Matokeo ya VPL: Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Dodoma Jiji FC

Matokeo ya VPL: Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Dodoma Jiji FC

Sijawahi kuna pamoja na ukubwa wa team kama Barca, Real, Man, Liver sijui city na wengine wengi wakaenda ugenini kucheza halafu watu waka support team ya wageni. Wenzetu mapenzi wanayo na team kubwa lakini full support team zao za nyumbani...
Catalonia.. nioneshe picha ya shabiki wa espanyol akiishangilia barca vs timu ya ugenini, madrid: shabiki wa atletico aishangilie real! Manchester: shabiki wa city aishangilie utd! liverfool aishangilie everton?

Mwishoni umejijibu mwenyewe vizuri, timu ya watu wa mwanza ni pamba, dodoma ni CDA na mji, Mbeya ni tukuyu, tabora ni milambo, moro ni reli huwezi kuzifuta mioyoni na siku zitakaporudi ni wageni tu ndio watashabikia simba na yanga. Tatizo hizi timu hazina mashabiki na mbaya zaidi mtu hawezi kushabikia timu asiyoipenda. Angalia Azam, kmc, mtibwa, prisons,jkt you can't buy football fan
 
Sijawahi kuna pamoja na ukubwa wa team kama Barca, Real, Man, Liver sijui city na wengine wengi wakaenda ugenini kucheza halafu watu waka support team ya wageni. Wenzetu mapenzi wanayo na team kubwa lakini full support team zao za nyumbani. Kwa hili tutabaki kuwa watumwa wa team hizi mbili. Kidogo miaka ile ya Pamba, CDA, Reli sijui Tukuyu hata RTC Kigoma team zilikuwa zinapendwa kwao. Penda Simba na Yanga sababu ya ukongwe ila wakija nyumbani kwenu shangilia team ya nyumbani nchi zote ndio utamaduni. Najuwa nitatukanwa humu ila ndio ukweli
Sio lazima saaana kufuata utaratibu wao..
 
[emoji3]
FB_IMG_1612469345868.jpg
 
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League VPL kuendelea kutimua vumbi leo January 4, 2021kwa mechi mbili kupigwa, ambapo Dodoma Jiji FC wanakabiliana na Mnyama Mkali Simba SC, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, huku KMC wakicheza na Namungo FC kwenye uwanja wa Uhuru Dar es salaam.

Mechi hizi ni za viporo na ni mwanzo wa kurejea kwa Ligi Kuu Tanzania VPL, baada ya kusimama kupisha michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN ambapo bado inaendelea nchini Cameroon.

Mchezo wa Dodoma Jiji FC na Simba SC unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 hasa ukizongatia ni mara ya kwanza kukutana kwenye VPL.

Kocha wa Simba SC Didier Gomes ambaye atakongoza jahazi kwanza mara ya kwenye VPL, amesema " Utakuwa mchezo mgumu lakini tupo tayari kupambana ni muhimu sana, tuna michezo mitatu mkononi tunatakiwa kushinda" amesema Gomes.

Kwa upande wa Kocha wa Dodoma Jiji, Mbwana Makatta amesema " Ni mechi muhimu kushinda kutokana na kuwa sehemu ambayo si rafiki kwenye msimamo wa VPL, lakini wapo tayari kuwakabili Simba SC na hata wachezaji wanalijua hilo.

Yote ni ndani ya dakika 90 za mchezo. Kumbuka mitanange hii ni kuanzia saa 10: 00 jioni Usikose Ukasimuliwa.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.

View attachment 1694210View attachment 1694211

Update;

===========================

Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Dodoma Jiji FC, mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma

Simba ilikuwa ya kwanza kuandika bao kupitia kwa mshambuaji Maddie Kagere na Bernard Morrison akifunga bao la pili huku Mkandala akifunga bao moja upande wa Dodoma Jiji FC

FT, VPL; Dodoma Jiji FC 1-2 Simba SC
.
 
Utopolo wanazidikudanganywa, kwanza walidanganywa Morison ana mshipa halafu wakaambiwa ana kesi lazima yeye na yanga walipe pesa ili isikilizwe mwisho wakaambiwa amezuiwa kucheza hadi kesi yake iishe
 
Hivi benchi la ufundi la simba wanashindwa kumwambia Wawa apunguze mipira mirefu maana anapiteza mipira mingi
Amekua akiilaazimisha sana sijui kwanini.niliona pia mechi na Tp mazembe alipoteza mipira mingi kwa kuipiga tu mbele bila accuracy .inabidi benchi la ufundi limuambie na nilazima aangalie timu wanayocheza nayo.Wawa ni beki mzuri ila kuna kipindi anakua mtegevu hasa kwenye mipira ya vichwa.
 
Kama uliona Cameron na Mali mipira ya kona,
Walikua wanapambana wote na kuhamasishana kuzuia

Wawa ni beki ndo kwanza angetakiwa washurutisha wenzie na yeye mwenyewe kama Lamine pia anavyofya
Yeye sasa anacheza ki bos boss wala hajali
Amekua akiilaazimisha sana sijui kwanini.niliona pia mechi na Tp mazembe alipoteza mipira mingi kwa kuipiga tu mbele bila accuracy .inabidi benchi la ufundi limuambie na nilazima aangalie timu wanayocheza nayo.Wawa ni beki mzuri ila kuna kipindi anakua mtegevu hasa kwenye mipira ya vichwa.
 
Kama Mashabiki wataamua kushabikia timu za mikoa yao naimani tutakua na ligi bora sana, Jana Dodoma jiji walikosa morali japo walikua na mipango mizuri wawapo golini ila ukosefu wa mashabiki wao umechangia kucheza walivyocheza kiasi utadhani wao ndio wapo ugenini.
 
Kama uliona Cameron na Mali mipira ya kona,
Walikua wanapambana wote na kuhamasishana kuzuia

Wawa ni beki ndo kwanza angetakiwa washurutisha wenzie na yeye mwenyewe kama Lamine pia anavyofya
Yeye sasa anacheza ki bos boss wala hajali
Yaa ni sahihi unapowatuma wenzio na wewe uwe wakwanza kutumika.kuna nafasi ya mwisho ambayo waliipata Dodoma Jiji ilipigwa foul jamaa akapiga kichwa peke yake na alitakiwa kukabwa na Wawa lakini Wawa akamuacha na ni manula tu alieokoa lasivyo ingalikua ni sare,ukiangalia vizuri kwa umakini ulitokea mzozo pale golini.

Tadeo Lwanga nafikiri alikua akifoka sana pale kumfokea Wawa kwanini amuache mtu apige kichwa ilhali yeye anamtizama, tu.wakaja wachezaji wengine wakaamua amua na mpira ukaishia pale.
 
Back
Top Bottom