Matokeo ya mchujo TAKUKURU: Let's be honest with each other

So aliambiwa na yule Mzee atoe around 4 million ili aweze kupatiwa nafasi,
Mkuu, binafsi sijui kama kweli mchezo mchafu umefanyika. Ila kwa kuangalia dogo mmoja ambaye anafanya internship ofisini kwetu aliomba nafasi ya afisa uchungu akafanya mtihani wa mchujo na amepita. Huyu dogo namjua hana connection na hana huo uwezo wa kuhonga. But at least amefanikiwa kupenya huo mchujo. Hata hapa job dogo ana discipline ya kazi na ana uwezo mzuri kichwani.
Binafsi nilikuwa ninauhakika dogo atapenya, na kweli amefanikiwa. Kwa kweli kwa hili binafsi nitawatetea TAKUKURU maana nimeona mtu ambaye ninamjua amevuka hatua hii bila kushikwa mkono.
Ninaamini hata hatua inayofuata atapenya pia bila kubebwa
 
takukuru kuna watu wao ukiona mtu ana connection amepenya basi jua uyo ni geresha anaenda kuondolewa kwenye iyo oral
 
takukuru kuna watu wao ukiona mtu ana connection amepenya basi jua uyo ni geresha anaenda kuondolewa kwenye iyo oral
Namuombea huyu intern wetu apite. Dogo yuko vizuri sana. Kama atakosa nafasi kwa hila, basi kweli ni kwamba kama nchi tutakuwa tumeamua kukumbatia uovu hata kwa taasisi ambayo inatakiwa iwe ndiyo kinara wa kupambana na uovu
 
Elimu yako haijakusaidia.
 
Nina rafiki yangu ana diploma yupo TPB ( sasa TCB) analipwa zaidi ya hiyo laki 6. Kwakua hajanitajia mshahara exact labda nikikutajia kiwango anachoweza kukopa utapata picha.

Anaweza kukopa Milioni 21.

Hapo inakuaje?
Huyo rafiki yako hayuko PCCB hapa tunazungumzia PCCB. kuhusu mkopo hata sijua criteria wanazoangalia huko benki, tangu niajiriwe sijawahi kukopa ba sitokaa nikope benki.
 
Takukuru wamekuja kujitetea [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Yaani mchakato wa kuwapata wachunguzi wanaoenda kupambana na rushwa wanapata kazi kwa rushwa

Rushwa haitokwisha, mkuu nenda kajiajiri tu mapori yapo ya kutosha
 
Huyo rafiki yako hayuko PCCB hapa tunazungumzia PCCB. kuhusu mkopo hata sijua criteria wanazoangalia huko benki, tangu niajiriwe sijawahi kukopa ba sitokaa nikope benki.
PCCB si autonomous au?
 
Kama imeshindikana basi, tafuta opportunity nyingine, maana hapa halitapatikana jibu, labda nenda makao makuu ya ofisi zao kateme cheche kule.
 
Namuombea huyu intern wetu apite. Dogo yuko vizuri sana. Kama atakosa nafasi kwa hila, basi kweli ni kwamba kama nchi tutakuwa tumeamua kukumbatia uovu hata kwa taasisi ambayo inatakiwa iwe ndiyo kinara wa kupambana na uovu
Mkuu, kuna wazuri wengi pengine zaidi ya huyo ulonaye karibu. Ni mazingira magumu wanapitia yanayowanyima fursa ya kuajiriwa kwa kufuata taratibu na misingi tulojiwekea. Uovu unaozungumzia hapa upo, yes upo, tena kwenye hizi hizi taasisi ambazo pengine tunaziamini hazina makando kando. Nchi hii inahitaji uponyaji kwenye mambo mengi sana.
 
Sasa wewe unaomba kazi kuzuia Rushwa Ubataka uhonge uipate itazuia nini?? Malalamiko kweli yapo na hayo ni kawaida kutokana na uhaba wa kazi...La Msingi tupange mkakati tupambane kuondoa hili janga...
 
Mi nashangaa wanalalamika,kama huna connection ukae tu kwa kutulia.achana na ajira za serikali,vibarua tu huku viwanda vya mshahara wa laki mbili kwa mwezi bila mchongo hupati kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…