Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Mtaa wa Lindi leo.
Tutapiga kelele hadi serikali msikilize uozo uliokuwa wa Jiji la DSM.
Jiji ilitoa tenda kwa wachina miaka minne tu iliyopita.
Kwa kawaida ujenzi wa barabara, barabara inatakiwa kutokuwa na matatizo yoyote ndani ya miaka 10.
Barabara ya Lindi, Kariakoo ndani ya miaka minne imekufa kabisa.
Lami unene hauzidi robo tatu inchi.
Huu nakumbuka ulikuwa mkopo wa World Bank.
Wakati huo Jiji likitoa tenda hizo za barabara za Kariakoo waliweka vikwazo vingi kuwazuia wakandarasi wazawa.
Watoa rushwa, wachina wakapata kazi.
Matokeo ya rushwa wote tunaona, ndani ya miaka minne barabara kwisha kabisa.
UPDATE
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais ndg Simbachawene ame sema sheria zibadilishwe ili viongozi waliohusika katika rushwa hasa kwa mfano barabara kuharibika ndani ya miaka miwili mitatu baada ya kujengwa, washitakiwe.
BIG UP Nd Simbachawene, sasa paka anafungwa kengele.
Ni matumaini yangu kuwa wakuu serikalini wameiona mada hii.