Matumizi na Faida za Asali katika afya ya binadamu

Matumizi na Faida za Asali katika afya ya binadamu

Mwenye ufahamu naomba msaada ni kweli Abdalasin almaarufu Mdalasini ukichanganywa na asali unatibu vidonda vya tumbo(ulcers)

kuna mdau mmoja amenieleza mchanganyiko huo ni dawa ilihali hapo awali nilikuwa nikifahamu Mdalasini ni kwa kupunguza au kuondoa Kitambi kwa maana inayeyusha mafuta

Kaka yangu ameanzwa na tatizo la ulcers kwenye utumbo mwembamba na yupo tayari kutumia dawa ya kienyeji au herbs tuu
Dawa ya vidonda vya tumbo Mfahamishe huyo kaka yako anayeumwa na Vidonda vya Tumbo atumie Dawa ya Hii ya Kienyeji Akiamka Asubuhi kabla ya kula kitu akojowe mkojo wake mwenyewe kwa kipimo cha Glasi moja awe anakunywa mkojo wake kila siku Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa Siku Saba kisha Aende kupima hivyo Vidonda vya Tumbo Vitapona na kukauka kabisa Mwambie ajaribu kutumia hiyo Dawa itamsaidia Sana.
 
fatwoman.jpg
Karibuni tena katika sehemu ya pili ya makala yetu ya leo kuhusu kupunguza unene, mada ambayo imeonekana kuvuta hisia za wasomaji wengi. Tatizo la unene limekuwa sugu. Kila mmoja anajaribu kutafuta suluhisho la tatizo hilo.Wiki iliyopita nilianza kuelezea uzito anaopaswa kuwa nao mtu kulingana na urefu wake. Kwa kuzingatia maelezo yale, sina shaka sasa umeshajua unatakiwa kupunguza kilo ngapi.Ingawa kuna baadhi ya wasomaji wametaka kujua jinsi ya kuongeza uzito, lakini kwa leo hatutaweza kuzungumzia hilo, tutaandaa makala yake siku nyingine, kwa sababu ni vitu viwili ambavyo vinahitaji kuongelewa kwa upana.KANUNI ZA KUPUNGUZA UZITOKanuni ya kwanza ya kupunguza uzito inatueleza kuwa ili mtu upunguze uzito, unahitaji kutoa kalori nyingi mwilini na kuingiza kalori kidogo (Less Calories In + More Calories Out= Weight Loss). Kwa lugha nyepesi, unapokula chakula chochote unaingiza kalori mwilini na unapofanya mazoezi au kazi yoyote unatoa kalori mwilini.Hivyo kupunguza unene ni lazima ujinyime kula ili uingize kalori kidogo lakini ufanye sana kazi au mazoezi ili utoe kalori nyingi mwilini. Baadhi ya watu wamesema kuwa wanajinyima kula lakini hawapungui. Kujinyima kula peke yake hakutoshi kama hufanyi kazi au mazoezi yoyote ya kutoa kalori nyingi kuliko unazoziingiza mwilini mwako.ASALI KATIKA KUSAIDIA KUPUNGUZA UNENEBaada ya kuzingatia kanuni hiyo, hatua inayofuata ni matumizi ya asali kwa mpangilio maalum unaoweza kukusaidia kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka, wakati ukifanya mzoezi na kujinyima kula.Matumizi ya asali ni rahisi sana. Kwanza kabisa hakikisha unapata asali halisi mbichi na siyo asali feki. Mjini kuna baadhi ya watu hutengeneza vitu mfano wa asali, matumizi ya asali hiyo hayawezi kukusaidia zaidi ya kukuletea matatizo mengine ya kiafya.Kuna kampuni na maduka (kama super markets) zinazouza asali halisi, nunua asali mbichi kutoka sehemu inayoaminika. Kula vijiko viwili (vya chai) vya asali kila siku wakati wa kwenda kulala. Katika muda wa saa nne za mwanzo za usingizi, asali itayeyusha mafuta (fat) mengi mwilini sawa na kufanya mazoezi makali.Mwanzilishi wa dayati hii ni Mike McInnes ambaye yeye ni raia wa Scottland na kitaaluma ni Mfamasia. Mtaalamu huyu aligundua kwamba wanariadha ambao hula matunda yenye virutubisho vingi vya ‘fructose’ (kama vile matunda yaliyokaushwa na asali) hupunguza mafuta mengi mwilini na huwa na stamina nyingi.Ili kufaidi vizuri manufaa ya asali katika kukusaidia kupunguza unene na mwili kuupa nguvu, ni vizuri ukatumia asali hiyo kama ilivyoelezwa hapo juu huku ukifanya mazoezi ya viungo, angalau mara tatu kwa wiki.Ni lazima ieleweke kwamba vitu vitatu lazima vifanyike kwa pamoja ili kupunguza unene kama unavyokusudia. Kitu cha kwanza ni kula vyakula sahihi na kwa kiasi kidogo, pili kula asali halisi na mbichi kila siku kabla ya kulala na tatu kufanya mazoezi au kazi nzito ili kutoa kalori mwilini. Umuhimu wa asali hapa ni ule uwezo wake wa kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka ukiwa umelala na wakati huo huo kuupa mwili stamina.ASALI NA MDALASINIMchanganyiko mwingine ambao umeelezwa kusaidia sana kupunguza uzito, ni asali na unga wa mdalasini. Mchanganyiko huu ni kama kinywaji ambapo utatakiwa kuchanganya asali, abdalasini na maji moto kisha kunywa mara mbili kwa siku.Ili kupata mchangayiko unaotakiwa, chukua nusu kijiko cha unga wa adbalasini (kijiko kidogo cha chai) kijiko kimoja cha asali (saizi ya kijiko cha chai) na kikombe kimoja cha maji yaliyochemka.Anza kuchanganya maji moto na unga wa abdalasini, koroga hadi uchanganyike vizuri kisha funika na uache muda wa nusu saa ili maji yapoe. Baada ya maji kupoa, weka asali yako kijiko kimoja kisha koroga tena hadi mchangayiko wako uwe kama kinywaji.
 
Ungetuwekea na sehemu zilizotangulia kwa pamoja ingesaidia sana hasa kwa sie ambao hatukuweza kuzisoma. Otherwise, thank you for all your efforts on these matters.
 
Ungetuwekea na sehemu zilizotangulia kwa pamoja ingesaidia sana hasa kwa sie ambao hatukuweza kuzisoma. Otherwise, thank you for all your efforts on these matters.

MDALASINI NA ASALI
Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee.
Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida.

Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora.

Kama ifuatayo:

1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}.

Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.

Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.

Katika tafiti iliyofanyika hivi karibuni na chuo kikuu kimoja huko Copenhagen, madaktari waliwapa wagonjwa 200, {syrup} mchanganyiko wa kijiko kimoja *cha chai* cha asali na kimoja cha mdalasini kila asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Asilimia 73% yao waliripoti nafuu kubwa ya maumivu yao na ongezeko katika kufanya shughuli kama kujongea na kutembea vyema.

2. kukatika kwa nywele {HAIR LOSS}
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

3. Ukungu wa miguuni {FUNGUS}
Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Shida yako itakwisha kwenye kipindi cha wiki moja.

4. Maamhukizo kwenye kihofu cha mkojo {BLADDER INFECTION}
Bilauri ya maji vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili {vya chai} vya mdalasini na kijiko kimoja {cha chai} cha asali huondoa bacteria kwenye kibofu. Unaweza ukatumia juisi ya cranberry badala ya maji ikiwa ambukizo la kibofu linakuwa sugu.

5. Maumivu ya jino {TOOTHACHE}.
Changanya sehemu tano za asali, na sehemu moja ya mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.
Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka.

6. Vidonda vitokanavyo kwa mgonjwa kulala kwa muda mrefu {CANKER
SORES}.

Saladi ya kupaka vidonda iliyochanganywa na asali pamoja na mdalasini kwenye chai ya raspberry
nyekundu ni dawa nzuri ya kuondoa maumivu makali ya canker sores.
 
[h=2]Dawa ya kupunguza mtu unene wa mwili[/h]
Maziwa ya mgando (Mtindi) ni ‘dawa' kupunguza unene
UTAFITI mpya umegundua kuwa, bakteria wanaopatikana katika maziwa ya mgando, mtindi na uji uliochacha vinaweza kufanya kazi mara mbili zaidi ya inayofanywa na vituo vya mazoezi (gym).

Matokeo ya utafiti huo yamekuja wakati mamilioni ya Watanzania wakihangaika kutafuta dawa na kufanya mazoezi ya aina mbalimbali ili kupunguza unene na uzito wa miili yao.

Utafiti huo uliotolewa hivi karibuni unaonyesha kuwa, bakteria rafiki, aitwaye ‘lactobacillus' anayepatikana katika maziwa ya mtindi na vitu vingine vilivyochacha anao uwezo wa kupunguza unene na uzito kupita kiasi (obesity) na huzalisha kinga ya kuyeyusha mafuta ya ziada mwilini.

Dk David Mwaniki, Mwanasayansi kutoka Taasisi ya Utafiti ya nchini Kenya, alisema kuwa tangu mwaka uliopita wa 2010, wanasayansi wamejitahidi kuonyesha jinsi bakteria hao wanavyoweza kufanya kazi ya kumeng'enya mafuta katika mwili wa binadamu.

"Ninaamini kuwa, hii ni sehemu ya utafiti ambayo italeta mapinduzi katika kudhibiti fetma (obesity), vilevile jinsi virutubisho vyake vinavyofanya kazi nyingine za ziada," alisema Mwaniki, ambaye taasisi yake imeonyesha hamasa ya kufanya utafiti kuhusu aina hiyo ya bakteria.

Wanasayansi hao walisema kuwa, watu wanaotoka katika jamii ambazo maziwa ya mtindi au uji ni sehemu ya mlo wao huwa wembamba kwa miili yao kutokana na aina hiyo ya bakteria.

"Wale wanaotumia maziwa ya mgando mara kwa mara au kwa muda mrefu wako katika nafasi ya kuwa na miili isiyo na mafuta pamoja na kupunguza kasi ya kushambuliwa na magonjwa yanayosababishwa na viumbe mbalimbali," alisema Mwaniki.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Tiba (NIMR), Dk Charles Massaga alisema, hana taarifa rasmi kuhusu utafiti huo, lakini akasema anakusudia kufuatilia kwa karibu ili ikiwezekana jopo la watafiti wa hapa nchini nao wachunguze kwa undani kama kweli maziwa ya mtindi yana uwezo huo.

"Kwa sasa sina taarifa kama kweli, maziwa ya mtindi yana uwezo wa kupunguza mafuta mwilini kama mnavyodai, lakini kwa kuwa habari kama hizo ni za msingi kwa watafiti kama sisi, hatuna budi kuzifanyia kazi kuanzia sasa,' alisema Dk Massaga.

Dk Massaga alisema kama bakteria hao wanaopatikana katika maziwa ya mtindi wana uwezo wa kufanya kazi kama zilivyotajwa na wanasayansi hao itakuwa ni moja kati ya tiba nyepesi na zisizo na gharama kubwa.

"Kama kweli bakteria wanaoishi katika maziwa ya mtindi wana uwezo wa kupunguza uzito, kuzuia maambukizi mbalimbali, wakati huo huo bado ikawa ni sehemu ya lishe tena ipatikanayo kwa urahisi basi itakuwa ni moja ya tiba za gharama nafuu na za muhimu," alisema.

Dk Massaga aliongeza kwa kusema, kama nchi za Afrika zimeweza kuwa na wanasayansi wenye uwezo mkubwa kiasi hicho basi Afrika inatarajiwa kuwa tishio katika wakati huu ambapo sayansi na teknolojia ndiyo msingi wa kila kitu.

Hata hivyo, utafiti mwingine kama huo uliofanywa hivi karibuni na Profesa Jeremy Nicholson kutoka Chuo Kikuu cha Imperial nchini Uingereza unaonyesha kwamba, bakteria aina ya lactobacillus wana uwezo wa kupunguza kiasi cha mafuta kilichonyonywa na mwili, hivyo kuondoa uwezekano wa kupata fetma au unene kupindukia.

Kwa mujibu wa profesa huyo, bakteria hao muhimu huweza pia kuweka makazi katika uke na utumbo, kisha kuteketeza wadudu waharibifu wanaojulikana kisayansi kama ‘probiotics'.

Probiotics ni viumbe hai wanaosaidia kuimarisha mmneng'enyo wa chakula, kudhibiti vijidudu vya maradhi katika utumbo mpana, kuzuia ukuaji wa bakteria wenye madhara na kuongeza nguvu ya kinga ya mwili.

Utafiti huo unaeleza kuwa bakteria hao, wana uwezo wa kuimarisha kinga ya mwili na kumpa mwanadamu maisha yenye afya.

Dk Mwaniki alisema utafiti wa Profesa Nicholson na wenzake umeongeza vipengele muhimu katika vimelea hivyo vya probiotics ambavyo ni kuimarisha afya kwa watoto na watu wengine, hasa katika ugonjwa hatari wa Ukimwi.

Alisema bakteria hao (lactobacillus) wana uwezo mara mbili wa kuzuia kuharisha na kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa watoto.

"Tumegundua kuwa, lactobacillus wana uwezo wa kubadilisha mimea midogomidogo katika utumbo na kuwafanya bakteria wanaosababisha madhara kwa watoto hata watu wazima wasiishi" alisema Dk Mwaniki.

Aliongeza kuwa: "cha kufanya kwa sasa, ni mataifa kuweka mipango ya kuwaongeza bakteria hao na kuanzisha sheria za nchi ambazo zitaonyesha jinsi watakavyotumika kama sehemu ya mlo ili kuimarisha afya za watu."

Mbali na tafiti hizo utafiti mwingine uliofanywa hivi karibuni na Taasisi ya Taifa ya Afya nchini Marekani,(ANIH) umeonyesha kuwa bakteria wa probiotics wana uwezo wa kuzuia maambukizi ya VVU kwa watoto wakati wa kunyonyesha.

Wakati huo huo watafiti hao walisema, wanawake wenye kiasi kidogo cha asidi katika mazingira ya uke wana nafasi kubwa ya kupata maambukizi ya VVU kwa urahisi ukilinganisha na wale ambao sehemu zao hazina tatizo hilo.

Takwimu za utafiti huo zinaonyesha kuwa, asilimia 78 ya wanawake wasio na tindikali ya kutosha katika uke wanaweza kuambukizwa maradhi kwa haraka na kwamba tiba ya tatizo hilo ni kuongeza bakteria wa lactobacillus.

Habari zinasema, wanasayansi wanaendelea kushawishika kuwa matumizi ya bakteria wasio na madhara huenda ikawa ni njia nyepesi ya kuzuia maambukizi, kwa kuwaongeza bakteria hao katika vyakula kama maziwa, mtindi, sukari au hata unga tangu viwandani wakati wa uzalishaji.

HAYA MNAOTAKA KUPUNGUZA UNENE TUMIENI MAZIWA YA MTINDI NA UJI ULIOCHACHA .Source P.h.D. MziziMkavu
 
Saluti kwako mkuu mzizi mkavu.
Hivi haiwezekan mkuu ukaandika kitabu au ungeanzisha hata blog yako ili hizi mambo zoote uziweke sehemu 1 ??

Mzizi mkavu unapatikana wapi? mkoa/wilaya gan??
Vip mkuu unaofisi??

Hakika kama ungekuwa ni mchungaji na unadin yako basi mim ni muumin wako mamba 1.

thread na posta zako huwa zinaniteka na kunikamata sana..
shukran sana mkuuuu MUNGU akuzidishie.
 
Saluti kwako mkuu mzizi mkavu.
Hivi haiwezekan mkuu ukaandika kitabu au ungeanzisha hata blog yako ili hizi mambo zoote uziweke sehemu 1 ??

Mzizi mkavu unapatikana wapi? mkoa/wilaya gan??
Vip mkuu unaofisi??

Hakika kama ungekuwa ni mchungaji na unadin yako basi mim ni muumin wako mamba 1.

thread na posta zako huwa zinaniteka na kunikamata sana..
shukran sana mkuuuu MUNGU akuzidishie.
 
Mkuu haswa kwenye formula ya less carlories intake =high calories out put watu wengi wanakosea sana kama ulivoelezea uzito hauwezi pungua tu kwa kujinyima kula inabidi uzingatie formula angali chakula chenye less calories wala si chakula chenye calories nyingi Na pia uzingatie vyakula vyenye bad fat mfano nyama . Jitaidi kutumia pia hata karanga huwa zinapunguza appetite ya kula kwa hiyo inakupunguzia calories intake , asali kama mkuu alivoeleza hapo juu , mazoezi yana ongeza metabolic activities nakufanya calories nyingi kupotea yani output inaongezeka, maji ya moto yanayeyusha mkusanyiko wa cholesterol na pia ya yana increase metabolic rate ya mwili hakikisha asubuhi unakunywa glass nne za maji ya uvuguvugu ,kabla hujala kunywa glass moja na baada ya kula kunywa glass moja kwa kila mlo na jioni unapoenda kulala kunywa glass nne. Utaona afya yako inavyobadilika Asante mzizi mkavu elimu yako inatusaidia sana
 
Mzizi wewe kiboko, nakuaminia kwa mambo ya diet

Mzizi mimi sio mnene kihiivyo, ila tumbo kwakweli ni kubwa, yaani baada ya kupata baby tumbo limegoma kabisa, nimeshajaribu kufanya vitu vingi lakini wapi, nitajaribu kufanya ulivyoshauri kwenye ile thread yako nyinginne maybe nitafanikiwa

Big up MziziMkavu
 
You must be a dietician. Following up all those diet related topics.

Thanx for the tips.
 
How does it do that? I need to understand it more because am weighing 120kg and my stomach is too big for more food to get in
 
Tuna matatizo ya unene ila hizi dawa za kusubiri nusu saa huo muda haupo. Wewe ungeenda mbali zaidi kwa kuandaa huo mchanganyiko, weka kwenye chupa na kutuuzia. Au wewe ni wale wa allowance za serikali?
 
kila asubuhi kabla ya kula chochote kile,huwa nakula asali,mdalasini,pamoja na maji ya uvugu vugu,ila usiku nilikuwa sijui.nitaanza rasmi leo kabla ya kulala.
 
kila asubuhi kabla ya kula chochote kile,huwa nakula asali,mdalasini,pamoja na maji ya uvugu vugu,ila usiku nilikuwa sijui.nitaanza rasmi leo kabla ya kulala.ila glasi 4 za maji kwa mkupuo siwezi,hunywa glasi moja tu
 
Back
Top Bottom