Matumizi sahihi ya Dabo indiketa, gia L,2,3 na O/D katika gari za Automatic


Ukiweka L maana yake isibadiri gia zaidi ya namba 1, na siku zote namba 1 ndo gia yenye nguvu zaidi na ndo maana tunaitumia unapkuwa umekwama, lengo la kuweka L ni kuwa gear box isijibadirishe gia yenyewe automatically kwa kufuata RPM yake, maana kila gear ina ingia kutegemeana na mzunguko wa injini/RPM. Sasa hili linakuwa tatizo kama umekwama maana unataka gia namba moja itumike kwa nguvu zaidi ili utoke kwenye kwamo let's say wa umbali labda wa mita 100 au zaidi, ambapo ukiwe D basi unaweza kujikuta by the time RPM imefika 3000 uko gia namba 4 ambapo gari inakuwa nyepesi na haina uwezo wa kukutoa kwenye tope au mchanga.

4WD ina maana Four Wheels Drive au mengine huandikwa Full Time Four Wheels hasa kwa gari ndogo, hii inamaana muda wote inakuwa kwenye 4WD haihitaji kubonyeza chochote kwa kuiweka au kuitoa, yaana tairi zote nne zinazunguka kwa mzunguko mmoja na hii inakuwa imetengenezwa moja kwa moja toka kiwandani, uzuri wake zikuwa hazikwami hovyo hovyo na hazina usumbufu wa kuweka au kutoa 4WD, ni nzuri kwa akina mama au watoto hasa wa kike japo ulaji wake wa mafuta ni juu kidogo maana muda wote inakuwa nzito kuliko gari ambayo sio Full Time 4WD ila uzuri mwingine zinanguvu sana
 
Kwahiyo mkuu akohi kwenye dashboard ikiwaka taa ya O/D OFF = ON; na kama haipo ni sawa na O/D iko OFF??

Ikizima ndo iko ON, ikiwaka ndo iko OFF

ku prove hilo fanya hivi:

Endesha wakati taa ya OD imewaka then nenda kasi mpaka speed 60 au zaidi, utasikia muungurumo umekuwa mzito na engine inapiga kelele/vuma/vibrate sana na RPM iko juu zaidi ya 3000, maana yake uko speed lakini gear box iko namba 4 na haiwezezi kuingia gia namba tano sababu umeweka OD OFF, basi hapo weka OD ON wakati uko speed then yafuatayo utaona:-

1. RPM itashuka mpaka 2000
2. Muungurumo wa Engine utarudi normal
3. Gari ita ingage gia namba 5
4. Speed itaongezeka zaidi
5. Gari itatulia au kuacha kuvibrate na hata mkononi utaisikia imetulia
6. etc
 
Katika gari zingine kuna N/P ukipress P kwenye Dashbord inawaka POWER hii inasaidia nini na inatumikaje?


ELCT au P=Power ya kwenye dashboard kazi yake ni kuipa gari nguvu zaidi na inatumika unapotaka kumaintain speed zaidi ya 140km kwa saa au zaidi ila kufanya hivyo inabidi uwe na uzoefu wa kukimbia na kumaintan hiyo speed lakini pia kiwango cha mafuta kitaongezeka takriban mara mbili ya kawaida...hahaha

Mi naitumia sana hasa ninapokuwa nasafiri kwenda mikoani na nina haraka
 
Fuatilia nyuzi kuna sehemu nimefafanua ila si kosa japo inaweza kusababisha ajari


alfredmkohiatgmaildotcom

Kuweka N wakati uko kwenye mwendo ni hatari sana maana unakuwa wewe huiendeshi gari na ni rahisi kupoteza control maana mf ikizima gafla ni kila kitu kika jilock mf steering au break zika fail basi hapo unaweza hata kupoteza maisha
 

Well said Chief, labda kuongezea tu.

kama una balance vizuri mafuta kwa kukanyaga huku unatizama RPM isizidi 3000 pale gia inapotaka kuingia na hasa unapokuwa safairini basi utaweza kukuta taa ya ECONO inawaka uko speed 120 bila tatizo chamsingi usiwe unakanyaga mafuta kwa nguvu, kanyaga kidgo tu halafu gari yenyewe itaongeza speed taratibu unless kama unaharaka hapo ndo inabidi ukanyage mafuta mengi of which taa lazima itazim
 
Mkuu me hyo nilitumia kwa Brevis la CC 3000 Aisee Ile Gari imetulia sana yani Raha
 
Mkuu nashukuru sana kwa kuanzisha uzi huu, utakuwa umetusaidia wengi wetu. Mimi kwenye gari yangu (AUTO) kuna button mbili ambazo sijiu matumizi yake, moja imeandikwa PWR (inawezekana ikawa Power kama ulivyoeleza hapa), lakini kuna nyingine inafuatia imeandikwa MANU. Naomba unieleweshe kama unafahamu kuhusu hizi.
Pili ni kama sijakupata vizuri kuhusu matumizi ya 2 na L kwenye hizi gari za AUTO, hivi ulisema unaweza pia kuzitumia kama unashuka mteremko mkali? Asante.
 
Thanks!
 
Mkuu naomba unieleweshe kitu kimoja...ni hivi. Mimi gari yangu siku zote naendesha nikiwa nimebonyeza kile kitufe cha OD. Hivyo pale kwenye dashboard inawaka taa ya orange inasoma O/D OFF sasa hapo inamaanisha nini na je ni sawa?
Hapo unakosea. Inatakiwa kile kitaa cha o/d kizimike...
 
Alfred asante sana kwa mada yako vipi elect pwr?

 
Nimefurahi sana kuhusu double indicators. Utaona watu wengi ambao ulidhani ni wazoefu sana wa magari wakiweka hizo taa ati kuonesha wanaenda mbele kwa mbele sio kupinda. Nikajiuliza, mbpna njiani tunapita barabara nyingi tu zenye muingiliano na tunayoipita lakini hatuweki hizo indicators??
Umewafafanulia vizuri sana mkuu. Aksante kwa somo.
 
Mkuu, Unaweza ukatoka kwenye D - ukenda kwenye 3 au 2 ikitegemeana na Spidi.

L- Inatembea mpaka 60km/hr
2 - Inatembea mpaka 120km/hr
3 - Inatembea mpaka 180km/hr
4 - inatembea mpaka 240km/hr - ( ikiwa imefungwa speed gorvenor itafika 220km.hr atleast)

In that case, kama umeweka D na umefika 160 km/hr unaweza ukashift kwenda 3rd gear bila tatizo lolote, ukifanya ivi utaona gari ikiwa inaongezeka nguvu kidogo.

Ila huwezi ukatoka kwenye D wakati upo 160, ukarudi kwenye 2nd Gear, safe mechanism ya gari inatakiwa ikate mafuta at once na gari kuzima kabisa.... sijawahi kujaribu kufanya ichi kitu 😀 wala sitojaribu.... lakini in theory it is suppose to cut off fuel mpaka pale gear itakapoweza kuendana na mzunguko wa engine.

Pia some of the info unazotoa hazipo sawa kuhusu OD. Unasema kuwa unaua gari ukiwa una drive wakati OD ikiwa Off? Na pia Suala la unywaji mafuta ukoje? Kuna baadhi ya vitu ni lazima uelewe theory yake ikoje.

OD kukaa off maana yake ni kuwa hio ni normal driving mode, wewe umeekewa option ya ku OVER DRIVE the Factory set limit tu. Na hapa ndio unywaji wa mafuta unaongezeka, kwa sababu, kwanza utakuwa umejihold kwenye lower gear for a period of time without efficiently using it. Pengine wewe unakwenda 60km/hr ndio mwendo wa kila siku, Over drive for what? unapoweka on, unapunguza efficiency ya gari. Kwa sababu gari automatic wakati unaendesha, huwa inakwenda kutulia kwenye higher gear kwa ajili ya kupunguza ulaji wa mafuta, higher gear haitumii ulaji mkubwa wa mafuta kwa sababu engine inakuwa nyepesiiiii mzunguko wake. Ndio maana utaona gear zinajibadilisha RPM ikiwa somwhere between 2000-3000.

In Theory, ukibonyeza zaidi accelerator, throttle body inazidi kufunguka, hii hupelekea hewa nyingi kuingia, manake na mafuta zaidi yataingia, na maanake mzunguko wa engine utaongezeka (RPMs). Sasa ukiweka Over drive on, practical kabisa, utaona kuwa utajikuta upo kwenye lower gear kisha rpm inaongezeka, ikiongezeka rpm basi ujue kuna ongezeko la hewa na mafuta ndani ya engine. Sasa ukinambia kuwa Over drive inasaidia kuokoa mafuta hapo itabidi unieleweshe hio engine inafanya kazi vipi?

Lengo la OD, sio efficiency ya mafuta kwenye gari. Lengo lake ni kukupa more power in the lower gear. Mfano wakati upo normal driving without OD on na uko kwenye 70km/hr, mbele yako kuna gari, unataka kuipita, hii gari nayo labda ipo kwenye 60km/hr, unajaribu ku overtake, bila ya OD, utajikuta kuwa unachukua mda kumpita huyu jamaa wa mbele, bila OD unaweza kumpita, lakini itachukuwa mda, sasa unapoweka OD, wakati una overtake halafu umekanyaga mafuta, maanake unaiambia engine kuwa, give me the most power i can get with the force i push the accelerator, engine nayo inajibu kwa kushusha gear ya chini yake ili kukupa nguvu zaidi, Tena hapa itategemea how hard you press the gas pedal, what speed you are into, hio hio OD inaweza ikashift from 4th Gear to 2nd Gear straight.

I hope nimeeleweka kama kuna hitajika ufafanuzi nipo
 
Asante kwa elimu nzuri mleta mada,
Nini kazi ya ECT SNOW?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…