Matukio mawili yaliyoniacha na tafakuri kubwa

Kabisa....hapo unaweza kuta kuna shule nyingi tu wilaya ya chalinze au bagamoyo hazina vyoo au madarasa ya kutosha au nyumba za walimu nk nk. Priorities zetu zina mushkeli mahali. Ubinafsi tu.
 
Mimi na shangaa sana kuona Benz ya 250 million emekuwa mjadala wa taifa ,huku kuna wakurugenzi 160 wamenunua magari bei 300 mpaka 450 million ,wakugurugenzi hawa wanao staili gari isio zidi 100 million !! Swali ni Hamuoni,hamjui au nichuki tuu !!????
 
Ila kuna tetesi hii Benz ni moja wapo kati ya Benz 20 ziliotolewa kama zawadi na Mfalme na Sio mwingine niyule aliojenga msikiti .mkubwa dar ,kwa hiyo hoja ya Benz ipe mtazamo huo, vinginevyo tuuza zawadi
Hiyo ni chini ya zulia wengi hatuijui..mpaka itakapothibitika vinginevyo... Tutaandika yatokanayo
 

..nadhani SHERIA ya mafao ya viongozi wakuu wastaafu siyo nzuri.

..sheria ilipaswa kuelekeza kuwa wastaafu watatunzwa na serikali ktk masuala ya makazi, matibabu, usafiri, ulinzi, na wasaidizi.

..kinachoendelea sasa hivi, na kinachotia ukakasi, ni kuona kama vile sheria imeelekeza viongozi wastaafu wajengewe / wapewe wao binafsi majumba makubwa ya kifahari.

..leo hii tunashuhudia Mzee Kikwete, na Mzee Mwinyi wakikabidhiwa majumba ya kifahari. Lakini mkumbuke kwamba bado kuna kina Mzee Warioba, Mzee Malecela, Mzee Msuya, Mzee Shein, Mzee Bilal,Mzee Salim Salim, Mzee Sumaye, Mzee Lowassa, Mzee Pinda, Mzee Msekwa, na Mama Makinda.

..Wote niliowataja hapo juu ni viongozi wastaafu wanaotambulika na sheria iliyotumika kuwajengea majumba makubwa Mzee Mwinyi, na Mzee Kikwete.

..Nadhani kinachoendelea ni utekelezwaji mbaya wa sheria ambayo ilitungwa na BUNGE kwa nia njema.

NB.

..Pia kuna nafasi za UBUNGE WA KUTEULIWA ambapo umekuwepo utamaduni wa wenza au watoto wa viongozi wastaafu kuteuliwa.
 
Mzee Mshana...

Nisingekuwa mwenye ukakasi iwapo makundi mengine katika jamii yangalikuwa na walau 1/3 ya kile walichonacho viongozi.

Nadindokwa na machozi sio ya wivu bali uchungu kuona mwanangu anasoma Kayumba jumla ya wanafunzi 800 na idadi ya walimu ni watatu (idadi ikimjumlisha Mwalimu Mkuu).

La ajabu zaidi si kwamba wenye taaluma ya ualimu hawapo la hashaa wamejaa tele, na wanalalamikia ajira kila uchao na uchwao.

Mzee Mwinyi kama kaikataa ile gari ni sahihi kabisa na kama kaipokea anajua sehemu ya dhulma tunayotendewa walipa kodi wa nchi hii.

NB:
Tatizo sio chama cha siasa bali mfumo uliokumbatia waimbaji na kuwatupa waimbiwaji. Siku Waimbiwaji tutakapogoma kusikia wanachoimba sijui itakuaje?
 
Nadindokwa na machozi sio ya wivu bali uchungu kuona mwanangu anasoma Kayumba jumla ya wanafunzi 800 na idadi ya walimu ni watatu (idadi ikimjumlisha Mwalimu Mkuu).

La ajabu zaidi si kwamba wenye taaluma ya ualimu hawapo la hashaa wamejaa tele, na wanalalamikia ajira kila uchao na uchwao.[emoji2827][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Huu uzi ni wa wivu na majungu ya kitanzania. Mleta mada kama wazazi wako hawakusoma kukuwezesha kuishi maisha ya juu usiwachukie wanaoyaishi.

Hizi ni mentalities za kimaskini kufuatilia riziki za watu. Kikwete ni mstaafu aliyeifanyia mengi nchi hii kupewa nyumba ni suala dogo sana kwa wanaojielewa.

JK kajenga MOI, Kajenga barabara na kila aina ya miundo mbinu akiwa rais, nyumba moja hata kama thaman yake ni tsh milioni 500 akipewa kuna ubaya gani?. Huwezi ukalinganisha na mema aliyoifanyia nchi hii.

Lako ni andiko lenye msingi wa wivu na roho mbaya ya kiafrika.
 
Kinacholeta ukakasi katika gari aliyo'zawadiwa' Mzee Mwinyi ni kwamba serikali hairuhusiwi kutumia kodi za wananchi kutoa ZAWADI kwa watu bali wajibu wa serikali ni kutoa HAKI.
Kodi za wananchi ndizo zinazowatunza marais. Ile misafara unayoiona mpaka juu kunakuwa na helikopta ni kodi za wananchi.

Kama tunaweza kugharamia tshs bilioni mbili kwa mwaka ule msafara wa rais peke yake, kuna dhambi gani kumpa benzi la milioni themanini?.
 
Uzi ulimejaa uongo mtupu
1. Mwalimu Julius Nyerere yeye alijengewa na jeshi kabla ya sheria kupitishwa ya kujengea viongozi nyumba
1. Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi alishakabidhiwa nyumba na rais SSH, kahamia tayari, lakini pia gari alipokea ila lilifanyiwa marekebisho kukidhi hali yake ya kiumri
2. Rais mstaafu Jakaya Kikwete alishabidhiwa nyumba na rais SSH, kahamia tayari, kwa mjibu wa sheria iliyotungwa enzi za Mkapa
3. Ni hayati JPM pekee ndio bado hajajengewa nyumba kwa mjibu wa sheria hiyo hiyo...sheria itatoa mwongozo endapo kama rais anafariki kabla ya kumaliza kipindi chake kama anastahili kujengewa nyumba; ngoja tusubiri tuone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…