Matukio yanayojiri Siku ya Uhuru wa Tanganyika Disemba 9, 2025: Hali yaonekana kuwa shwari maeneo mengi nchini

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Maandamano yatafanikiwa kumuondoa Rais Samia na kufanywa wauaji waajibishwe safari hii?

Siku yenyewe ndio imefika, ikiwa ni miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika, lakini upande mwingine tunasema bado hatujapata uhuru. Bado tumefungwa na minyororo ileile iloyotufunga wakati na wa ukoloni na sasa zaidi, Watanzania wenzetu ndio wamekuwa wamesi wetu.

Kwa upande mwingine hii inakuwa siku ya kwanza ya kupata 'uhuru wa kweli' kwa kuweka misingi ya Haki, Utawala wa Sheria na kutokomeza matukio yote ya utekaji, ukatili wa polisi na matukio mengine yanayokiuka haki za binadamu.

Wananchi wamepanga kufanikisha hilo kwa kufanya maandamano ya amani na kuhakikisha matakwa yao yote ikiwemo Rais Samia kujiuzulu yanafanikiwa.

Je, hilo litafanikiwa au kwa mara nyingine vyombo vya ulinzi vitamaliza Watanzania kwa risasi?

Wacha tuone hali itakavokuwa, ukipata update popote utakapokuwa umetoka weka hapa ili kila mtu ajue kinachotokea.

=====
Saa nne asubuhi
Hali imeendelea kuwa shwari katika maeneo yote nchini, huku barabara zikiwa nyeupe kabisa ikionyesha watu wametii agizo la serikali mpaka sasa.

Usafiri unatajwa kuwa wa shida, na watu hasa wagonjwa kupata changamoto ya kufika hospitalini.

Polisi wanaendelea na ukaguzi mtaani, wakikagua vitambulisho vya watu na kuwauliza wanapoelekea ili kuimarisha usalama.

Saa sita mchana
Bado hali inaonekana kuwa shwari katika maeneo mengi nchini, huku kukiwa na teteesi huku na kule kuwa wanananchi wamejitokeza barabarani kuandamana kwa amani wakiwa na mabango.

Saa kumi na mbili jioni
Vyombo vya Ulinzi bado vimetenda barabarani, kukiwa na vizuizi kila baada ya hatua chache kuhakikisha hakuna maandamano (vurugu kama asemavyo Gerson Msigwa, dr. Mwigulu Nchemba na mama yao). Miji imeendelea kuwa tulivu kwa siku nzima, huku wafanyabiashara wakilia hakuna wateja.
 
Maandamano yatafanikiwa kumuondoa Rais Samia na kufanywa wauaji waajibishwe safari hii?

Siku yenyewe ndio imefika, ikiwa ni miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika, lakini upande mwingine tunasema bado hatujapata uhuru. Bado tumefungwa na minyororo ileile iloyotufunga wakati na wa ukoloni na sasa zaidi, Watanzania wenzetu ndio wamekuwa wamesi wetu.

Kwa upande mwingine hii inakuwa siku ya kwanza ya kupata 'uhuru wa kweli' kwa kuweka misingi ya Haki, Utawala wa Sheria na kutokomeza matukio yote ya utekaji, ukatili wa polisi na matukio mengine yanayokiuka haki za binadamu.

Wananchi wamepanga kufanikisha hilo kwa kufanya maandamano ya amani na kuhakikisha matakwa yao yote ikiwemo Rais Samia kujiuzulu yanafanikiwa.

Je, hilo litafanikiwa au kwa mara nyingine vyombo vya ulinzi vitamaliza Watanzania kwa risasi?

Wacha tuone hali itakavokuwa, ukipata update popote utakapokuwa umetoka weka hapa ili kila mtu ajue kinachotokea.
Hamna sisimizi ataandamana
 
Wananchi wamepanga kufanikisha hilo kwa kufanya maandamano ya amani na kuhakikisha matakwa yao yote ikiwemo Rais Samia kujiuzulu yanafanikiwa.
Sina hakika na hili.

Samia Suluhu Hassan hawezi kuachia madaraka kwa sababu kuwepo kwa maandamano ya AMANI!

Hapana, hili haliwezekani.

Sana sana, ataacha maandamano yawepo na yahitimishwe kwa amani; watu waende nyumbani, na kesho yake ajitokeze na ulaghai ule ule wa "AMANI". Hali hiyo itampa fursa nzuri ya kuendelea kutawala; huku akiendeleza sarakasi zake za "maridhiano".

Hapo atakuwa amemaliza kazi kwa kuwasahaulisha waTanzania uovu mkubwa aliowafanyia katika miaka hii minne.

HAPANA. Maandamano hayaweze kuwa na lengo la AMANI bila ya Samia kuondoka madarakani.
Hiyo ndiyo 'bottom line'. ya maana ya maandamano.
 
Kwa ulinzi uliopo mtaani hakuna wa kuandamana hapa natoka lindo kila mtaa ni ulinzi
Kila mtaa?, wapi huko?. Kwa uzoefu wa 29 october nilijiridhisha kuwa askari ni wachache kudhibiti watu wengi. Vijana waliowaweka Bize kwa siku 3 hawakuwa wengi, ni vikundi vidogovidogo vya vijana wasiofika hata 50.. imagine kama watajitokeza wengi kwenye makundi ya 200-500 sehemu mbalimbali, obviously mtalemewa.
Anaye jitahidi kuepusha maandamanao kutokea yupo realistic zaidi ya yule canayelenga kupambana na waandamanaji.
 
Dar wakijitokeza hata watu 600,000 tu kwisha habari.

Tanzania nzima hakuna idadi hiyo ya askari.
 
KWA WALE WA KAHAMA

KUNA KAMATA KAMATA YA BODABODA AU YEYOTE ALIYE MAENEO YA VIJIWE VYA BODABODA

HAWA WATU WAMECHANGANYIKIWA NA DESEMBA 09 NA WANAFANYA VITUKO

HABARI NJEMA: TANZANIA MPYA IMESHAKUJA NA HAKUNA WA KUIZUIA KWA NAMNA YOYOTE ILE
 
Back
Top Bottom