Matukio na Masimulizi ya Wazee wa Mwaka 47

Matukio na Masimulizi ya Wazee wa Mwaka 47

Kuna mama mmoja mrembo sana aliukwaa alikuwa akiishi Mitaa hiyo. Aliniuma sana yule mama wa rafiki yangu.
1994
Alikuwa ni mwanamke pekee aliyemiliki tv na kombe la dunia mwaka huo wengi walienda pale ukiangalia burudani za soka.
Basi sharti ilikuwa iwe umeoga ndio mtaruhusiwa kuingia na unaulizwa kabisa..
Vipi alishafariki ama aliwahi njugu?
hukuwa mmoja wapo wewe na lotion zako???
Si unajua nina ugonjwa wa presha, mbona unauliza maswali magumu jirani 😜

Mimi nilikuwa mtu mwema ujue, kwahiyo alinipita mbali 😂🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
Kama vp twende zetu selou
Hili neno, twenzetu tukapumzike huko.....nifanye maandalizi?😉
 
Nina matukio kazaa tuanze na haya
1: kipindi niko darasa la tano, usiku mmoja nilitoka nje kukojoa usiku wa manane, jilani na nyumbani kulikua na tajiri alijijenga vizuri na kuweka uzio na kuweka mlinzi juu, ujenzi wa zamani wa uzio mbele ya nyumba ulikua wazi, walikuwa wakichomelea vyuma au nondo ili show ya nyumba iweze kuonekana kwa mtu atakae pita mbele nyumba iweze kuonekana . Basi mi nilipotoka nje wakati nakojoa kuangalia pembeni kulikua na mti mkubwa wa mchristmas juu ya mti nikaona mtu mrefu miguu sioni akawa kama anasogea nilipo aisee nilitoka mbio nikakimbilia kwa mlinzi huku napiga kelele kuomba msaada, wazazi wakatoka nje lakini yule mtu hakuonekana tena..
Pole sana Mkuu, miaka ya zamani hayo mambo yalikuwa mengi sana vijijini, Mimi nimewahi kukutana na kisa cha namna hiyo pia.

Ilikuwa majira ya saa 7 usiku, nilikuwa natoka prepo kupiga msuli, wakati naelekea bwenini nilikutana na paka mkubwa na mrefu kama Simba, nilipomkazia macho na kumwangalia usoni, akabadilika na kurudi umbo la paka wa kawaida kisha akakimbia.....baada ya tukio hilo nilibadirisha ratiba ya kujisomea, nikawa naingia prepo saa 4 usiku na kutoka saa 10 alfajiri
2:Baada ya kumaliza O level nikazamia mgodini kusaka madini, kipindi hicho Kuna binti nilikua namtongoza lakini haeleweki, Muda mwingine hata kunisikiliza hataki wala kusimama na mm, hapo alikuwa darasa la saba(zamani binti wa la saba ni mkubwa tu). Katika harakati zangu za kusaka madini zikazidi kuwa ngumu madini hayapatikani, wenzangu wakashauri twende kwa mganga, kweli tulienda tukatengezwa haswa, sharti tulilopewa nikutotembea na mwanamke, tukagwa jioni na tulifika siku Hiyo Hiyo maana hapakua mbali sana, huwezi amin kesho yake asubuh sana ngoma 12 asubuh nasikia mlango unagongwa( hodi hodi nyingi) Kufungua ni yule binti alikua hataki hata kunisikiliza, akazama gheto, namuuliza Leo mbona huenda shule anajibu nimekuja kwako, kumbuka hapo tumepewa sharti la kutolala na mwanamke, kufupisha nilikula mzigo, Mashariti nikaharibu nakuambukizwa kaswende juu.
Ukienda kwa mganga kwaajili ya utajiri ama biashara, huwa wanakupa dawa za kuongeza mvuto pia, ambayo inawafanya wanawake kukupenda zaidi, ukikutana na wanawake 50 kwa siku, kisha ukawatongoza, basi wanawake 45 ama wote 50 watakukubali siku hiyo

Ndiyo maana masharti wanayotoa ni kutotakiwa kuwa karibu na wanawake, maana wanajua utajiri hauwezi kukaa kwa Mwanaume Malaya
 
Tukio la mstaafu kupeleka Pensheni yote kwa nyumba ndogo

Mwaka fulani, mstaafu mwenzangu mmoja aliyeitwa Mzee Masanja(Sio jina halisi) ambaye kimsingi aliwahi kustaafu miaka mitano (5) hivi kabla yangu, alikuwa amepokea pensheni yake kiasi cha kama shilingi milioni 103. Miaka ile mstaafu alikuwa akipokea fedha zake zote kwa mkupuo tofauti na sasa ambapo kwa mujibu wa sheria mpya ya kikokotoo, mstaafu analipwa asilimia 33 kwa mkupuo na baadaye kuanza kulipwa asilimia 67 iliyobaki kidogo kidogo kila mwezi kwa kupokea 1/3 ya mshahara wake hadi atakapofariki.

Huyu Mzee alikuwa mwenyeji wa Kijiji cha Kitongo katika Wilaya ya Ushetu huko Mkoani Shinyanga lakini alibahatika kustaafia Wilaya ya Kinondoni hapa Jijini DSM.

Mara baada ya kustaafu alidakwa na Dada mmoja wa Mjini aliyejulikana kwa jina la Juliana (sio jina halisi), Mzee akawa haambiliki, wala hasikii kuhusu huyu bidada. Ilifikia wakati alihama kabisa nyumbani kwake Mbezi kwa Msuguri, na kuhamia Kinondoni mtaa wa Msisiri ‘B’ kwa huyu Dada ambapo alikuwa amempangia nyumba ya vyumba viwili na sebule.

Mkewe ambaye tulikuwa tukifahamiana, alikuja kunilalamikia kuhusu kutelekezwa na mumewe Mzee Masanja huku akishindwa kuwahudumia kwa chakula wala kodi ambayo ilikuwa imebaki miezi 3 kuisha yeye na watoto wake wanne.

Mzee Masanja alikuwa ni rafiki yangu wa toka nitoke, kwahiyo kama marafiki tunajuana udhaifu wa kila mmoja, Mimi nilikuwa mnywaji lakini yeye alikuwa ni mpenda chini (isokeme hivyo), nakumbuka mwaka fulani tukiwa kwenye semina Mkoani Tanga, mara baada ya semina kuisha, badala ya kuanza safari saa 2 asubuhi kesho yake kurudi DSM, tulimsubiri hadi saa 8 mchana ili kusubiri nguo zake zikauke, baada ya mdada wa Kitanga kumlowekea ili asiondoke. Nakumbuka Mimi ndiyo nilienda kumkaripia yule binti na kumwambia azianike nguo za Mzee Masanja kabla sijampeleka kituo cha Polisi maana tulikuwa tumefikia hotel moja.

----------------------------

Kwahiyo alipokuja shemeji Mama Janeth kunilalamikia kuhusu kutelekezwa na Mzee Masanja, nikawa nawaza wapi pa kumpata, maana kazini alikuwa ameshastaafu miezi 2 nyuma, na bahati mbaya nilikuwa sijui wapi pa kuanzia kumtafuta. Miezi 7 nyuma niliwahi kugombana naye sana Mzee Masanja kwa nia ya kujaribu kumbadirisha mwenendo wake juu ya tabia yake ya wanawake, ukizingatia alikuwa amebakiza miezi 5 mbele ya kustaafu, imani ilinijia kwa kuona amebakiza miezi michache kustaafu halafu hakuwa amejenga nyumba ya kuishi iwe hapa DSM ama kule Kijijini kwao Kitongo. Kubwa zaidi hakuwa na biashara wala kitega uchumi chochote cha kumuingizia kipato akistaafu.

Baada ya kugombana naye, akaamua kupunguza urafiki na mimi, baadaye akakata urafiki kabisa.

Kazi ya kumtafuta ikaanza, pale ofisini kulikuwa na dereva mmoja ambaye alikuwa na taarifa za watumishi wote, utasema alikuwa spy. Kwahiyo nikampaga task ya kunitafutia taarifa za Mzee Masanja, akaniambia unamuulizia yule Mzee mrefu mstaafu anayeishi na yule binti mrembo Juliana?

Nikamwambia sijui kuhusu huyo Juliana, lakini Mzee mwenyewe ndiyo huyo huyo Masanja, akaniambia kwa sasa Mzee Masanja anaishi pika nipakue na Juliana. Juliana ni yule msichana anayetoka na Msanii mmoja wa bendi ya dansi inayotamba na wimbo wao maarufu wa “Jirani”

Baada ya siku 5 na Shemeji yangu, Mke wa Mzee Masanja, nilifanikiwa kuonana na mumewe Mzee Masanja, tukazungumza na kumsihi kuhusu kumtelekeza mkewe na watoto

Mzee Masanja, akanijibu kavu kabisa, akaniambia kama unampenda na kumjali huyo shemeji yako, nenda umwoe wewe na hao watoto wake wewe ndiyo uwe Baba yao!

Kwa kweli nilipandwa na hasira sana, nikajikuta nime mwasha vibao viwili vya mashavuni, tukafokeana pale na mazungumzo yetu yakakavunjika

Jumatatu nikapigiwa simu na huyo Juliana mwenyewe, alinitukana sana, akasema kama na wewe unataka uje nikupe utamu ninaompa Mzee Masanja ili nawewe utelekeze familia yako. Akasema yeye ni binti wa Pwani, na ana ujuzi wa kumteka mwanaume yeyote, ujuzi ambao alifundishwa tangu akiwa na miaka 7 na kwamba hivyo vitu adimu hata wanawake zetu hawatupi.

------------------

Kumbe Juliana alikuwa amesikia Mzee Masanja, anakaribia kupewa kiinua mgongo chake (pensheni) kwahiyo alitaka ikitoka hiyo pensheni ahakikishe anapewa yote yeye. Kwahiyo alihakikisha anamteka sawasawa Mzee Masanja.

Kwa mujibu wa yule dereva wetu Bwana Bakari (sio jina halisi), alisema Mzee Masanja alikuwa anawahadithia marafiki zake kila walipokuwa wanakutana kucheza bao, eti Juliana anampa vitu adimu ambavyo tangu kuzaliwa hakuwahi kuvipata.

Katika kumdadisi, ndiyo akawa anafunguka kwamba anabebwa mgongoni kupelekwa bafuni kabla hajaogeshwa maji ya hiriki na karafuu. Kingine akawa anawahadithia marafiki zake kwamba Juliana akiwa anamfanyia usafi wa kumnyoa mavuzi, alikuwa anamlaza kitandani kisha anachukua kisosi maalumu ambacho anachukua korodani za Mzee Masanja na kuziweka kwenye kisosi wakati wa kumsafisha kabla hajampaka mafuta ya mzeituni yaliyotoka kupashwa motoni.

Katika kumalizia hivyo vitu vyake anavyochanganywa na Juliana, ni pamoja kuimbiwa na Maiki, anasema mkewe kwenye ndoa yao ya miaka 24 waliyokaa pamoja, hajawahi kumuimbia na maiki, na kingine cha kuogopa ni kwamba huyo Juliana alikuwa ameanza kumpa ngono ile nyingine….nyie vijana wa miaka hii sijui mnaita nini…….

Mwezi Agosti,mwaka 47, pensheni ya Mzee Masanja ilitoka, akaipokea na yote akampelekea Juliana wake.

Kwa kuwa Juliana alikuwa mtoto wa mjini, alimshawishi Mzee Masanja kwamba anataka kufanya biashara ili wasitetereke kiuchumi, kwahiyo ampatie kiasi chote cha fedha.

Jioni kama ilivyo kawaida ya Mzee Masanja, kutoka na kwenda kucheza bao na Wazee wenzie, alipotoka, huku nyuma Juliana akachukua gari, beba vitu vyake vyote kuanzia kitanda,mapazia, godoro hadi vijiko na kuhama mtaa kabisa.

Mzee Masanja aliporudi akakuta nyumba imepigwa kufuli, kuuliza majirani wakamwambia kwamba Mkeo (Kwa maana ya Juliana) kasema mmepata nyumba nyingine kwahiyo hapa mnahama. Piga simu ya Juliana, saa ngapi asibadirishe laini, kwahiyo kila akipiga simu, anajibiwa simu haipatikani.

Kama mnavyofahamu, Wazee wengi tuna tatizo la Presha na Kisukari, Mzee Masanja Presha na kisukari vilipanda akajikuta ameanguka na kuzimia.

Kukimbizwa hospitali ya Sinza Palestina, akiwa njiani akafariki Dunia.

------------------

Mkewe Mrs Masanja, baada ya kushindwa kumudu gharama za maisha hapa mjini ikiwemo chakula na gharama za kodi pale kwa Msuguri, aliamua kurudi kijijini kwao Chololo huko Kondoa, Dodoma. Mtoto wao wa kwanza alifanikiwa kuhitimu shahada ya Elimu, mwaka 2020 na ameajiriwa shule moja ya sekondari ya binafsi Wilaya ya Kilosa.

-------------

Watu wanajifunza kupitia makosa, ninyi Wanaume wenzangu mnaotegemea kustaafu miaka 5, 10 ama 20 ijayo, fanyeni utaratibu kujiwekeza sasa kwaajili ya uzee wenu, lakini sio vibaya kama huna nyumba, pambaneni kujenga hata vyumba vitatu kwaajili ya familia.

Hakuna mke mzuri kuliko huyo uliyenaye nyumbani, Dunia ya sasa ni ya uwazi, kama kuna kitu unatamani kufanyiwa na mkeo, ongea naye kwa lugha nzuri mtajifunza kwa pamoja muhimu hakitwezi utu wake.

Siku hizi kuna wimbi kubwa la sisi Wanaume kutamani kukandwa miili (Massage) kila tukienda saluni, ongea na mkeo nyumbani akukande.

Siku hizi kuna tutorial videos nyingi huko YOUTUBE, mnaweza kuangalia na mkajifunza, si mnajua mke naye anahitaji kukandwa mwili eeh, ni kama wanaume tunavyohitaji kukandwa mwili nao wanahitaji vile vile.

Kuweni macho na akina Juliana, wapo wengi mtaani wakiwasubiri na pensheni zenu.
Mambo ya simu haipatikani ni miaka ya 90s mwisho na kuendelea. Mwaka 47 Tz hii kulikuwa hakuna mobile phone.
 
Mambo ya simu haipatikani ni miaka ya 90s mwisho na kuendelea. Mwaka 47 Tz hii kulikuwa hakuna mobile phone.
Hahaha...........ni tukio la miaka mingi, lakini likiwa na lengo la kuwatonya wastaafu wa miaka 5,10 ama 20 ijayo

Maana akina Juliana wanajuaa kunusa hela ilipo 😜
 
Hahaha...........ni tukio la miaka mingi, lakini likiwa na lengo la kuwatonya wastaafu wa miaka 5,10 ama 20 ijayo

Maana akina Juliana wanajuaa kunusa hela ilipo 😜
Yeah hio issue mpaka leo bado inawakumba wazee wenzetu.
 
Yeah hio issue mpaka leo bado inawakumba wazee wenzetu.
Mwaka juzi, kuna Mzee mmoja naye ilimkuta, alipokea pensheni yake ya kikokotoo cha asilimia 33 kama milioni 23 hivi

Alafu yote ilichukuliwa na akina Juliana, yule Mzee saivi ni kama amechanganyikiwa, maana hakuwa amejenga
 
Pole sana Mkuu, miaka ya zamani hayo mambo yalikuwa mengi sana vijijini, Mimi nimewahi kukutana na kisa cha namna hiyo pia.

Ilikuwa majira ya saa 7 usiku, nilikuwa natoka prepo kupiga msuli, wakati naelekea bwenini nilikutana na paka mkubwa na mrefu kama Simba, nilipomkazia macho na kumwangalia usoni, akabadilika na kurudi umbo la paka wa kawaida kisha akakimbia.....baada ya tukio hilo nilibadirisha ratiba ya kujisomea, nikawa naingia prepo saa 4 usiku na kutoka saa 10 alfajiri

Ukienda kwa mganga kwaajili ya utajiri ama biashara, huwa wanakupa dawa za kuongeza mvuto pia, ambayo inawafanya wanawake kukupenda zaidi, ukikutana na wanawake 50 kwa siku, kisha ukawatongoza, basi wanawake 45 ama wote 50 watakukubali siku hiyo

Ndiyo maana masharti wanayotoa ni kutotakiwa kuwa karibu na wanawake, maana wanajua utajiri hauwezi kukaa kwa Mwanaume Malaya
Yote uliyosema ni kweli aisee hii dunia ina mambo.
 
Back
Top Bottom