Kuanguka kwa majengo nchini Kenya mwaka 2026, hadi lini tutapoteza maisha?
Leo Tarehe 23 Oktoba 2026, macho ya Wakenya yanaelekezwa Eastleigh, Nairobi, baada ya jengo la ghorofa nyingi zaidi 10 lililokuwa kwenye ujenzi kuripotiwa kuanguka.
Tukio hili linaibua Maswali, Je, usalama wa majengo nchini Kenya unazingatiwa kwa kiwango kinachotakiwa au bora liende tuwe na majengo mengi ila hakuna ubora?
Kuanguka kwa jengo hilo kunaibua wasiwasi kuhusu usalama wa wafanyakazi wa ujenzi na wakazi wa maeneo hayo na wenye shughuli za kibiashara juu ya usalama wao kwani hofu ni kuwa huenda wamefukiwa na kifusi.
Taarifa za awali ni kuwa shughuli za uokoaji zinaendelea japo Idadi ya waliofariki au kujeruhiwa bado haijatangwa iwpo wapo waliofikwa na madhira hayo.
SOUTH C, NAIROBI
Mnamo Januari 2, 2026, jengo lililo kwenye ujenzi liliripotiwa kuanguka South C, na watu wawili wakapoteza maisha.
Kila tukio kama hili linatukumbusha kuwa nyuma ya takwimu kuna familia, ndoto na maisha yaliyokatizwa, kwa nini matukio haya yanajirudia rudia, ndio swali linalotakiwa kuwa kwenye vichwa vya wahusika wa ujenzi.
KAREN, NAIROBI
Januari 10 pia, jengo lililo kwenye ujenzi liliripotiwa kuanguka Karen. Taarifa ziliripoti vifo vya wafanyakazi wawili na majeruhi saba.
OGEMBO, KISII
8 Septemba 2026, jengo la ghorofa tano liliripotiwa kuanguka Ogembo.
Matukio ya aina hii yanahitaji uchunguzi wa kitaalamu ili kubaini kilichosababisha kuanguka
MAMBOLEO, KISUMU
21 Septemba 2026 pia, jengo liliripotiwa kuanguka Mamboleo, Kisumu, huku taarifa za awali zikieleza kuwa watu wanane walijeruhiwa.
Hivi Majengo yanakaguliwa kabla na wakati wa ujenzi kweli? Hali inatisha
Serikali za kaunti, National Construction Authority (NCA), wahandisi na wakandarasi wanapaswa kujitafakari.
Pia soma: Jengo la Ghorofa Laanguka Eastleigh, Watu Wadaiwa Kunaswa Kwenye Kifusi