Matokeo ya mchujo TAKUKURU: Let's be honest with each other

Matokeo ya mchujo TAKUKURU: Let's be honest with each other

We acha tu hana raha msepa anasema paper simple kwake sana aliona alibaki dom huko tangu huo mwezi wa kwanza ila mambo yamekuwa kinyume
Alitegemea akipata 100 ndio kapata kazi? Kuna michakato ya backend lazma ifanyike kama hamjui mtu kaumia.
 
Huu ni zaidi ya usanii kama si uhuni. Yaani watoto wa maskini wanasafiri kutoka Mpitimbi Songea Vijijinia au Mkwenangi Katavi kuja Dodoma kufanya Usaili na kuambilia patupu kumbe kuna watoto wa wenye nazo hata hawajishughulishi kuhudhuria Usaili na eti majina yao yanatoka wamefaulu. Ushahidi wa majina hayo ninao wote.

Hakika nchi ngumu sana hii. Mheshimiwa Mama Samia ingilia kati uonevu huu
Mlaumu baba yako hakuwatengenezea nafasi mapema😅
 
Same to me. Kuna ambaye niliwasiliana nae na alinitumia hadi screenshot ya msg za kigogo anaewapigania watoto wawili. Niliumia sana, basi tu ndio vile utafanyaje. Yaani sisi tulienda Dom kufanya Aptitude test halafu wengine wamekaa makwao wanaperuzi kwenye pages za umbea Instagram na mwisho wa siku wana nafasi za kazi tayari.
Hahahahhah halafu huyo mzee atasimama na kusema vijana mkajiajiri ajira hakuna ila wanae anawapambania wakakae kwenye AC nyie mpambane na virungu vya migambo na moto wa masokoni😅
 
CARDLESS tumia busara,sio suala la wote kuitwa,inachotakiwa ni HAKI,si sawa watoto wa maskini watumie gharama kusafiri kutoka makwao mpaka Dodoma,gharama za malazi na chakula halafu nafasi wapewe watoto wa wakubwa ambao hata kuhudhuria Usaili hawakuhudhuria,hii si sawa. Chombo kama TAKUKURU kikiwa KICHAFU wakati kipo Kisheria kupambana na mambo MACHAFU ni aibu
Utafanyaje hii ndio Tanzania mkono mtupu haulambwi na mambo yote yanaenda kimichongo!😅
 
Familia duni hizo mzee, ww na pesa zako utakubali mtoto wako awe TAKUKURU??
Familia duni we unajua Mkurugenzi wa Takukuru anaweza kuwa na maisha kuliko mjomba wako anaemiliki bar 3 temeke?

Msiongee kipumbavu tu watu wa serikalini wapo ambao wana mitonyo mirefu tu na maisha bora kuliko wapambanaji. Wana miliki mijengo ya maana na mabiashara vile vile licha ya yote usalama ni full time.

Tafta hela upate connection watoto wako wasije kuteseka
 
Tanzania ajira ni vita ! Yaani watu wanachutama na kufanya kila linalowezekana wachomeke matakwa yao. Piga ua garagaza, sio mbaya kama mtu ana sifa but inaaishia kuacha talented people wasio na wakuwashika mkono
Sio tu vita bali ajira yenye maslahi mazuri. Kwa level za mishahara ofisi inayolipa 1.7m au zaidi maslahi ni mazuri. Humo kuna hata wafanyakazi wengine wamekimbilia humo kuhonga ili wapate chance imagine unatoka ofisi unayolipwa laki 7 gross mpaka ofisi ya kulipwa 2.2m kwanini usipambane?

Wazazi wanaumiza vichwa sana mtoto umemsomesha anazeekea nyumbani hata kuoa hataweza maana hata kazi ya maana ya kulisha mke hana. Kwanini usihonge kama inawezekana mwanao apate kazi
 
Mkuu, kijana kama huyo ni hasara kuanzia kwa familia yake mpaka Taifa. Ndio sababu nime comment kwake ni takataka.
We ndo taka taka ndo maana sikutaka kubishana na ww, mara nyingi mkisha feri written ndo maana kuleta porojo kuwa usaili haukuwa wa haki, ukweli ni kwamba uliferi written.

Ukiwa mpiga porojo kama wale utaishia kuwa mchawi tu
 
Mitihani ya shule ikivuja mnashangilia huto sikia hata mmoja akisema kwa nn mnavujisha mitihani ili watu wafaulu, ila ya usaili ikivuja utaona nyuzi zimejaa kila kona ya dunia taasisi furani wanawapa watu mitihani, sijui wanapendelea watu wao.
 
Mkuu, binafsi sijui kama kweli mchezo mchafu umefanyika. Ila kwa kuangalia dogo mmoja ambaye anafanya internship ofisini kwetu aliomba nafasi ya afisa uchungu akafanya mtihani wa mchujo na amepita. Huyu dogo namjua hana connection na hana huo uwezo wa kuhonga. But at least amefanikiwa kupenya huo mchujo. Hata hapa job dogo ana discipline ya kazi na ana uwezo mzuri kichwani.
Binafsi nilikuwa ninauhakika dogo atapenya, na kweli amefanikiwa. Kwa kweli kwa hili binafsi nitawatetea TAKUKURU maana nimeona mtu ambaye ninamjua amevuka hatua hii bila kushikwa mkono.
Ninaamini hata hatua inayofuata atapenya pia bila kubebwa
Huyo si amejitolea na anafahamika hapo ofisini! Utasemaje hana connection wakati kuna ma bro wake hapo ofisini. We unadhani wangemuachaje kwenye nafasi 200 hizo?
 
Kwanini mamlaka za juu zisiingilie swala hili?kwani haiwezekani au hawana taarifa?
Nawaliohusika wote wachukuliwe hatua kali kwa mujibu wa sheria hii ni nchi yetu sote
Ukumbuke tuko awamu ya 4B mzee subiria tume ya mchongo
 
Huyo si amejitolea na anafahamika hapo ofisini! Utasemaje hana connection wakati kuna ma bro wake hapo ofisini. We unadhani wangemuachaje kwenye nafasi 200 hizo?
mkuu haujamuelewa uyo jamaa, sio kwamba anamaanisha uyo dogo anajitolea pccb noo, anajitolea kwenye ofisi yao nyingine ya private hawana mausiano yeyote na pccb
 
mkuu haujamuelewa uyo jamaa, sio kwamba anamaanisha uyo dogo anajitolea pccb noo, anajitolea kwenye ofisi yao nyingine ya private hawana mausiano yeyote na pccb
Duh sasa ofisi ya private ila kachaguliwa PCCB?
 
Huyo si amejitolea na anafahamika hapo ofisini! Utasemaje hana connection wakati kuna ma bro wake hapo ofisini. We unadhani wangemuachaje kwenye nafasi 200 hizo?
Mkuu, hao mabro wake unaowazungumzia ni wepi? Sisi ni independent law firm sasa sijui ulitaka kusemaje hapa!
 
Aptitude test karibia zote wanandika number sioni haja ya kulalamika,

Pili kutotoa no na kuleta majina kama ni mtu ulie soma excel ni kazi ya dk tuu wala hutoki jasho ya matakoni.

Ajira kama hizi ni kutoa matangazo ya kuleta lawama bora wangekuwa wanajiliwa kimia kimia mtoto wa fulani na fulani sijui msaafu fulani rahisi tu.
Naunga mkono hoja, ni bora waajiri kama TISS
 
We ndo taka taka ndo maana sikutaka kubishana na ww, mara nyingi mkisha feri written ndo maana kuleta porojo kuwa usaili haukuwa wa haki, ukweli ni kwamba uliferi written.

Ukiwa mpiga porojo kama wale utaishia kuwa mchawi tu
Eti huyu nae anachangia hoja ya msingi. Mkisha "feri" ndio nini? "uliferi" ndio nini?
[emoji706][emoji706]
 
Back
Top Bottom