushikamana ili kuinusuru kwani hakuna njia nyengine ila kuwa na umoja hapo bara ndio wanabaki hawajui nini wagfanye
 
Tonga, Hiyo Tanganyika ndio nchi gani? natazama ramani siioni kitu isipokuwa naona Zanzibar hapa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…