Matumizi sahihi ya Dabo indiketa, gia L,2,3 na O/D katika gari za Automatic

Matumizi sahihi ya Dabo indiketa, gia L,2,3 na O/D katika gari za Automatic

Asante kwa somo , ila sijui sijakuelewa vizuri, ina maana 2,3 na L zote zinafanya kazi moja? najua mojawapo ni kama unapita sehemu ambayo kuna utelezi, nyingine kwenye mteremko n.k naomba ufafanuzi tafadhali

Habari Debora, hapana labda nikujibu Kwa swali.

Ina maana katika manual transmission 1,2,3,4,5 na 4WD zinafanya kazi moja?

Jibu ni hapana maana kila gia inasehemu na matumizi yake ndo maana unaanza na 1 baadae mpaka 5 na si ajabu usitu hata 4wd kama hujakwamwa au labda unapnda mlima mkali hasa maporini (watu wa site wataelewa naongea nini) maana kama gari ni manual unaweza ukaondokea hata namba 5 ila wakati 4wd iko on

Zaidi ni Kuwa Kwa kadri namba ya gia inavyozidi Kuwa kubwa ndo uwezo au nguvu ya gia inapungua.

alfredmkohiatgmaildotcom
 
Ebwana ahsante sana kwa kututoa matongotongo, nimejifunza vitu vizuri kwa kweli....!pamoja sana kaka..!
 
Katika Over Drive switch kuna only two Alternatives, put it own on ur own consent and put it off. Katika dashboard ukiona O/D off, basi ujue iko off, sio kwamba inskualert je wataka kuizima? No, it dont alert you, there is no YES or NO option wakati wa kuieka off

Haha mkuu hyo english lol
 
Asante sana mkuria Kwa Kuwa mkweli na muwazi kitu ambacho wengi wetu hatukubali kusema Kuwa sikuwa najua namna ya ku endesha hizi autos na hata Mimi Nina marafiki, ndugu jamaa wengi ambao siku zote huamini Kuwa wanjua kila kitu, anyways ni ubinadamu, nirudi ktk swali lako la msingi kuhusu RPM ni kwamba inamaanisha Revolution per Minute ambayo maana yake halisi ni mzunguko wa injini husika Kwa dakika 1 sasa ukiona iko kwenye 1000rpm maana yake injini inazunguka Mara hizo ndani ya dakika 1 na si gari zote hasa za zamani ambazi dashboard yake ina onyesha RPM, ni makosa maana ice ndo inakusaidia kujua namna ya kusave fuel concerption japo wengi hasa mafundi huskiliza muunguruno wa injini then can Tel Kuwa silencer iko juu ipunguzwe au iko chini iongezwe.

Ndio huna haja ya kusimama ili ubadilishe toka D kwena L, 2,3 au kinyume chake ila hakikisha speed sin zaidi ya 40au 60kph

alfredmkohiatgmaildotcom

Pia inafaa ieleweke kwamba hizo RPM mara nyingi kama siyo mara zote kutegemeana na gari, utaona katika ile circle yake namba 1, 2, 3, 4....... na katikati ya hiyo circle kuna x1000rpm. Maana yake ni 1x1000rpm, 2x1000rpm nk. Driving nzuri usivuke 3x1000rpm.
 
Ukiisha weka D na ukaanza kuondoka na huna haraka na pia una budget ya mafuta basi hakikisha OD taa yake ktk dashboard imezima na rpm haizidi kwenye 2 (2000rpm) na inapotaka kuzidi au imezidi kidogo maana yake gia box inataka kuongeza gia mf toka 4 kwenda 5 au 3 kwenda 4 na kwa kawaida gia 4 na tano zinaongezeka/ingeji rpm inapofika 3 (3000rpm) ila kwa sababu unataka kusave mafuta na hautaki speed kubwa basi unachofanya ni kulegeza kwa mbali sana pedal ya mafuta kwa sekunde 1.5 au 2 hivi then unaongeza mafuta huku unaangalia rpm yako, matokeo yake gia itaongezeka na rpm itashuka chini ya 2 (2000rpm), hili linawezekana kwa gia kuanzia 3 hadi 5.

Bad news to fuel stations hahahaha...!!!

My next article will be on how to use "Air Conditioning" effectively...kaa mkao wa kula
 
Dabo indiketa inashauriwa itumike wakati una dharula kubwa mf: Ajari au gari Mbovu maana lengo lake ni kuwataarifu madereva wenzako kuwa gari yako inatatizo so wapite kwa uangalifu zaidi lakin utakuta wengi wetu tunatumia visivyo mf; katika kupita njia panda au ukipaki pembezoni mwa barabara. Pia niongezee kuna ambao aki over take gari anawasha indiketa ya kulia (hiyo sawa kabisa ila sasa unapotaka kurudi upande wako wa kushoto hunahaja yak u indiketa tena unless kama kuna gari nyuma yako na iko jirani sana sio
Hata uko pekee yako unawasha indiketa tu.

Katika gari za Automatic kuna gia za L, 2, 3 na O/D.
Kwanza ujue kabisa katika hali ya kawaida gari yako inapaswa kuwa katika D kwa maana ya Drive na hii inategemeana na mazingira ya barabara na hali yali ya hewa kama ni nzuri ila 2, 3 hutumika tu pale unapokuwa either unashuka au unapanda mlima/mteremuko mkali sana na mrefu mf’ sekenke na unataka ushuke au upande kwa speed ile ile ila isizidi 40/60 basi ndo unaruhusiwa kutumia 2, 3. Namba 2, 3 na L inamaana kuwa ina inalock gear box ili gear zisibadilike (-/+) kama ambavyo zinabadika ukiweka D na itambulike kuwa unaweza kubadili toka D kwenda 2 au 3 wakati wowote gari inapokuwa katika mwendo ila hakikisha usiwe speed zaidi ya 40/60 maana kinachofanyika ni kwamba D inasababisha sahani (disks) zilizomo ndani ya gearbox kufanya gazi nah ii upelekea ile hydrolic iliyomo kupata joto linalotoka katika zile sahani ambalo joto lile husababisha gear box kutokuwa na nguvu ile ile (constant velocity) na ndo maana ukiweka 2, 3 au L gear box inakuwa kwenye lock na sahani hazisuguani maana inakuwa inatumika sahani/disk moja tu kwa hiyo inasaidia ile hydrolick kupoa pia na ndo maana gari huongeza nguvu kwa ghafla. L inatumika pale unapokuwa either umekwama au unavuta gari jingine au tera ila inapaswa itumike kwa muda mfupi sana maana inanguvu sana na pia inaongeza ulajo wa mafuta, so kama ukiishatoka katika mkwamo na unaona bado barabara si nzuri labda utelezi au unavuta mzigo kwa mwendo mrefu basi unaweka 2 au 3 na wakati huohuo unaweza kuweka hata D kama hali ya njia na mzigo vinaruhusu na unaweza kuongeza walau speed 40/60 au zaidi kama utaweka D. kwa maana rahisi zaidi kwamba 2,3,na L inafanya kazi kama gari ya Manual nah ii inakuwa rahisi kwa yeyote ambaye anafahamu kuendesha manual.

Over Drive inatumika pale gari inapokuwa speed zaidi ya 60/80 kutegemeana na aina ya gari na hili hutokea bila wewe kujua maana gari yenyewe ndo inafanya nan do maana unashauriwa iwe on muda wote kusudi gari ichague ni wkati gani iweke on au of maana uukiwa chini ya 60/80 hata kama umeweka on bado inakuwa haifanyi kazi.
Cha mwisho ndugu zangu ni kwamba OD unaweza kuitumia kama break/stop engine hasa unapokuwa zaid ya 80 na wakati huo iko ON yaan katika dashboard taa ya OD izime ikiwaka maana yake iko OFF, basi ili upunguze mwenda kwa haraka unachofanya ni kuweka OFF na wakati huo unakanyaga break taratibu utaona mwenyewe gari lako linavyopunguza mwendo tartibu na wakati mwingine si lazima ukanyage break, we iweke OFF tu halafu toa mguu katika pedal ya mafuta gari lazima li slow down na kama lilikuwa ni tuta na umeliisha lipita basii iweke tena ON ongeza mafuta auu unaweza kuweka 2 au 3 ili gari ianze kwa kasi zaidi na ikiisha changanya basi rudi kwenye D na endelea kama kawaida.

Tahadhari: never ever kata kona wakati uko speed kubwa na gear namba tano (Kwa manual) au rpm iko 3000 Kwa automatic hii husababisha kupitiliza maana gari inakuwa nyepesi sana. Hakikisha ume slow down mpaka gia namba nne na break kidogo na Kwa autimatic either uweke 2 au 3 ila lazima weka OD off na break kidogo

Sijui kama ntakuwa nimeeleweka maana Kiswahili na lugha yetu ila mmh …!

Mkifata ushauri huu uhai wa gearbox zenu utakuwa mdogo sana.
 
Kiongozi somo lako nimelipenda sana na bila shaka limeleta manufaa kwa wana jf wengi asante sana kwa darasa huru. Mimi naendesha both manual na automatic effectively ila nikiwa naenda safari ndefu napenda saana kuendesha manual cause inakukeep bussy na nahisi kama ni effective sana katika mazingira yoyote ya barabara. nikiwa dar napenda kuendesha automatic kutokana na folen. swali kidogo! hivi ukibadilisha mafla na kuweka zile zenye ngurumo kubwa na kupiga kelele kama gari za mashindano, kuna athari zozote injini?
 
mkuu multmandalin, kwa haraka wewe unaonekana huna msaada! kwa nn u criticize mafundisho ya akohi bila ya kuonyesha mapungufu yake? Somo hili nimelipenda sana kwa sababu binafsi kama mimi natumia manual kwa muda mrefu sanana sijawahi kutumia automatic hata mara moja! na hii ni kwa watu wengi hivyo hili suala kuwa janga kwa watu wengi kwani siku hizi auto kwenye gari ndiyo fasheni namagari mazuri siku hizi mengi ni auto! kwa hiyo kwangu mm nashukuru sana lakini pia na wewe tueleze kama kuna sehemu jamaa yetu kakosea sehemu! iku njema!!
 
Last edited by a moderator:
Dabo indiketa inashauriwa itumike wakati una dharula kubwa mf: Ajari au gari Mbovu maana lengo lake ni kuwataarifu madereva wenzako kuwa gari yako inatatizo so wapite kwa uangalifu zaidi lakin utakuta wengi wetu tunatumia visivyo mf; katika kupita njia panda au ukipaki pembezoni mwa barabara. Pia niongezee kuna ambao aki over take gari anawasha indiketa ya kulia (hiyo sawa kabisa ila sasa unapotaka kurudi upande wako wa kushoto hunahaja yak u indiketa tena unless kama kuna gari nyuma yako na iko jirani sana sio
Hata uko pekee yako unawasha indiketa tu.

Katika gari za Automatic kuna gia za L, 2, 3 na O/D.
Kwanza ujue kabisa katika hali ya kawaida gari yako inapaswa kuwa katika D kwa maana ya Drive na hii inategemeana na mazingira ya barabara na hali yali ya hewa kama ni nzuri ila 2, 3 hutumika tu pale unapokuwa either unashuka au unapanda mlima/mteremuko mkali sana na mrefu mf’ sekenke na unataka ushuke au upande kwa speed ile ile ila isizidi 40/60 basi ndo unaruhusiwa kutumia 2, 3. Namba 2, 3 na L inamaana kuwa ina inalock gear box ili gear zisibadilike (-/+) kama ambavyo zinabadika ukiweka D na itambulike kuwa unaweza kubadili toka D kwenda 2 au 3 wakati wowote gari inapokuwa katika mwendo ila hakikisha usiwe speed zaidi ya 40/60 maana kinachofanyika ni kwamba D inasababisha sahani (disks) zilizomo ndani ya gearbox kufanya gazi nah ii upelekea ile hydrolic iliyomo kupata joto linalotoka katika zile sahani ambalo joto lile husababisha gear box kutokuwa na nguvu ile ile (constant velocity) na ndo maana ukiweka 2, 3 au L gear box inakuwa kwenye lock na sahani hazisuguani maana inakuwa inatumika sahani/disk moja tu kwa hiyo inasaidia ile hydrolick kupoa pia na ndo maana gari huongeza nguvu kwa ghafla. L inatumika pale unapokuwa either umekwama au unavuta gari jingine au tera ila inapaswa itumike kwa muda mfupi sana maana inanguvu sana na pia inaongeza ulajo wa mafuta, so kama ukiishatoka katika mkwamo na unaona bado barabara si nzuri labda utelezi au unavuta mzigo kwa mwendo mrefu basi unaweka 2 au 3 na wakati huohuo unaweza kuweka hata D kama hali ya njia na mzigo vinaruhusu na unaweza kuongeza walau speed 40/60 au zaidi kama utaweka D. kwa maana rahisi zaidi kwamba 2,3,na L inafanya kazi kama gari ya Manual nah ii inakuwa rahisi kwa yeyote ambaye anafahamu kuendesha manual.

Over Drive inatumika pale gari inapokuwa speed zaidi ya 60/80 kutegemeana na aina ya gari na hili hutokea bila wewe kujua maana gari yenyewe ndo inafanya nan do maana unashauriwa iwe on muda wote kusudi gari ichague ni wkati gani iweke on au of maana uukiwa chini ya 60/80 hata kama umeweka on bado inakuwa haifanyi kazi.
Cha mwisho ndugu zangu ni kwamba OD unaweza kuitumia kama break/stop engine hasa unapokuwa zaid ya 80 na wakati huo iko ON yaan katika dashboard taa ya OD izime ikiwaka maana yake iko OFF, basi ili upunguze mwenda kwa haraka unachofanya ni kuweka OFF na wakati huo unakanyaga break taratibu utaona mwenyewe gari lako linavyopunguza mwendo tartibu na wakati mwingine si lazima ukanyage break, we iweke OFF tu halafu toa mguu katika pedal ya mafuta gari lazima li slow down na kama lilikuwa ni tuta na umeliisha lipita basii iweke tena ON ongeza mafuta auu unaweza kuweka 2 au 3 ili gari ianze kwa kasi zaidi na ikiisha changanya basi rudi kwenye D na endelea kama kawaida.

Tahadhari: never ever kata kona wakati uko speed kubwa na gear namba tano (Kwa manual) au rpm iko 3000 Kwa automatic hii husababisha kupitiliza maana gari inakuwa nyepesi sana. Hakikisha ume slow down mpaka gia namba nne na break kidogo na Kwa autimatic either uweke 2 au 3 ila lazima weka OD off na break kidogo

Sijui kama ntakuwa nimeeleweka maana Kiswahili na lugha yetu ila mmh …!

Asante kwa somo, mimi nina tatizo moja, ninajua kuendesha gari ila ninaogopa kuendesha kwenye highway, ninapopishana na magari huwa napunguza mwendo. Natakiwa nifanyeje ili ku overcome hili tatizo? Ushauri please
 
Mkuu akohi, tuelezee na Yale maandishi ya kijani yanayoandika kwenye dashboard 'ECONO'

Ukiona taa ya kijani imewaka na nino "ECONO" liasomeka maana yake ni kuwa hapo gari ya inatumia vizuri mafuta na neno linamaana "ECONOMICAL" wanafupisha tu. which means taa ikizima basi inamaana ulaji wa mafuta unaongezeka pia na hii kutokea hasa ukizidi RPM 3000 (RPM=Revolution Per Minute) inamaana mzungo wa injini ya gari kwa muda wa dakika moja
 
Mkuu nami nashukuru sana kwa somo hili murua, hakika nmevuna mengi, ila gari yangu mimi haina gear "L" wala "3", ina 1, 2 na D. Hii ni sawa au kwangu ni unique?

hiyo 1 ndo sawa na L kwa maana ukiweka 1 haitaingiza gear nyingine, vivo hivyo ukiweka 2 na hutumika unapokuwa umekwama kwenye mchanga au tope
 
Asante kwa somo, mimi nina tatizo moja, ninajua kuendesha gari ila ninaogopa kuendesha kwenye highway, ninapopishana na magari huwa napunguza mwendo. Natakiwa nifanyeje ili ku overcome hili tatizo? Ushauri please

Hali hii humtokea kila mtu hasa napokuwa hajazoea lakini cha msingi ni kujenga kujiamini tu na hakikisha unabaki upande wako na endesha kana kwamba uko peke yako njia nzima wala usijenge hofu maana itakupotezea kujiamini na zaidi endelea kufanya mzoezi
 
Haya Mkuu kuna kitu kinaitwa Cruise Control kipo kwenye steering Hiyo initwa cruise Control... unaiwasha then ukifika speed yoyote above 45km/h na kukisukuma chini (set) gari inamaintain hiyo speed bila wewe kukanyaga accelerator.. na ukitaka pandisha speed unakapandisha juu to +RES.. gari inakuwa inakwenda bila ule mngurumo wa kukanyaga wese kama ndege vile
 
mkuu multmandalin, kwa haraka wewe unaonekana huna msaada! kwa nn u criticize mafundisho ya akohi bila ya kuonyesha mapungufu yake? Somo hili nimelipenda sana kwa sababu binafsi kama mimi natumia manual kwa muda mrefu sanana sijawahi kutumia automatic hata mara moja! na hii ni kwa watu wengi hivyo hili suala kuwa janga kwa watu wengi kwani siku hizi auto kwenye gari ndiyo fasheni namagari mazuri siku hizi mengi ni auto! kwa hiyo kwangu mm nashukuru sana lakini pia na wewe tueleze kama kuna sehemu jamaa yetu kakosea sehemu! iku njema!!

Umenena vizuri, nadhani watanzania tuzidi kumuomba Mungu atuondolee hii roho ya kukosoa kosoa hata pasipositahiri ili muradi tu ukosoe, ni vizuri kusahihisha na kusaidiana
 
Asante kwa kuniulizia swali hilo. Ila mimi huwa sibonyezi hicho kitufe hivyo huwa hiyo taa haiwaki. Sijui kama huwa niko sahihi au la!

Ni vizuri muda wote unaendesha gari huku taa ya OD imezima, maana yake ni kuwa gear box itakuwa na uwezo wa ku ingage hadi namba tano au sita, lakini OD ikiwaka maana yake gari itakomea gear namba 4 tu ambapo ualaji wa mafuta utaongezeka lakini pia engine itapiga kelele sana hasa ukiwa speed kubwa na zaidi unaichosha engine
 
Sema inafaa kwa barabara ambayo hamna kusimama simama au kona kali..
Haya Mkuu kuna kitu kinaitwa Cruise Control kipo kwenye steering Hiyo initwa cruise Control... unaiwasha then ukifika speed yoyote above 45km/h na kukisukuma chini (set) gari inamaintain hiyo speed bila wewe kukanyaga accelerator.. na ukitaka pandisha speed unakapandisha juu to +RES.. gari inakuwa inakwenda bila ule mngurumo wa kukanyaga wese kama ndege vile

Sahihi kabisa, CControl inasaidia sana hasa unapokuwa Off Road maana ukiisha ingage, katika speed unayotaka basi huna haja ya kukanyaga mafuka, so utakuta hata mwili ume relax, japo pia ina option ya kuongeza na kupunguza speed hapo hapo kwenye steering kwa alama ya + kwa maana ya kuongeza au - kwa maana ya kupunguza speed na hii utaitumia zaidi either kwenye kona au unapotaka kupunguza kwendo maana si kila muda ukanyage break, so unachofanya ni kubonyeza alama - kwa idadi ya speed unayotaka, sijui gari yako maana kuna ambazo kila kubonyeza inaongeza au kupuza speed 5 na zingine speed 10 na zingine speed 20
 
Mkuu kwa hiyo kwenye njia panda unatakiwa uwashe nn wakati unaenda moja kwa moja kama sio hizo hazard light?

Hutakiwi kuwasha chochote, Hazard huwashwa unapokuwa na dharula tu hasa main road
 
Mkuu nna kigari changu Auto kimeandikwa 4WD lkn sioni sehemu yoyote ya Ku activate. Always huwa nafikiri hiyo L ndo sehemu ya ku activate hiyo four wheel. Na hii nilipata nguvu baada ya kuiweka hiyo L na kuona gari haibadirishi gia, iko constant kwenye gia Moja. Je nipo sahihi juu ya hilo?
 
Hakuna kitu kwenye gari kinaitwa 'dabo indiketa', nafikiri ulimaanisha HAZARD LIGHT, but YES, they are for emergency as the name describes. Waendesha magari wasio madereva huwasha kwenye njia panda wakidhani ni kiashiria cha kwenda moja kwa moja.

Asante kwa maelezo mazuri
 
Back
Top Bottom