LGE2024 Matokeo ya Uchaguzi Mwanza yaanza kutangazwa, CCM yaongoza maeneo mengi ikifuatiwa na CHADEMA

LGE2024 Matokeo ya Uchaguzi Mwanza yaanza kutangazwa, CCM yaongoza maeneo mengi ikifuatiwa na CHADEMA

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika baadhi ya mitaa Jijini Mwanza yameanza kutangazwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikionesha kuongoza kwenye vituo vingi Wilayani Nyamagana.

Aidha, licha ya baadhi ya Mitaa Wilayani Nyamagana na kushuhudiwa Wagombea wa CCM wakitangazwa kuongozwa Kwa kura wakifuatiwa na wagombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao hata hivyo wameeleza kutoridhishwa na mwenendo wa Uchaguzi huku wakibainisha baadhi ya changamoto kuwa ni pamoja na kuongezwa kwa vituo na Wapiga kura hewa.
 
Athari za yule jamaa zitachukua muda mrefu kuisha

Zamani uchaguzi wa serikali za mitaa haki ilikuwa inatendeka japo sio Kwa 100%

Leo kuanzia katika grassroots hadi juu kuna uchafuzi. Kura za mazengo n.k

Sioni umuhimu wa kupiga kura Kwa sasa
 
Yule jamaa alifuta uchafu wote wa matapeli wanaojiita wapinzani
 
Ameshafariki ila si unaona legacy yake inavyoishi, mpaka umemkumbuka ujamtaja mkapa wala mwinyi
😁😁😁 wewe unazungumzia utoto sasa I can't make any argument with you anymore.
 
Nyamagana Ina mitaa 178 ccm imepata mitaa 175 chadema 3
Taja walioondokewa maana hakuna sehemu ambayo hamjawatoa wagombea wa chadema. Taja mliwatoa wangapi wakabaki wangapi? Ndiyo utaje ushindi maana wengine wamepita bila kupigiwa kura maana walikua wenyewe tu
 
Tumesha ipigia ccm kura, tutu lie sasa ushindi ni mnono na wa kihistoria.
Tanzania hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Sasa huo ushindi unausubiri kwenye uchaguzi gani?
 
Taja walioondokewa maana hakuna sehemu ambayo hamjawatoa wagombea wa chadema. Taja mliwatoa wangapi wakabaki wangapi? Ndiyo utaje ushindi maana wengine wamepita bila kupigiwa kura maana walikua wenyewe tu
Wilaya ya Nyamagana wagombea wote walioteuliwa na vyama vyao hakuna hata mmoja aliyeenguliwa kugombea wote walipitishwa.
 
Huku haukuwa uchaguzi bali ushenzi wa namna ya ajabu.
 
Back
Top Bottom