Ni shida mno watu walikuwa wanatukana hovyo humu jamvini,wengine walidiriki kusema hata UKAWA wakimuweka Idd Amin awe mgombea wao watamchagua tu awe kiongozi mkuu wa nchi yetu,nikawaambia yaani Watanzania tumesahau ubaya aliowafanyia ndugu zetu wa Kagera enzi hizo Mkoa wa Ziwa Magharibi alipoivamia nchi yetu,kipindi hicho hakuna Tv ni RTD peke yake nchi nzima,wakati wa Taarifa ya Habari tunakimbilia kusikiliza redio 277,tukafundishwa kuchimba mahandaki na namna ya kukimbilia humo kujificha,lkn eti watu wakawa wanamtaka huyo Fashisti aje awe mtawala hapa kisa kuiondoa CCM madarakani haya sasa Watanzania wameamua nadhani wamezingatia usemi Zimwi likujualo...............