Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Niliota kifikra kuhusu Tanzania niitakayo baada ya vyama kusimamisha wagombea wake wa Udiwani, Ubunge na Urais.
Kwa kadri matokeo yanavyobandikwa kwenye vituo, ndoto yangu inazidi kutimia.
Niliomba kifikra Taifa lipate wabunge wengi wa upinzani ili wakaweze kufanya kazi zao kiufanisi bungeni. Hili ninaelekea kutimia. Hongera Watanzania.
Niliomba Taifa lipate Rais Magufuli ili akalitumikie taifa katika msingi wa Uadilifu,uchapakazi na Uzalendo wenye nguzo ya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Hili pia linaelekea kutimia. Hongera Watanzania.
Tanzania mpya inazaliwa ambayo mihimili ya nchi (Bunge, Dola na Mahakama) itafanya kazi zake kifanisi.
Mungu endelea kubariki Taifa letu.
Kwa matokeo haya na kwa wapenda taifa endelevu, hakuna aliyeshindwa bali Taifa limeshinda!
Taifa Kwanza, Vyama Baadaye.
Hukuwahi kuomba wapinzani washinde hata siku moja wewe ni mnafiki, ungekuwa uliomba wapinzani washinde tungeona hata ukiikemea serekali iliyoagiza magari 777 ya kuja kupiga wananchi watakaoikataa ccm. Leo hii bila aibu mnaagiza magari ya kupigia wananchi waliowakinai wakati hata kulipa wasimamizi wa uchaguzi hamuwezi, waalimu wamelalamika mpaka wamechoka lakini wapi!!? Kulikuwa na ugomvi gani mpaka muagize magari mengi hivyo wakati ni mwezi wa nne sasa kila siku ni mgao wa umeme?
Watu waliacha weledi wakawa wanapewa vyeo kwa kujipendekeza. Viongozi wengi wa taasisi za hapa nchini wamepata vyeo kwa kujipendekeza na sio uwezo mfano, viongozi wa jeshi la polisi, wakuu wa wilaya/mikoa, mawaziri nk. Matokeo yake taasisi hizo zimeshindwa kufanya kazi kwa kufuata sheria bali kuwafurahisha walioweka madarakani. Na bado ngoja matokeo rasmi yatoke ndio mtajua mlikuwa mnajidanganya kwa propaganda za kizee. Hebu rudia tena ule msemo mliojidanganya nao wa "kata tatu chopa tatu"