Kwani nyie Ngangari kweli? Mtu wa kwanza kutumia hiyo "simu" ni Marehemu Mzee Mloo (Yule wa Kikwajuni) Jee wewe unamuelewa huyo?Ukitaka kuujua ungangari wetu weka jina lako halisi halafu tutukane utajua kama bado ni ngangari ama nini.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani nyie Ngangari kweli? Mtu wa kwanza kutumia hiyo "simu" ni Marehemu Mzee Mloo (Yule wa Kikwajuni) Jee wewe unamuelewa huyo?Ukitaka kuujua ungangari wetu weka jina lako halisi halafu tutukane utajua kama bado ni ngangari ama nini.
Mh!!!!!!!!!!!!!!!
Udumu Ushirika kati ya CUF na CCM
Udumu utawala wa mafisadi na walevi na zidumu fikra za mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba !
Kwani Vinibu si hata wa CUF wanapiga? sasa mnazogana wapi nyie watu. Nafikiri Ulevi ni wa wote, kama vile ilivyokuwa Msala ni wa woteMMhm... Ananikumbusha ziara ya Mh. Rais JK kule PBA
Kwa kuweka kumbukumbu sawa, awali nimetumia neno "...zanzibaris themselves..." na baadaye nikatumia neno "...wazanzibari wenyewe...",kwa maana hiyo hiyo, hilo neno "wote",umelileta wewe kutaka kunilisha maneno au kupotosha maana niliyokusudia,tusema kama ningesema 'wazanzibari wote' kama unavyotaka wewe,basi nisingekuwa nimekosea,hata hivyo, kwa kuwa the move imeanzishwa na kiongozi,upande mmoja(Maalim Seif) anayewakilisha kundi lenye ufuasi mkubwa kabisa wa siasa Zanzibar yaani CUF, na upande wa pili, ni Karume(rais)ambaye ni kiongozi wa Wazanzibari wote....na lengo ni kuendeleza maslahi ya wazanzibar...sasa utegemee Mzanzibari gani hapendi maendeleo?Junius unaposema "makubaliano ni ya Wazanzibari wote" una maana ilipitishwa kura ya maoni au hilo neno "wote" linamaanisha nini? Na kama kweli makubaliano ni ya Wazanzibari wote mbona Hamad alizomewa na wana-CUF wakati akitangaza uamuzi wa kumtambua Karume? Labda ungesema uamuzi ni wa Wazenj "wengi" ningekuelewa! Hongereni Wazenj kwa kuanzisha Chama kipya: CCUF "kwa maslahi yenu!"
CUF kumtambua Karume ni moja, kubwa ni Maalim sasa amalizane na Karume kumaliza game la mgogoro wa vitambulisho vya ukaazi, na kuwasisitiza wafuasi wake wakajiandikishe daftarini, vinginevyo, nimeongea na watu wa kawaida hapa mitaani Pemba, CUF ni watu wa msimamo, wako tayari kwa lolote mpaka kieleweke. Juzi walijitokeza kwa wingi, leo wamegoma tena wasubiri kauli ya Seif kujiandikisha ila wametulia kimya, hakuna vurugu yoyote, ni amani na utulivu kwa kwenda mbele. Ila kimya chao na hiki kisuso, kina mshindo mkuu.
Kwa kuweka kumbukumbu sawa, awali nimetumia neno "...zanzibaris themselves..." na baadaye nikatumia neno "...wazanzibari wenyewe...",kwa maana hiyo hiyo, hilo neno "wote",umelileta wewe kutaka kunilisha maneno au kupotosha maana niliyokusudia,tusema kama ningesema 'wazanzibari wote' kama unavyotaka wewe,basi nisingekuwa nimekosea,hata hivyo, kwa kuwa the move imeanzishwa na kiongozi,upande mmoja(Maalim Seif) anayewakilisha kundi lenye ufuasi mkubwa kabisa wa siasa Zanzibar yaani CUF, na upande wa pili, ni Karume(rais)ambaye ni kiongozi wa Wazanzibari wote....na lengo ni kuendeleza maslahi ya wazanzibar...sasa utegemee Mzanzibari gani hapendi maendeleo?
Ni kweli kabisa, awali wanachama wa CUF,Unguja,hawakuelewa hatua hii ya ghalfa,jambo ambalo ni la kawaida katika wakati wa mabadiliko,popote pale,lakini siku ya pili, mkutano ulifanyika Pemba na wanachi wameunga mkono na hakukuwa na rabsha zozote na siku ya tatu,Maalim akatembelea mashina na matawi ya chama Unguja na mikutano kufanyika katika matawi mengine na viongozi wa chama kuwaelewesha kwa utaratibu wanachama na wapenzi ambao walielewa na kukubaliana na msimamo wa chama. Hata wale ambao siku ile ya mkutano walikuwa na jazba,walikubali ana walimpongeza Maalim na chama cha CUF,baada ya kuelewa vizuri nini kilikuwa kinaendelea.
Mazungumzo yao yalichukua saa mbili, ndani ya closed doors, wao wawili tu! Hii ina maana yaliyozungumzwa wanayajua wao wenyewe! Si ajabu hadi leo hii Waziri Kiongozi nae yupo gizani kama watu wengine!Haya uchaguzi unakaribia, ni ahadi gani ambazo Mh. Karume amewahakikishia CUF kwamba maisha ya wana CUF hayatakuwa hatarini ikiwa CUF itamtambua yeye kuwa ni rais wa Zanzibar..Na isipotokea je, kama walivyoahidiwa Muafaka.. ndio itakuwaje?
Kuwa na wishes ni kitu kimoja kufanikisha wishes ni kitu kingine..ndugu hata mrema alitaka kuwa rais lakini siku hazigandi..kuna mkakati gani zaidi ya kumsikiliza Maalim seif alone???CUF ni chama cha wananchi ,jiandae kuwa na rais Professor wa kwanza Tanzania.
Nchi itageuzwa darasa!CUF ni chama cha wananchi ,jiandae kuwa na rais Professor wa kwanza Tanzania.
Wikiendi inaanza tena.
Mkuu inaonesha unaanza kuota...
Maalim Seif alikuwa miongoni mwa waanzilishi na waasisi wa CCM Zanzibar...anaijuwa CCM kuliko hata Jakaya Kikwete..anajuwa nje ndani ya CCM...ndiyo Maana alikubali jeuri ya Mwalim Nyerere kuwa "bora uwe mpinzani nje ya CCM kuliko ndani yake..." na Maalim akachkuwa ustaarabu wake...unajuwa alipokelewa vipi na Wazanzibari...kwa kishindo kikubwa hakijawahi kutokea,mpaka mshairi mmoja maarufu visiwani akamtungia shairi lililoimbwa na Naad Ikhwan Safaa(Malindi musical club),akatunga na watu wakaimba:
Mtajirusha wenyewe, roho na akili zenu
Kisemeni msizuwe, kilichomtoa kwenu
Na huku kaja mwenyewe, kajuwa hamna lenu
Ya bure yenu mayowe, huyu sasa siye wenu.
Chorus:Mtajirusha wenyewe roho na akili zenu na msema msizuwe kilicho mtoa kwenu.
Sasa Maalim arudi CCM akatafute nini...wazanzibar hawajasahu ahadi yake ya mwaka 1989 katika uwanja wa Tibirizi,Pemba...alisema "...nitakuwa pamoja nanyi hadi mwisho wa maisha yangu na sitawasaliti..."
Na mwenyewe Maalim heshi kutukumbusha ahadi hiyo mara kwa mara...akionyesha kuwa ni mtekelezaji wa ahadi zake na si mnafiki...ipo siku yatatimia kama si leo kesho
Endelea kuota.
Labda nikupe kwa ufupi...Maalim Seif ni Mpinzani wa CCM kabla ya mfumo wa vyama vingi...hapo ndo sikuelewi unachoongea.upepo unapovumia ustadhi si huko unapotaka wewe watch this space for a soon to be a breaking news! yule Maalim kwa taarifa yako ni shushushu na aliwekwa kule kuwapumbaza Wazanzibari! sasa uamuzi umetolewa wa yeye kurudi rasmi alipotokea we subiri utaona na kuniambia humu ndani