Matokeo ya Maalim Seif Kumtambua Karume

Ukitaka kuujua ungangari wetu weka jina lako halisi halafu tutukane utajua kama bado ni ngangari ama nini.
Kwani nyie Ngangari kweli? Mtu wa kwanza kutumia hiyo "simu" ni Marehemu Mzee Mloo (Yule wa Kikwajuni) Jee wewe unamuelewa huyo?
 
Junius unaposema "makubaliano ni ya Wazanzibari wote" una maana ilipitishwa kura ya maoni au hilo neno "wote" linamaanisha nini? Na kama kweli makubaliano ni ya Wazanzibari wote mbona Hamad alizomewa na wana-CUF wakati akitangaza uamuzi wa kumtambua Karume? Labda ungesema uamuzi ni wa Wazenj "wengi" ningekuelewa! Hongereni Wazenj kwa kuanzisha Chama kipya: CCUF "kwa maslahi yenu!"
 
CUF kumtambua Karume ni moja, kubwa ni Maalim sasa amalizane na Karume kumaliza game la mgogoro wa vitambulisho vya ukaazi, na kuwasisitiza wafuasi wake wakajiandikishe daftarini, vinginevyo, nimeongea na watu wa kawaida hapa mitaani Pemba, CUF ni watu wa msimamo, wako tayari kwa lolote mpaka kieleweke. Juzi walijitokeza kwa wingi, leo wamegoma tena wasubiri kauli ya Seif kujiandikisha ila wametulia kimya, hakuna vurugu yoyote, ni amani na utulivu kwa kwenda mbele. Ila kimya chao na hiki kisuso, kina mshindo mkuu.
 
Kwa kuweka kumbukumbu sawa, awali nimetumia neno "...zanzibaris themselves..." na baadaye nikatumia neno "...wazanzibari wenyewe...",kwa maana hiyo hiyo, hilo neno "wote",umelileta wewe kutaka kunilisha maneno au kupotosha maana niliyokusudia,tusema kama ningesema 'wazanzibari wote' kama unavyotaka wewe,basi nisingekuwa nimekosea,hata hivyo, kwa kuwa the move imeanzishwa na kiongozi,upande mmoja(Maalim Seif) anayewakilisha kundi lenye ufuasi mkubwa kabisa wa siasa Zanzibar yaani CUF, na upande wa pili, ni Karume(rais)ambaye ni kiongozi wa Wazanzibari wote....na lengo ni kuendeleza maslahi ya wazanzibar...sasa utegemee Mzanzibari gani hapendi maendeleo?
Ni kweli kabisa, awali wanachama wa CUF,Unguja,hawakuelewa hatua hii ya ghalfa,jambo ambalo ni la kawaida katika wakati wa mabadiliko,popote pale,lakini siku ya pili, mkutano ulifanyika Pemba na wanachi wameunga mkono na hakukuwa na rabsha zozote na siku ya tatu,Maalim akatembelea mashina na matawi ya chama Unguja na mikutano kufanyika katika matawi mengine na viongozi wa chama kuwaelewesha kwa utaratibu wanachama na wapenzi ambao walielewa na kukubaliana na msimamo wa chama. Hata wale ambao siku ile ya mkutano walikuwa na jazba,walikubali ana walimpongeza Maalim na chama cha CUF,baada ya kuelewa vizuri nini kilikuwa kinaendelea.
 

Kweli CUF wana msimamo! Leo: "Hatumtambui Karume kama Rais!" Baada ya miaka minne: "Karume ni Rais halali wa Zanzibar!" Kaazi kweli kweli!
 

Sorry, nimepitiwa kuingiza neno "wote"! Ni maslahi ya Zanzibar yaliyopo kwenye Muungano (km vile mafuta hewa) ndio mnayoyatetea au yapi?
 
Jamani nashindwa kuelewa kabisa hapa. Ningeomba kiongozi wa CUF anifahamishe vizuri..
Hivi vurugu zote za Zanzibar zilitokana na CUF kutomtambua Karume?.. na ilikuwaje vurugu za mwaka 2000 na hata 2005 zilikuwepo hata kabla CUF haijatangaza kupinga matokeo ya uchaguzi.. Hii habari ya vurugu hadi Sief kukutana na Karume inahusiana vipi na kumtambua Karume yaani sielewi kabisa!

Jamani kuweni wakweli wambieni wananchi wananchama wa chama chenu ukweli kwani wanapofahamu sababu hujirudi ktk kutazama makosa yaliyotangulia hata wao kufiikia kutomtambua rais wao.. Binafsi naamini kabisa kwamba maamuzi ya Seif kukutana na Karume na hata kutambua Urais wake ni swala ambalo limepitishwa na kamati kuu ya chama pasipo kuwafahamisha wananchi wanachama nini sababu za kufikia hatua hiyo. Na why always ni kitu kinachomhusu Maalim Seif ndio kiwe kipaumbele zaidi, hicho kiti cha rais wa Zanzibar yeye ndiye alikuwa mgombea, basi chama kizima kiadhibiwe!

Haya uchaguzi unakaribia, ni ahadi gani ambazo Mh. Karume amewahakikishia CUF kwamba maisha ya wana CUF hayatakuwa hatarini ikiwa CUF itamtambua yeye kuwa ni rais wa Zanzibar..Na isipotokea je, kama walivyoahidiwa Muafaka.. ndio itakuwaje?
 
Haya uchaguzi unakaribia, ni ahadi gani ambazo Mh. Karume amewahakikishia CUF kwamba maisha ya wana CUF hayatakuwa hatarini ikiwa CUF itamtambua yeye kuwa ni rais wa Zanzibar..Na isipotokea je, kama walivyoahidiwa Muafaka.. ndio itakuwaje?
Mazungumzo yao yalichukua saa mbili, ndani ya closed doors, wao wawili tu! Hii ina maana yaliyozungumzwa wanayajua wao wenyewe! Si ajabu hadi leo hii Waziri Kiongozi nae yupo gizani kama watu wengine!
 
CUF ni chama cha wananchi ,jiandae kuwa na rais Professor wa kwanza Tanzania.
 
CUF ni chama cha wananchi ,jiandae kuwa na rais Professor wa kwanza Tanzania.
Kuwa na wishes ni kitu kimoja kufanikisha wishes ni kitu kingine..ndugu hata mrema alitaka kuwa rais lakini siku hazigandi..kuna mkakati gani zaidi ya kumsikiliza Maalim seif alone???
 
Jamani naombeni kuuliza jungu kuu halimalizi ukoko habari zisizoaminika zinadai Maalim Seif yuko mbioni kujiunga na CCM! na wana CCM wako mbioni kumpa ama urais Zanzibar ama umakamu urais Jamhuri. Naomba nipate ukweli wa habari hii! Sitaki matusi jamani maana lisemwalo lipo!
 
Wikiendi inaanza tena.
Mkuu inaonesha unaanza kuota...
Maalim Seif alikuwa miongoni mwa waanzilishi na waasisi wa CCM Zanzibar...anaijuwa CCM kuliko hata Jakaya Kikwete..anajuwa nje ndani ya CCM...ndiyo Maana alikubali jeuri ya Mwalim Nyerere kuwa "bora uwe mpinzani nje ya CCM kuliko ndani yake..." na Maalim akachkuwa ustaarabu wake...unajuwa alipokelewa vipi na Wazanzibari...kwa kishindo kikubwa hakijawahi kutokea,mpaka mshairi mmoja maarufu visiwani akamtungia shairi lililoimbwa na Naad Ikhwan Safaa(Malindi musical club),akatunga na watu wakaimba:
Mtajirusha wenyewe, roho na akili zenu
Kisemeni msizuwe, kilichomtoa kwenu
Na huku kaja mwenyewe, kajuwa hamna lenu
Ya bure yenu mayowe, huyu sasa siye wenu.
Chorus:Mtajirusha wenyewe roho na akili zenu na msema msizuwe kilicho mtoa kwenu.

Sasa Maalim arudi CCM akatafute nini...wazanzibar hawajasahu ahadi yake ya mwaka 1989 katika uwanja wa Tibirizi,Pemba...alisema "...nitakuwa pamoja nanyi hadi mwisho wa maisha yangu na sitawasaliti..."
Na mwenyewe Maalim heshi kutukumbusha ahadi hiyo mara kwa mara...akionyesha kuwa ni mtekelezaji wa ahadi zake na si mnafiki...ipo siku yatatimia kama si leo kesho
Endelea kuota.
 

upepo unapovumia ustadhi si huko unapotaka wewe watch this space for a soon to be a breaking news! yule Maalim kwa taarifa yako ni shushushu na aliwekwa kule kuwapumbaza Wazanzibari! sasa uamuzi umetolewa wa yeye kurudi rasmi alipotokea we subiri utaona na kuniambia humu ndani
 
Maalim akirudi CCM ni kama mtu anarudi kwao vile!
 
Labda nikupe kwa ufupi...Maalim Seif ni Mpinzani wa CCM kabla ya mfumo wa vyama vingi...hapo ndo sikuelewi unachoongea.
 
Serikali mseto Z'bar yanukia

Mwandishi Wetu​
Novemba 11, 2009

MAPATANO ya ghafla kati ya Rais wa Zanzibar, Aman Abeid Karume na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, yakihusisha kumtambua rasmi Karume, na Hamad kudai hatua hiyo inafungua makubwa zaidi, ni hatua za awali kuandaa serikali ya mseto, Raia Mwema imeelezwa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka vyama vya CCM na CUF, serikali ya mseto itaundwa ikiwa ni moja ya mkakati wa vyombo vya usalama kujipatia fursa ya kubaini kasoro na namna ya kuzifanyia kazi kwa kipindi hiki cha miezi kadhaa kabla ya Uchaguzi Mkuu, mwakani.


Rais Karume
Mara baada ya Uchaguzi Mkuu mwakani, vyama vya CCM na CUF vilikubaliana rasmi kuwa Zanzibar itakuwa ikiendeshwa kwa mfumo wa serikali ya mseto, lakini sasa imebainika kuwa ni vizuri zaidi kufanyia kazi wazo hilo ili kupunguza msuguano utakaoweza kujitokeza baada ya uchaguzi mkuu.
Baada ya mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM uliofanyika kijijini Butiama, mkoani Mara, Machi, mwaka jana, CCM kimsingi ilikubali kuanzishwa kwa Serikali ya mseto lakini mvutano kati ya chama hicho na CUF ulijitokeza kwa swali kwamba lini mseto uanze.
CCM walitaka mseto uanze baada ya Uchaguzi Mkuu mwakani, lakini CUF wakataka uanze sasa. Wakati mvutano huo ukiendelea kulijitokeza hoja ndani ya CCM kwamba yatafutwe maoni ya Wazanzibari wote kuhusu suala hilo kwa kuwa Zanzibar si ya CCM wala CUF pekee.
Kati ya watu wanaoamini kuwa serikali ya mseto inawezekana kuundwa Zanzibar ili kumaliza mpasuko wa kisiasa ulioibuka tangu uchaguzi wa mwanzo wa vyama vingi uliofanyika mwaka 1995.
Viongozi waliokwishaweka msimamo wao wazi tangu Agosti mwaka jana ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz, alipozungumza na moja ya magazeti ya kila siku nchini.
Mapema wiki hii, Rais Karume alikutana na Maalim Seif, Ikulu ya Zanzibar katika kikao cha faragha ambacho baada ya kukamilika, Seif alifanya mkutano wa hadhara wa wanachama wa chama chake na kuwaeleza kuwa wanamtambua rasmi Karume kwa kuwa hatua hiyo inafungua milango ya makubwa zaidi, ambayo hata hivyo hakuyataja.


Maalim Seif
Hatua ya viongozi hao imetanguliwa na kauli ya Rais Jakaya Kikwete alipozungumza na wananchi miezi michache iliyopita kuwa suala la ufumbuzi wa migongano ya kisiasa Zanzibar bado halijamashinda Rais Karume kiasi cha yeye kuingilia kati.
Hata hivyo, wakati hayo yakijiri hali imekuwa tete katika vyama vya CCM na CUF. Wakati CCM na hususan wahafidhina ndani ya chama hicho wakianza kuratibu mikakati ya kupinga suala hilo, CUF wanaitazama hatua ya kiongozi wao kumtambua Karume kwa hadhari kubwa baadhi wakiamini hiyo ni ‘janja' ya CCM kuweka utulivu wa nchi hususan kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Tayari viongozi mbalimbali wa kitaifa wa vyama hivyo wameunga mkono uamuzi wa CUF kumtambua Karume. Viongozi hao ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, na Kingunge Ngombale-Mwiru ambaye alishiriki kwenye timu ya mazungumzo ya muafaka ya makatibu wakuu wa vyama hivyo.
Suala la utatuzi wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar lilizungumzwa na Rais Kikwete katika hotuba yake ya kuzindua Bunge, Desemba 30, mwaka 2005, akisema mgogoro wa Zanzibar unamsononesha na kuahidi kuufanyia kazi.
 
Makamba anakwambia kiatu cha dhahabu kitarejeshwa kwa kiatu cha dhahabu na kiatu cha dhahabu kipo ccm;kazi kwako!!!!!!!!!!111
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…