Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Kongamano la 8 la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu limeanza leo jijini Dar es Salaam ambapo wito ukitolewa kwa wanataaluma kuongeza umakini kukabiliana na changamoto za teknolojia mpya.
Kupitia kongamano hilo lililoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo maandalizi ya taifa kuingia kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda mojawapo ikiwa ujio wa teknolojia na athari zake chanya na hasi kwenye elimu.
Akichangia mada hiyo leo Juni 14, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma (Udom), Profesa Lughano Kusiluka ameeleza kuwa mapinduzi hayo yamekuja na changamoto ambazo zinaweza kuathiri mifumo mbalimbali ikiwemo elimu.
Amesema ili kuepuka athari hasi ni muhimu kwa wanataaluma kwenda na kasi ya teknolojia hizo ili kubaini udanganyifu unapojitokeza.
Akitolea mfano wa programu rununu ya Chat GPT amesema inatumika vibaya na wanafunzi hivyo ni muhimu kuwa walimu kuwa makini kufanya ufuatiliaji.
“Sasa hivi kuna hii Chat GPT ni teknolojia nzuri lakini matumizi yake yanaweza kuleta shida kwenye elimu yetu, huku vyuoni sasa hivi tuna shida mwanafunzi anaweza kukuletea tasnifu imeandikwa vizuri na akapata 'A' ukiifanyia tathmini utagundua wala hakustahili kupata hiyo alama.
“Hii inatufanya vyuo vikuu na sisi tuone haja ya kuwekeza ili kuzibaini tasnifu zinazofanywa kwa njia hii, tuongeze umakini kwenye tathmini. Teknolojia hizi zipo na hatuna namna ya kuzikwepa lakini tuhakikishe hazitumiki kushusha kiwango cha elimu yetu,” amesema Profesa Kusiluka.
Akizungumzia hilo Mkurugenzi wa zamani wa Costech Dk Hassan Mshinda amesema teknolojia hiyo ni tatizo kwenye elimu kwani inawawezesha wanafunzi kufanya udanganyifu.
“Mtu anaweza kuandika tasnifu nzuri kabisa ya kurasa tano ndani ya dakika tano. Hata hivyo hatuwezi kupingana na maendeleo haya lazima tuendane na kasi hiyo. Changamoto ni kwamba kama tutaenda taratibu kila siku tutakuwa nyuma lazima kazi kubwa ifanyike kuendana na mabadiliko na maendeleo haya teknolojia,” amesema.