Tatizo lako wewe hujitambui, ukiambiwa ukweli unaona unadharauliwa kitu ambacho hakina ukweli wowote. Na kwa taarifa yako hakuna anayekudharau ila watu wana haki ya kukwambia ukweli pale unapotetea mambo ambayo hayastahili kutetewa, badilika na kuanza kutafakari mambo kwa kina badala ya kukurupuka.
CC: Wapwa zangu Chakaza, MANI, Elli, zumbemkuu, Eli79
Mimi ni mtetezi mkubwa sana wa HOJA ninayoiamini, sio mtetezi wa watu!!
Nilikuwa najiuliza labda kuna aliye hack JF account ya Buchanan...hata hivyo sijapata jibu kwani huyu ni mtetezi mkubwa wa yule mpangaji wa magogoni.
Nibadilike ili nifikiri kama unavyofikiria wewe?
Hapana jamani, Buchanan is merely crying for help. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Ni kweli Clinton aliishambulia Iraq ila ni ulimbukeni kulihusisha swala la Iraq na Lewinski. Iraq ilishambuliwa 1993 na wakati huo Lewinski alikuwa bado mdogo sana akiwa shule ya msingi. Scandal ya Clinton na Lewinski ilikuja kuibuka miaka kadhaa baadaye katika awamu ya pili ya utawala wa Clinton mwaka 1998. Buchanan, karibu sana kwenye mwanga...kuishi muda mrefu gizani kunapofusha macho. Naomba wana JF wasikejeli hicho kitendo chako kwani kinahitaji ujasiri mkubwa, asante sana...taratibu tutafika.Clinton hujawah ishambuliwa Iraq..umetupotosha kwa nia njema!
Hapana jamani, Buchanan is merely crying for help. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Ni kweli Clinton aliishambulia Iraq ila ni ulimbukeni kulihusisha swala la Iraq na Lewinski. Iraq ilishambuliwa 1993 na wakati huo Lewinski alikuwa bado mdogo sana akiwa shule ya msingi. Scandal ya Clinton na Lewinski ilikuja kuibuka miaka kadhaa baadaye katika awamu ya pili ya utawala wa Clinton mwaka 1998. Buchanan, karibu sana kwenye mwanga...kuishi muda mrefu gizani kunapofusha macho. Naomba wana JF wasikejeli hicho kitendo chako kwani kinahitaji ujasiri mkubwa, asante sana...taratibu tutafika.
Umebadilika Sana mkuu au nawewe umetendewa Kama Manyerere Jackton ambaye alitumika kufanya hila ili kuufagilia njia mtandao Wa JK matokeo yake akapata shukrani ya punda?
Watu wenye maono ya kuijenga nchi huwa hawasubiri kuzawadiwa vyeo au vitu kwa sababu tu walishiriki kumsaidia fulani kwa hili au lile. Watu makini hupenda kuona wamemaliza kazi yao halali na kinachofuata ni kuhakikisha maudhui ya misimamo yao kwa waliyemwwamini yanatekelezwa. Kama kuna mtu anamsaidia mwingine kwa matarajio ya kuwa DC (kazi ya kuzuia maandamano ya wapinzani na mapokezi ya viongozi), huyo hana weledi. Maslahi ya nchi ni muhimu kuliko maslahi binafsi ya kusaka vyeo au fadhila.
Ndugu yangu Buchanan, nchi yoyote inayoendelea kwa kasi lazima ikumbwe na misuko suko. Kwa haya yanayoendelea Tanzania ni athari mojawapo ya maendeleo chanya ya nchi yetu
Umebadilika Sana mkuu au nawewe umetendewa Kama Manyerere Jackton ambaye alitumika kufanya hila ili kuufagilia njia mtandao Wa JK matokeo yake akapata shukrani ya punda?
Hapana jamani, Buchanan is merely crying for help. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Ni kweli Clinton aliishambulia Iraq ila ni ulimbukeni kulihusisha swala la Iraq na Lewinski. Iraq ilishambuliwa 1993 na wakati huo Lewinski alikuwa bado mdogo sana akiwa shule ya msingi. Scandal ya Clinton na Lewinski ilikuja kuibuka miaka kadhaa baadaye katika awamu ya pili ya utawala wa Clinton mwaka 1998. Buchanan, karibu sana kwenye mwanga...kuishi muda mrefu gizani kunapofusha macho. Naomba wana JF wasikejeli hicho kitendo chako kwani kinahitaji ujasiri mkubwa, asante sana...taratibu tutafika.
...Yote ni ukweli ila kama kawaida ya watz ni watu wepesi hivyo hawawezi na huwa hawataki conclusion ya jambo ndio maana mambo mengi ktk nchi hii yanaaza na kwendaaaaaaathen kimyaaaaa.Tatizo ni kuwa mengine ni ya hatari kweli kwa taifa mfano suala laa kuchinja imepewa panadol tu.....,ijumaa kuwa mapumziko,serikali 3,maazimio mbalimbali ya bunge,suala la ardhi,wahaamiaji haramu,ziwa nyasa..........,east africa na issue ya rwanda,yaani ni hatari kweli kweli.Rais ajaye ana kazi sana kwanza ya kuunganisha taifa...ni mharibifu....angalie unafiki wake hapa;anakwenda eti kuwasuluhisha Sudan kusini wakati yeye kwake haelewani na viongozi wenzake,uandikaji wa katiba hovyo,katiba ambayo itapingwa kuanzia sekunde ya 1 ya kupitishwa kwake.....je kazi ya Nyerere foundation ni nini?.wanahujumu mpaka taasisi ya baba wa taifa.Je huko ndio kumwezi baba wa taifa.Wakuu,
1. JK amekabidhiwa nchi ikiwa na amani kabisa, lakini Mheshimiwa huyu amekuwa ni mtu anayejificha kwenye matukio mbali mbali UDHAIFU wake usijulikane!
2. Alianza na Richmond ambayo ilitusumbua sana, hatimaye alivunja Baraza zima la Mawaziri, mambo yakatulia kidogo!
3. Hatujakaa vizuri tukasikia "Zanzibar sio nchi!" Hili nalo lilitusumbua sana hadi kupelekea Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 ili kuitambua Zanzibar kama "nchi!" Baadaye mambo yakatulia!
4. Tulishuhudia mgomo wa Madaktari na kuteswa kwa ULIMBOKA, lilisumbua sana akili za watu. Matukio mengine yaliyofanana na hayo: Kuuawa kwa wafuasi wa CHADEMA, waandishi wa Habari, Gesi ya Mtwara, nk. Yote hayo yalitufanya tu-concentrate na matukio menyewe zaidi kuliko ku-concentrate na mambo ya maendeleo!
5. Hili la ESCROW sihitaji hata kulielezea maana bado linaendelea kusumbuma akili za watu.
6. Hili la Katiba Mpya nalo limeleta kizaa zaa, ni kama vile limeletwa makusudi ili tugangamane nalo ili Mzee amalize ungwe yake ya Awamu ya Nne!
7. Hili la Mahakama ya Kadhi ndio funga kazi. JK anajua kabisa litatugawanya na litagawanya nchi vipande vipande! Kwa kuwa yeye ni mzee wa matukio yanayo-draw attention kwenye tukio lenyewe badala ya yeye mwenyewe basi tutakomaa nalo wakati yeye anaendelea kumalizia safari zake kwenye nchi ambazo alikuwa bado hajazitembelea! Hana shida na mshikamano na mustakabali wa nchi hii!
8. Bill Clinton alipoona issue yake na Monica Lewinsky imepamba moto, alihamisha attention kwa kuishambulia Iraq. JK naye akishaona kwamba kuna tukio ambalo linamlenga yeye na Serikali yake moja kwa moja analeta tukio jingine. Hili la Katiba lilifunikwa na ESCROW, hili tukio la ESCROW halijaisha tumeshaletewa mambo ya Mahakama za Kadhi.
Tunakorogwa sana kwa kweli! Nikimtafakari JK nashindwa kummaliza! Hapa sijagusia Mgogoro wa Malawi na Rwanda na baadaye na Kenya, Rwanda na Uganda kwa umoja wao! Yaani ni tatizo juu ya tatizo!
Karibuni kwa mjadala zaidi!!