Matukio ya kukumbukwa mwaka 2004

Matukio ya kukumbukwa mwaka 2004

Sio specific 2004 ila uvumi wa stori za uwepo wa popo bawa ziliniogopesha sana namkumbuka yule sheikh aliyekuwa na kipindi Channel Ten akitoa mbinu za kujilinda dhidi ya popobawa
Huy mwamba popobawa kama atarudi tena safari hii ajitahidi aje na wenzake.
Maana mademu wa siku hizi wanavyopenda kutelezeshwa atajua hajui
 
Huu uzi unahusu matukio yoyote yaliyotokea mwaka 2004, basi na wewe mwanajukwaa andika hapa tukio lolote lililotokea mwaka 2004.

Mimi nitaanza na tukio la shindano la kutafuta vipaji vya waimbaji mwaka 2004 lililotambulika km East Afrika Coca Cola Pop Stars Talent Search Competition, ili ni tukio lililohusisha kusaka vipaji vya waimbaji mbalimbali, nakumbuka kipindi hicho tulikua tunafuatilia kipindi mida ya jioni jioni kwenye Luninga (Televisheni) km nitakua sijasahau ilikua ni ITV, baadae mwisho wa shindano wakaibuka washindi watatu ambao ni Witness Mwaijage 'Witness' (Bad Gear), Langa Kileo 'Langa' (RIP) & Sarah Kaisi 'Shaa'.

Baada ya ushindi huo washindi hao wa Coca Cola Pop stars Talent Search Competition wakaunda kundi lililotambuliwa km 'Wakilisha' ikiwa ni muungano wa majina yao ya kisanii yaani Witness, Langa na Shaa, meneja wa kundi hilo alikua anaitwa Daniel Kiondo na wakaachia kibao chao cha kwanza kilichoitwa 'HOI'.

Baadae wakaachia kibao kingine cha pili kikali kilichokwenda kwa jina la 'Kiswanglish'. Baada ya hapo mwaka uliofuatia kundi hilo likafika tamati rasmi na kila mmoja akaanza kufanya kazi zake peke yake.

Shaa akaelekea zake Washington DC kuendelea na masomo. Huku Langa' yeye akaanza kuachia vibao vyake vikitanguliwa na kibao cha kwanza kilichoitwa 'Matawi ya Juu' kule 'Witness' akitoa kibao chake cha kwanza kilichoitwa 'Kichekesho' na pia kupita kwenye kolabo ya kushiriki kwenye kibao cha Fid Q kilichoitwa 'Zero'.

Baadae Witness na Langa waliungana wakaunda kundi lililoitwa 'Wakili' ambalo pia halikudumu muda mrefu sana.
miaka hiyo nakumbuka kampeni ya uchaguzi kuelekea 2005 Agustine lytonga mrema mzee wa jogoo alivyokimbiza, nakumbuka mitaa ya pale moshi mjini na relini coffe curing mzee alikuwa anabebwa kama vile watwana na waarabu kipindi cha wakoloni, dah ila maisha basi tu. 2004 na ndo nakwea mlima kilimanjaro hadi uhuru peak kwa mara ya kwanza kupitia marangu route
 
Hakika mimi nitakua napiga misele huu uzi utafika mbali sana maana hio 2004 kuna dogo anasoma uzi huu muda huu kipindi hicho yeye alikua ndio kwanza ana mwaka mmoja na bado hajamaliza kunyonya hapa anachoona ni maluweluwe tu memories zitaendelea kuishi
Mimi nisiwe muongo kwa kweli hiyo 2004 ndo Kwanza nilikuwa na miaka 8
 
Back
Top Bottom