HAYA JAMANI TUSHINDWE WENYEWE KUPUNGUZA UZITO ILI UENDANE NA KIMO/UREFU NA HATIMAYE
BMI ZETU YAANI BODY MAX INDEX YETU IWE VIZURI
kupunguza unene ni lazima ujinyime kula ili uingize kalori kidogo lakini ufanye sana kazi au mazoezi ili utoe kalori nyingi mwilini. Baadhi ya watu wamesema kuwa wanajinyima kula lakini hawapungui. Kujinyima kula peke yake hakutoshi kama hufanyi kazi au mazoezi yoyote ya kutoa kalori nyingi kuliko unazoziingiza mwilini mwako. ASALI KATIKA KUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE Baada ya kuzingatia kanuni hiyo, hatua inayofuata ni matumizi ya asali kwa mpangilio maalum unaoweza kukusaidia kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka, wakati ukifanya mzoezi na kujinyima kula. Matumizi ya asali ni rahisi sana.
Kwanza kabisa hakikisha unapata asali halisi mbichi na siyo asali feki. Mjini kuna baadhi ya watu hutengeneza vitu mfano wa asali, matumizi ya asali hiyo hayawezi kukusaidia zaidi ya kukuletea matatizo mengine ya kiafya. Kuna kampuni na maduka (kama super markets) zinazouza asali halisi, nunua asali mbichi kutoka sehemu inayoaminika. Kula vijiko viwili (vya chai) vya asali kila siku wakati wa kwenda kulala. Katika muda wa saa nne za mwanzo za usingizi, asali itayeyusha mafuta (fat) mengi mwilini sawa na kufanya mazoezi makali. Mwanzilishi wa dayati hii ni Mike McInnes ambaye yeye ni raia wa Scottland na kitaaluma ni Mfamasia. Mtaalamu huyu aligundua kwamba wanariadha ambao hula matunda yenye virutubisho vingi vya fructose (kama vile matunda yaliyokaushwa na asali) hupunguza mafuta mengi mwilini na huwa na stamina nyingi.
Ili kufaidi vizuri manufaa ya asali katika kukusaidia kupunguza unene na mwili kuupa nguvu, ni vizuri ukatumia asali hiyo kama ilivyoelezwa hapo juu huku ukifanya mazoezi ya viungo, angalau mara tatu kwa wiki. Ni lazima ieleweke kwamba vitu vitatu lazima vifanyike kwa pamoja ili kupunguza unene kama unavyokusudia. Kitu cha kwanza ni kula vyakula sahihi na kwa kiasi kidogo, pili kula asali halisi na mbichi kila siku kabla ya kulala na tatu kufanya mazoezi au kazi nzito ili kutoa kalori mwilini. Umuhimu wa asali hapa ni ule uwezo wake wa kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka ukiwa umelala na wakati huo huo kuupa mwili stamina.
ASALI NA MDALASINI Mchanganyiko mwingine ambao umeelezwa kusaidia sana kupunguza uzito, ni asali na unga wa mdalasini. Mchanganyiko huu ni kama kinywaji ambapo utatakiwa kuchanganya asali, abdalasini na maji moto kisha kunywa mara mbili kwa siku. Ili kupata mchangayiko unaotakiwa, chukua nusu kijiko cha unga wa adbalasini (kijiko kidogo cha chai) kijiko kimoja cha asali (saizi ya kijiko cha chai) na kikombe kimoja cha maji yaliyochemka. Anza kuchanganya maji moto na unga wa abdalasini, koroga hadi uchanganyike vizuri kisha funika na uache muda wa nusu saa ili maji yapoe. Baada ya maji kupoa, weka asali yako kijiko kimoja kisha koroga tena hadi mchangayiko wako uwe kama kinywaji.
MDALASINI NA ASALI
Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee.
Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida.
Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora.
Kama ifuatayo:
1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}.
Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.
Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.
Katika tafiti iliyofanyika hivi karibuni na chuo kikuu kimoja huko Copenhagen, madaktari waliwapa wagonjwa 200, {syrup} mchanganyiko wa kijiko kimoja *cha chai* cha asali na kimoja cha mdalasini kila asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Asilimia 73% yao waliripoti nafuu kubwa ya maumivu yao na ongezeko katika kufanya shughuli kama kujongea na kutembea vyema.
2. kukatika kwa nywele {HAIR LOSS}
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.
3. Ukungu wa miguuni {FUNGUS}
Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Shida yako itakwisha kwenye kipindi cha wiki moja.
4. Maamhukizo kwenye kihofu cha mkojo {BLADDER INFECTION}
Bilauri ya maji vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili {vya chai} vya mdalasini na kijiko kimoja {cha chai} cha asali huondoa bacteria kwenye kibofu. Unaweza ukatumia juisi ya cranberry badala ya maji ikiwa ambukizo la kibofu linakuwa sugu.
5. Maumivu ya jino {TOOTHACHE}.
Changanya sehemu tano za asali, na sehemu moja ya mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.
Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka.
6. Vidonda vitokanavyo kwa mgonjwa kulala kwa muda mrefu {CANKER
SORES}.
Saladi ya kupaka vidonda iliyochanganywa na asali pamoja na mdalasini kwenye chai ya raspberry
nyekundu ni dawa nzuri ya kuondoa maumivu makali ya canker sores.