A
Anonymous
Guest
NB: Lalamiko hili linawasilishwa kwa heshima na kwa nia ya kulinda haki za wanafunzi pamoja na uadilifu wa kitaaluma wa Chuo.
Kumekuwa na ucheleweshaji wa kutolewa kwa matokeo, hususan kwa wanafunzi waliofanya mitihani ya marudio (Supplementary/SUP), ambapo hadi sasa baadhi ya matokeo hayajawekwa kwenye mfumo. Hali hii imewaacha wanafunzi katika sintofahamu, kwani licha ya kumaliza masomo, hawajui kwa uhakika iwapo wamefaulu, wanatakiwa kufanya mtihani mwingine au kurudia baadhi ya masomo.
Hali hii imekuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwa wanafunzi, hasa ikizingatiwa kuwa mahafali yanakaribia huku baadhi yao wakiwa hawajui hatma ya masomo na matokeo yao.
Aidha, kumekuwa na viashiria na malalamiko kuhusu uwezekano wa ukiukwaji wa maadili na matumizi mabaya ya mamlaka katika mchakato wa utoaji wa alama, ikiwemo madai ya vitendo vya rushwa ya ngono. Kwa kuzingatia uzito wa madai haya, tunaomba mamlaka husika zisiyapuuze, bali zifanye uchunguzi wa siri, huru na wa haki ili kubaini ukweli na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Chuo.
Tunaomba Uongozi wa Chuo:
Tunasisitiza kuwa tunachohitaji ni haki yetu ya msingi ya kupata matokeo yetu kwa wakati na kuhakikisha kuwa mchakato wa kitaaluma unasimamiwa kwa haki na uadilifu.
Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua mapema ili suala hili lisizidi kuwaathiri wanafunzi na maandalizi yao ya kuhitimu.
Kwa heshima,

- Kufuatilia na kuhakikisha matokeo yote yanayostahili kutolewa yanaingizwa kwenye mfumo kwa wakati;
- Kuhakikisha wanafunzi wanapewa taarifa na majibu ya wazi kuhusu hali ya matokeo yao;
- Kuhakikisha mchakato wa utoaji na usahihishaji wa alama unafanyika kwa haki, uwazi na uadilifu;
- Kufanya uchunguzi kuhusu viashiria na malalamiko ya ukiukwaji wa maadili pamoja na matumizi mabaya ya mamlaka;
- Kuchukua hatua stahiki kwa wahusika watakaobainika kukiuka taratibu, kanuni na maadili ya Chuo.