Matukio ng'amuzi kwa mwaka huu wa uchaguzi 2025.

Matukio ng'amuzi kwa mwaka huu wa uchaguzi 2025.

mtunzasiri

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2012
Posts
1,449
Reaction score
993
Tafakari,, Mwaka huu wa uchaguzi 2025 una migogoro mingi hatarishi kuliko miaka yote-
1). Kuna mgomo baridi ya kimichezo kutokucheza na wanaenda mbele wanatishia kuandamana, kati ya YANGA UPANDE MMOJA na bodi ya ligi, TFF kwa pamoja Kwa upande mwingine, ukiangalia utasema ni suala la michezo tuu tuwaachie TFF lakini katika historia inasemekana Yanga walihusika pakubwa katika kupigania uhuru nchini ikitambulika enzi za ukoloni haikuwahi kuwa rahisi kufanya harakati za kisiasa hadharani hivyo timu ya Yanga zikatumika kama njia ya wazalendo kukutana kwa mipango mingine, sasa ni mwaka wa uchaguzi. Tusisahau pia kulikuwa na marufuku ya kisiasa kwa miaka mitano nyuma hivyo raia wanaopenda siasa walihamishiwa hisia zao huko kuna siasa za mpira siku hizi.

2). Kuna kampeini ya mgomo usio rasmi kuhusu kususia uchaguzi kama hakutakuwa na sera mpya na sheria za uchaguzi kubadilishwa maarufu (No reform No election) , hii inashika kasi isiyotarajiwa na wengi mtandaoni na mitaani ikiungwa mkono na jamii nzima isipokuwa ccm na serikali wanasisitiza wameshafanya mabadiliko ya sheria za uchaguzi hivyo hukuna hoja ya msingi sana Swali hivi ikitokea raia wakagoma kweli kwenda kupiga kura hiyo serikali itapata uhalali gani kuongoza? Je vipi ikiwa vuguvugu hili likijumuika na lile la kwanza nini hatima yake?
3). Polisi na usalama wa raia kwa mtizamo wangu umejikita sana kufuatilia mambo ya siasa za vyama vingi kuliko makundi mengine kama michezo na dini, na kwa namna ya ajabu mwaka huu wa uchaguzi wameamua kushughulikia kufungia mpaka taasisi za dini na makanisa vipi kama haya yakaungana na kundi la kwanza na la pili mwaka wa uchaguzi huu AMANI YETU ITAHUBIRIWA WAPI?

TAFAKARI CHUKUA HATUA
HAKI HUINUA TAIFA. 📜
 
Back
Top Bottom