Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Watu wanashindwa kutambua kuwa Marekani ilishaachana na sera za kujenga mabarabara na shule, ajenda yao kuu ni kuwa na nguvu Duniani, kuitawala Dunia, kuiweka Dunia kiganjani.
Ulaya yote hakuna anayekoroma pale ambapo Marekani anatoa maelekezo yake kuhusu Dunia, zaidi ya kuwa watu wa Ulaya ni vibaraka wa Mmarekani.
Chochote Marekani inachokifanya Duniani sio wazo la Rais peke yake, bali ni mpango wa muda mrefu uliosimikwa tangu enzi na enzi. Kila Rais anayeingia ni kufuata mipango ya muda mrefu aliyoikuta katika nchi.
Obama aliingia Rais Bush akamsaka Saddam Hussein na kumuangamiza ila hakufanikiwa kumkamata Gaidi na moja wa Dunia Osama Bin Laden, akaingia Obama akaakikisha ajenda hizo anazifuata. Obama akaakikisha Osama anatafutwa kila chocho na kuwawaa jambo alililofanikisha, Obama akaangalia tena nani ni tishio kwa Marekani akamuona Gaddaffi, basi Gadaffi nae akasakwa na kuuliwa. Marekani akawa kwa kiasi fulani kafanikiwa kuiweka Dunia katika utulivu wa mikono yake, kwa sababu wale walioonekana kuwa tishio kwake kawatuliza.
Licha ya Marekani kuwa katika hatua za kutaka kuituliza Urusi, lakini Urusi haina madhara ya moja kwa moja kwa Mmarekani. Urusi sio tishio la moja kwa moja na hakuna viashiria vya ugaidi kutoka kwa Urusi kwenda kwa Mmarekani.
Alivyoingia Trump aliendeleza ubabe huo huo, na badae Joe Biden nae akaja, na kisha Trump kurejea.
Sasa hivi wamarekani wanachokifanya ni kuzituliza Nchi zozote zinazoleta ubishi kwa kuwagombanisha na majirani zake. Ukraine na Urusi vita yao, Ukraine kutumika kama chambo tu. Ukraine baada ya kujazwa kichwa akajaa badala ya kushituka kuwa anatumiwa kumdhoofisha Mrusi. Marekani alichokifanya ni kumrudisha nyuma Mrusi kwenye kila kitu ikiwemo uchumi kama tunavyojua athari za vita.
Kwa pale mashariki ya kati kuna mbishi mmoja anaitwa Iran, yeye shughuli yake kakabidhiwa Muisrael. Israel pale Middle East ni kama kiranja aliyepewa mamlaka ya kunyamazisha wanafunzi. Mtu yoyote akibweka hapo uarabuni basi anachezea konzi kutoka kwa Muisrael huku Marekani akiwa kama anachungulia nani anafanywa nini, na akiona Israel kama anapelekewa moto basi Marekani utafuta namna ya kutuliza ugomvi.
Kwa upande wa China, Mchina yeye kakabidhiwa nchi kama Japan, Ufilipino na vilevile Mmarekani anaitumia Nchi ya Taiwani kuivuruga China... mpaka leo China hataki kuiachia Taiwan uhuru. Japan na Ufilipino ni nchi zinazofanya China ikae macho pale Asia.
Tukija pale Korea Kaskazini kwa kiduku, kiduku yeye kakabidhiwa Korea Kusini... yani kila mara kiduku akifurukuta basi Wakorea kusini wako nae, hizi ni nchi mbili jirani zinazochukiana kufa.
Pale Pakistan, show ya Pakistan kakabidhiwa Mhindi.... Pakistan akileta ukuda, basi Mhindi yuko nae
Afrika huku Marekani ajaweka sana nguvu, japo mfano kwa hapa Afrika Mashariki, Mkenya ndio kibaraka namba moja wa Mmarekani. Na kuna eneo maalumu ambalo ni base ya majeshi ya Marekani hapo Kenya. Majeshi haya ya Marekani nchini Kenya yapo kwa ajili ya kutuliza nchi zinazoleta ushubwada hususani kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki. Kuna kipindi Somalia aliwavuruga sana wamarekani kwenye utekaji wa ndege na meli za Mmarekani. Mwamba akana isiwe tabu ngoja nikuletee vijana ukae nao hapo hili somalia akileta ujinga basi iwe rahisi kula kichapo.
Hata Tanzania kama italeta Soo kwa Mmarekani basi Mkenya anaweza kutumiwa kuwa fimbo kwetu, na tukawa tunazichapa kila mara.
Kwa kifupi Marekani akiona Nchi fulani inataka kumzingua basi anatafuta jirani yako ambae hampendani au mna vita nae baridi basi anaweka kambi hapo mixture majeshi. Hizi ni ajenda zao za muda mrefu.