Matumizi na Faida za Asali katika afya ya binadamu

Matumizi na Faida za Asali katika afya ya binadamu

Thanx Mzizimkavu, hebu chagua avatar moja unayopenda ya kudumu, tiba zako za uhakika haifai kubadilikabadilika sura kila siku, haiendani na hadhi ya utaalam wako.
 
kote nilikonunua asali nakutana na asali feki,wapi naweza kupata asali mbichi halisi?
Kuipata Asali Safi mbichi hapo ulipo kama ni Dares-Salaam huwezi kuipata mpaka utoke nje ya mji kama vile Kibaha kwa wafugaji Asali nakushauri mkuu. Asali Safi mbichi kuipima kwake ukisha nunuwa weka ndani ya Freji basi kama ni kweli hiyo Asali sio Feki basi haito ganda lakini kama ni Asali ni feki basi itaganda kwenye Friji.
 

HAYA JAMANI TUSHINDWE WENYEWE KUPUNGUZA UZITO ILI UENDANE NA KIMO/UREFU NA HATIMAYE
BMI ZETU YAANI BODY MAX INDEX YETU IWE VIZURI





honey-and-cinnamon-against-cancer-and-arthritis.jpg



kupunguza unene ni lazima ujinyime kula ili uingize kalori kidogo lakini ufanye sana kazi au mazoezi ili utoe kalori nyingi mwilini. Baadhi ya watu wamesema kuwa wanajinyima kula lakini hawapungui. Kujinyima kula peke yake hakutoshi kama hufanyi kazi au mazoezi yoyote ya kutoa kalori nyingi kuliko unazoziingiza mwilini mwako. ASALI KATIKA KUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE Baada ya kuzingatia kanuni hiyo, hatua inayofuata ni matumizi ya asali kwa mpangilio maalum unaoweza kukusaidia kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka, wakati ukifanya mzoezi na kujinyima kula. Matumizi ya asali ni rahisi sana.

Kwanza kabisa hakikisha unapata asali halisi mbichi na siyo asali feki. Mjini kuna baadhi ya watu hutengeneza vitu mfano wa asali, matumizi ya asali hiyo hayawezi kukusaidia zaidi ya kukuletea matatizo mengine ya kiafya. Kuna kampuni na maduka (kama super markets) zinazouza asali halisi, nunua asali mbichi kutoka sehemu inayoaminika. Kula vijiko viwili (vya chai) vya asali kila siku wakati wa kwenda kulala. Katika muda wa saa nne za mwanzo za usingizi, asali itayeyusha mafuta (fat) mengi mwilini sawa na kufanya mazoezi makali. Mwanzilishi wa dayati hii ni Mike McInnes ambaye yeye ni raia wa Scottland na kitaaluma ni Mfamasia. Mtaalamu huyu aligundua kwamba wanariadha ambao hula matunda yenye virutubisho vingi vya ‘fructose’ (kama vile matunda yaliyokaushwa na asali) hupunguza mafuta mengi mwilini na huwa na stamina nyingi.

Ili kufaidi vizuri manufaa ya asali katika kukusaidia kupunguza unene na mwili kuupa nguvu, ni vizuri ukatumia asali hiyo kama ilivyoelezwa hapo juu huku ukifanya mazoezi ya viungo, angalau mara tatu kwa wiki. Ni lazima ieleweke kwamba vitu vitatu lazima vifanyike kwa pamoja ili kupunguza unene kama unavyokusudia. Kitu cha kwanza ni kula vyakula sahihi na kwa kiasi kidogo, pili kula asali halisi na mbichi kila siku kabla ya kulala na tatu kufanya mazoezi au kazi nzito ili kutoa kalori mwilini. Umuhimu wa asali hapa ni ule uwezo wake wa kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka ukiwa umelala na wakati huo huo kuupa mwili stamina.

ASALI NA MDALASINI Mchanganyiko mwingine ambao umeelezwa kusaidia sana kupunguza uzito, ni asali na unga wa mdalasini. Mchanganyiko huu ni kama kinywaji ambapo utatakiwa kuchanganya asali, abdalasini na maji moto kisha kunywa mara mbili kwa siku. Ili kupata mchangayiko unaotakiwa, chukua nusu kijiko cha unga wa adbalasini (kijiko kidogo cha chai) kijiko kimoja cha asali (saizi ya kijiko cha chai) na kikombe kimoja cha maji yaliyochemka. Anza kuchanganya maji moto na unga wa abdalasini, koroga hadi uchanganyike vizuri kisha funika na uache muda wa nusu saa ili maji yapoe. Baada ya maji kupoa, weka asali yako kijiko kimoja kisha koroga tena hadi mchangayiko wako uwe kama kinywaji.


MDALASINI NA ASALI
Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee.
Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida.

Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora.

Kama ifuatayo:

1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}.

Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.

Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.

Katika tafiti iliyofanyika hivi karibuni na chuo kikuu kimoja huko Copenhagen, madaktari waliwapa wagonjwa 200, {syrup} mchanganyiko wa kijiko kimoja *cha chai* cha asali na kimoja cha mdalasini kila asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Asilimia 73% yao waliripoti nafuu kubwa ya maumivu yao na ongezeko katika kufanya shughuli kama kujongea na kutembea vyema.

2. kukatika kwa nywele {HAIR LOSS}
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

3. Ukungu wa miguuni {FUNGUS}
Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Shida yako itakwisha kwenye kipindi cha wiki moja.

4. Maamhukizo kwenye kihofu cha mkojo {BLADDER INFECTION}
Bilauri ya maji vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili {vya chai} vya mdalasini na kijiko kimoja {cha chai} cha asali huondoa bacteria kwenye kibofu. Unaweza ukatumia juisi ya cranberry badala ya maji ikiwa ambukizo la kibofu linakuwa sugu.

5. Maumivu ya jino {TOOTHACHE}.
Changanya sehemu tano za asali, na sehemu moja ya mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.
Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka.

6. Vidonda vitokanavyo kwa mgonjwa kulala kwa muda mrefu {CANKER
SORES}.
Saladi ya kupaka vidonda iliyochanganywa na asali pamoja na mdalasini kwenye chai ya raspberry
nyekundu ni dawa nzuri ya kuondoa maumivu makali ya canker sores.​
 
Thanks!!! Kama sio a bother unaweza kutuambia haswa ni maduka yepi yenye asali mbichi isiyochakachuliwa? Maana huo nao ni mtihani. Au itakuwa promo?
 
tangawizi.jpg
Tangawizi

KARIBU msomaji katika toleo letu hili la leo, ili kujua namna ya kutumia tiba mbadala kuokoa maisha.
Leo tutazungumzia faida na matumizi ya asali, zao muhimu linalopatikana nchini Tanzania katika mikoa ya Tabora, Singida na Dodoma.

Asali ina manufaa mengi mojawapo ikiwa ni kusaidia kupunguza uzito. Mtumiaji huweka kijiko kikubwa kimoja ndani ya maji ya moto na kunywa kila siku asubuhi. Hii pia humsaidia kupunguza kitambi.


Pili, asali husaidia kutibu vidonda vya tumbo. Mtumiaji anaweza kunywa kijiko kikubwa kimoja asubuhi, mchana na jioni. Kama hiyo haitoshi, asali pia - hasa ile ya nyuki wadogo - husaidia kutibu kikohozi kwa watoto na wakubwa.

Wakati mwingine baadhi ya watumiaji huchanganya na kiini cha yai na kutengeneza mkorogo unaonyeshwa watoto. Kumbuka kuwa ni vema mkorogo huo ukatumika siku hiyo hiyo.

Pamoja na matumizi hayo, asali pia husaidia pale inapotokea mtu ameungua kwa moto. Basi ni vema ikapakwa mara moja wakati mgonjwa akielekea hospitali kwa matibabu zaidi. Waweza pia kupaka na yai bichi lililovunjwa kama unalo.


Kwa ndugu zangu akina dada na akina mama, asali pia hutumika kwa ajili ya kufanyia steaming ya nywele. Ukienda nayo saloon wataalamu watakusaidia bila kusahau kuongeza mng’aro wa ngozi ya mtumiaji iwapo anatumia.


Labda niseme kuwa katika nyakati za hivi karibuni kumekuwa na tatizo sana la kisukari linaloathiri nguvukazi ya taifa. Tatizo hili pia linaweza kuepukwa kwa kiwango fulani kwa mtumiaji wa chai na kahawa, kuweka asali badala ya sukari katika vinywaji hivyo.

Vile vile badala ya kupaka jamu kwenye mkate, kwa wenzangu wenye shida ya uzito mkubwa waweza kuweka asali. Kumbuka si tu utaburudika bali pia unatibu shida za kiafya. Ikumbukwe kuwa matumizi makubwa ya sukari hayana tija sana kwa mwili, hivyo ni bora kukinga kuliko tiba kwa sababu ni ghali.

Hivyo basi, ni vema wanafamilia mkajitahidi kuhakikisha kuwa mnakaa na asali nyumbani kama huduma ya kwanza. Asali inayopatikana katika maduka mbalimbali au katika vibanda maalumu vya uuzaji asali pia inafaa.

Kiungo kingine kilicho na manufaa ni tangawizi. Tangawizi si tu hutibu magonjwa mbalimbali bali pia ni kiburudisho. Mathalani, uwapo na

mafua makali na kikohozi, osha na kisha twanga tangawizi na uichemshe katika maji kwa muda mrefu.

Unaweza kuweka majani ya chai au maziwa na kisha kunywa taratibu ikiwa ya moto. Fanya hivyo kwa siku mbili na mafua na homa hushuka> Ila maumivu yakizidi pata ushauri wa kitabibu.

Faida nyingine ya tangawizi ni kurekebisha matumizi ya kina mama katika zile siku ngumu. Mathalani, iwapo tarehe zinabadilika mara kwa mara unaweza kutumia kurekebisha mwenendo wa siku hizo muhimu.

Vile vile, tangawizi hutumika kulainisha nyama wakati inapotwangwa na kuwekwa wakati wa kuchemsha kabla ya kukaanga au kuunga mchuzi. Kiungo hiki si tu hulainisha nyama bali pia huongeza ladha ya chakula husika.

Tiba nyingine mbadala ni pamoja na mchicha ambao unaweza kuoshwa na maji salama na kisha kutwangwa katika kinu na kuweka maji salama kidogo na kuchuja. Juisi yake huongeza damu kwa kasi ya ajabu.


Juisi hii hutakiwa kunywewa mara moja na si kuwekwa kiporo. Hii inaweza kutumika pia na watoto ambao wengi hawapendi kula mboga za majani kwa madai ya kwamba wao si sungura.


Na kuhusu suala la kiporo japo ni chakula cha kawaida, lakini kushindwa kuweka mahali penye ubaridi wa kutosha huweza kufanya chakula hicho kuwa sumu. Ni vema kiporo cha wali, kwa mfano, kikapashwa moto wa kutosha na ikiwezekana kuweka mafuta kidogo na maji ili kujiridhisha.


Mara nyingi watumiaji wa viporo wamejikuta wakianza kuhara na mara wafikapo hospitalini huambiwa ni ‘food poisoning’ (sumu itokanayo na chakula), nao hudhani wamewekewa sumu wakati sumu wanakuwa wamejipa wenyewe katika viporo vya ubwabwa, maharage na vinginevyo.


Ikumbukwe pia kuwa moja ya vyakula vyenye sumu kali ni samaki iwapo atakuwa ameanza kuoza, basi mtumiaji atarajie kuwa tumbo litaleta mageuzi makubwa yatakayomfanya aende kujisaidia haja ndogo mara nyingi.

Hivyo wasomaji, kuweni makini na matunzo ya vyakula vilivyopikwa ili kukwepa tatizo hili. Kama ilivyo ada, maumivu yakizidi pata ushauri wa kitabibu.



image.jpg

ASALI

 
NIMEYAPENDA MAWAZO YAKO MKUU, MARA NYINGI TUNAHITAJI MAWAZO PEVU KAMA HAYO KWANI YANATUSAIDIA SANA SISI ZOTE NA TUKUMBUKE KWA SASA MARADHI IMEKUWA NI SEHEMU YA MAISHA YETU. BIG UP MKUU.:nod:
 
kiukweli nimependa mawazo hayo.naombeni wenye kujua njia mbadala Za kupunguza KITAMBI aniambie maana umri wangu ni mdogo pia kiwango changu cha uwanjani kinashuka siku hadi siku.tafadhali nisaidieni
 
Back
Top Bottom