Matokeo ya Rushwa Halmashauri JIJI, serikali inafumba macho, utafikiri haioni!

Matokeo ya Rushwa Halmashauri JIJI, serikali inafumba macho, utafikiri haioni!

View attachment 2814721View attachment 2814722View attachment 2814723View attachment 2814724View attachment 2814725
Mtaa wa Lindi leo.

Tutapiga kelele hadi serikali msikilize uozo uliokuwa wa Jiji la DSM.

Jiji ilitoa tenda kwa wachina miaka minne tu iliyopita.

Kwa kawaida ujenzi wa barabara, barabara inatakiwa kutokuwa na matatizo yoyote ndani ya miaka 10.

Barabara ya Lindi, Kariakoo ndani ya miaka minne imekufa kabisa.

Lami unene hauzidi robo tatu inchi.

Huu nakumbuka ulikuwa mkopo wa World Bank.

Wakati huo Jiji likitoa tenda hizo za barabara za Kariakoo waliweka vikwazo vingi kuwazuia wakandarasi wazawa.

Watoa rushwa, wachina wakapata kazi.

Matokeo ya rushwa wote tunaona, ndani ya miaka minne barabara kwisha kabisa.
UPDATE
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais ndg Simbachawene ame sema sheria zibadilishwe ili viongozi waliohusika katika rushwa hasa kwa mfano barabara kuharibika ndani ya miaka miwili mitatu baada ya kujengwa, washitakiwe.

BIG UP Nd Simbachawene, sasa paka anafungwa kengele.
Ni matumaini yangu kuwa wakuu serikalini wameiona mada hii.
Mwenye barabara alishaondoka so tegemea matanuru baada ya miaka kazaa.
 
Serikali Awamu ya Sita imeondoka?
Kuna kikundi cha wahuni kinamhujumu Dkt Samia, ni kile cha Makamba, yaani fikiria yule aliyekwapua mabilion kazaa toka bank 6 na kuondoka nchini, sasa unadhani ni mchongo wa mtu wa kawaida??? Au issue ya kuvuruga umeme, kandarasi za barabara zimejaa rushwa yaani ni balaa sana. Ila uzuri Dkt Samia ni mwenda pole yaani watakuja kufumuliwa na kupotezwa kabisa kwenye siasa
 
Tutataka hicho kikundi ndani ya serikali kijulikane na kuchukuliwa hatua.
Barabara itafumukaje baada ya miaka miwili mitatu baada ya kujengwa?
 
Back
Top Bottom