Mahatma Gandhi katika kitabu chake kiitwacho,
The Story of My Experiments With Truth akiwahi kuandika, ''The seeker after truth should be humbler than the dust. The world crushes the dust under its feet, but the seeker after truth should so humble himself that even the dust could crush him. Only then, and not till then, will he have a glimpse of truth''.
Being humble is one of the most important qualities of leadership!
Kuna viongozi wengi tu nchini ambao historia yao katika kulitumikia taifa haina madoa lakini kwa vile walikuwa wanyenyekevu kwa wananchi wao, hawakutaka kukubali kubebwa kama hawa viongozi wetu.
Nilipoziona hizi picha zilinipa maswali mengi sana kuhusu aina ya fikra za viongozi wetu wa kesho nchini. Sikufahamu pia kama kuna watanzania wengi ambao wana uwezo wa kuangalia, kuchuja na kutoa haki kulingana tabia, mwenendo na utendaji wa viongozi wetu.
Picha kama hizi nilikuwa ninaziona wakati wa wakoloni, wafalme wa kale na kwenye utawala wa Idd Amin nchini Uganda. Historia inatuambia viongozi wa aina hii walipotea kisiasa haraka sana!
Inadhihirisha Wananchi wapiga kura wengi hawakupendezwa na aina hii ya viongozi (Wenje & Lembeli) ndiyo maana wameamua
kwa haraka kuwastaafisha kisiasa kupitia sanduku la kura.
Kwa fikra hizi ndiyo maana Maandiko ya Mungu yalikemea na kusema, ''ajikwezae hushushwa na ajishushae hukwezwa."
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama, James Lembeli akiwa amebebwa kama walivyokuwa wanafanya enzi za wakoloni.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Ezekiel Wenje akiwa amebebwa kama alivyokuwa anafanya Idd Amin