Matumizi sahihi ya Dabo indiketa, gia L,2,3 na O/D katika gari za Automatic

Asante kwa somo , ila sijui sijakuelewa vizuri, ina maana 2,3 na L zote zinafanya kazi moja? najua mojawapo ni kama unapita sehemu ambayo kuna utelezi, nyingine kwenye mteremko n.k naomba ufafanuzi tafadhali

Habari Debora, hapana labda nikujibu Kwa swali.

Ina maana katika manual transmission 1,2,3,4,5 na 4WD zinafanya kazi moja?

Jibu ni hapana maana kila gia inasehemu na matumizi yake ndo maana unaanza na 1 baadae mpaka 5 na si ajabu usitu hata 4wd kama hujakwamwa au labda unapnda mlima mkali hasa maporini (watu wa site wataelewa naongea nini) maana kama gari ni manual unaweza ukaondokea hata namba 5 ila wakati 4wd iko on

Zaidi ni Kuwa Kwa kadri namba ya gia inavyozidi Kuwa kubwa ndo uwezo au nguvu ya gia inapungua.


alfredmkohiatgmaildotcom
 
Ebwana ahsante sana kwa kututoa matongotongo, nimejifunza vitu vizuri kwa kweli....!pamoja sana kaka..!
 

Haha mkuu hyo english lol
 

Pia inafaa ieleweke kwamba hizo RPM mara nyingi kama siyo mara zote kutegemeana na gari, utaona katika ile circle yake namba 1, 2, 3, 4....... na katikati ya hiyo circle kuna x1000rpm. Maana yake ni 1x1000rpm, 2x1000rpm nk. Driving nzuri usivuke 3x1000rpm.
 
Ukiisha weka D na ukaanza kuondoka na huna haraka na pia una budget ya mafuta basi hakikisha OD taa yake ktk dashboard imezima na rpm haizidi kwenye 2 (2000rpm) na inapotaka kuzidi au imezidi kidogo maana yake gia box inataka kuongeza gia mf toka 4 kwenda 5 au 3 kwenda 4 na kwa kawaida gia 4 na tano zinaongezeka/ingeji rpm inapofika 3 (3000rpm) ila kwa sababu unataka kusave mafuta na hautaki speed kubwa basi unachofanya ni kulegeza kwa mbali sana pedal ya mafuta kwa sekunde 1.5 au 2 hivi then unaongeza mafuta huku unaangalia rpm yako, matokeo yake gia itaongezeka na rpm itashuka chini ya 2 (2000rpm), hili linawezekana kwa gia kuanzia 3 hadi 5.

Bad news to fuel stations hahahaha...!!!

My next article will be on how to use "Air Conditioning" effectively...kaa mkao wa kula
 

Mkifata ushauri huu uhai wa gearbox zenu utakuwa mdogo sana.
 
Kiongozi somo lako nimelipenda sana na bila shaka limeleta manufaa kwa wana jf wengi asante sana kwa darasa huru. Mimi naendesha both manual na automatic effectively ila nikiwa naenda safari ndefu napenda saana kuendesha manual cause inakukeep bussy na nahisi kama ni effective sana katika mazingira yoyote ya barabara. nikiwa dar napenda kuendesha automatic kutokana na folen. swali kidogo! hivi ukibadilisha mafla na kuweka zile zenye ngurumo kubwa na kupiga kelele kama gari za mashindano, kuna athari zozote injini?
 
mkuu multmandalin, kwa haraka wewe unaonekana huna msaada! kwa nn u criticize mafundisho ya akohi bila ya kuonyesha mapungufu yake? Somo hili nimelipenda sana kwa sababu binafsi kama mimi natumia manual kwa muda mrefu sanana sijawahi kutumia automatic hata mara moja! na hii ni kwa watu wengi hivyo hili suala kuwa janga kwa watu wengi kwani siku hizi auto kwenye gari ndiyo fasheni namagari mazuri siku hizi mengi ni auto! kwa hiyo kwangu mm nashukuru sana lakini pia na wewe tueleze kama kuna sehemu jamaa yetu kakosea sehemu! iku njema!!
 
Last edited by a moderator:

Asante kwa somo, mimi nina tatizo moja, ninajua kuendesha gari ila ninaogopa kuendesha kwenye highway, ninapopishana na magari huwa napunguza mwendo. Natakiwa nifanyeje ili ku overcome hili tatizo? Ushauri please
 
Mkuu akohi, tuelezee na Yale maandishi ya kijani yanayoandika kwenye dashboard 'ECONO'

Ukiona taa ya kijani imewaka na nino "ECONO" liasomeka maana yake ni kuwa hapo gari ya inatumia vizuri mafuta na neno linamaana "ECONOMICAL" wanafupisha tu. which means taa ikizima basi inamaana ulaji wa mafuta unaongezeka pia na hii kutokea hasa ukizidi RPM 3000 (RPM=Revolution Per Minute) inamaana mzungo wa injini ya gari kwa muda wa dakika moja
 
Mkuu nami nashukuru sana kwa somo hili murua, hakika nmevuna mengi, ila gari yangu mimi haina gear "L" wala "3", ina 1, 2 na D. Hii ni sawa au kwangu ni unique?


hiyo 1 ndo sawa na L kwa maana ukiweka 1 haitaingiza gear nyingine, vivo hivyo ukiweka 2 na hutumika unapokuwa umekwama kwenye mchanga au tope
 
Asante kwa somo, mimi nina tatizo moja, ninajua kuendesha gari ila ninaogopa kuendesha kwenye highway, ninapopishana na magari huwa napunguza mwendo. Natakiwa nifanyeje ili ku overcome hili tatizo? Ushauri please

Hali hii humtokea kila mtu hasa napokuwa hajazoea lakini cha msingi ni kujenga kujiamini tu na hakikisha unabaki upande wako na endesha kana kwamba uko peke yako njia nzima wala usijenge hofu maana itakupotezea kujiamini na zaidi endelea kufanya mzoezi
 
Haya Mkuu kuna kitu kinaitwa Cruise Control kipo kwenye steering Hiyo initwa cruise Control... unaiwasha then ukifika speed yoyote above 45km/h na kukisukuma chini (set) gari inamaintain hiyo speed bila wewe kukanyaga accelerator.. na ukitaka pandisha speed unakapandisha juu to +RES.. gari inakuwa inakwenda bila ule mngurumo wa kukanyaga wese kama ndege vile
 

Umenena vizuri, nadhani watanzania tuzidi kumuomba Mungu atuondolee hii roho ya kukosoa kosoa hata pasipositahiri ili muradi tu ukosoe, ni vizuri kusahihisha na kusaidiana
 
Asante kwa kuniulizia swali hilo. Ila mimi huwa sibonyezi hicho kitufe hivyo huwa hiyo taa haiwaki. Sijui kama huwa niko sahihi au la!

Ni vizuri muda wote unaendesha gari huku taa ya OD imezima, maana yake ni kuwa gear box itakuwa na uwezo wa ku ingage hadi namba tano au sita, lakini OD ikiwaka maana yake gari itakomea gear namba 4 tu ambapo ualaji wa mafuta utaongezeka lakini pia engine itapiga kelele sana hasa ukiwa speed kubwa na zaidi unaichosha engine
 
Sema inafaa kwa barabara ambayo hamna kusimama simama au kona kali..


Sahihi kabisa, CControl inasaidia sana hasa unapokuwa Off Road maana ukiisha ingage, katika speed unayotaka basi huna haja ya kukanyaga mafuka, so utakuta hata mwili ume relax, japo pia ina option ya kuongeza na kupunguza speed hapo hapo kwenye steering kwa alama ya + kwa maana ya kuongeza au - kwa maana ya kupunguza speed na hii utaitumia zaidi either kwenye kona au unapotaka kupunguza kwendo maana si kila muda ukanyage break, so unachofanya ni kubonyeza alama - kwa idadi ya speed unayotaka, sijui gari yako maana kuna ambazo kila kubonyeza inaongeza au kupuza speed 5 na zingine speed 10 na zingine speed 20
 
Mkuu kwa hiyo kwenye njia panda unatakiwa uwashe nn wakati unaenda moja kwa moja kama sio hizo hazard light?

Hutakiwi kuwasha chochote, Hazard huwashwa unapokuwa na dharula tu hasa main road
 
Mkuu nna kigari changu Auto kimeandikwa 4WD lkn sioni sehemu yoyote ya Ku activate. Always huwa nafikiri hiyo L ndo sehemu ya ku activate hiyo four wheel. Na hii nilipata nguvu baada ya kuiweka hiyo L na kuona gari haibadirishi gia, iko constant kwenye gia Moja. Je nipo sahihi juu ya hilo?
 
Hakuna kitu kwenye gari kinaitwa 'dabo indiketa', nafikiri ulimaanisha HAZARD LIGHT, but YES, they are for emergency as the name describes. Waendesha magari wasio madereva huwasha kwenye njia panda wakidhani ni kiashiria cha kwenda moja kwa moja.

Asante kwa maelezo mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…